93.7 EFM inaendeleza burudani kupitia kampeni yake ya muziki mnene bar kwa bar. Jumamosi ilikuwa zamu ya wakazi wa bunju kuongea na muziki wa 93.7 EFM. Burudani hiyo iliendeshwa na timu nzima ya EFM, iliyocheza mechi na carlfonia FC ya boko na kuwafunga magoli mawili kwa moja katika uwanja wao wa nyumbani uliopo ndani ya shule ya msingi boko. “Kwa bahati mbaya tumeshafungwa mechi tatu ila kuanzia mechi hii ni mwendo wakufunga magori ya kishujaa” alisema Dennis Ssebo mkuu wa...
UMOJA wa Ulaya na Uturuki zimekubaliana kushirikiana pamoja kukabiliana na ongezeko la wahamiaji wanaoingia barani Ulaya. Viongozi wa nchi za Umoja wa Ulaya na Uturuki walifanya mkutano wa kilele hapo jana mjini Brussels na kukubaliana kuwa na mpango wa pamoja wa kushughulikia mzozo huo licha ya kuwa bado baadhi ya masuala hayajafikiwa kikamilifu. Uturuki kwa hivi sasa inawahifadhi zaidi ya wakimbizi milioni mbili wengi wao kutoka Syria na ni mojawapo ya kituo kinachotumika na wahamiaji kuingia barani...
TAASISI isiyokuwa ya Kiserikali ya Twaweza inatarajia kuandaa mdahalo wa wagombea urais unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 0ktoba mwaka huu kwa lengo la kuwawezesha Wagombea waweze kutoa sera zao kwa Wananchi pamoja na kuruhusu Wananchi hao kuwauliza maswali Wagombea wao ili waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 Mwaka huu. Mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema kuwa hadi sasa wamepata uthibitisho wa ushiriki wa vyama vine vya siasa ambavyo ni ACT- Wazalendo , Alliance for Democratic...
ALIYEKUWA mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe ambaye alikuwa anatetea nafasi hiyo kupitia chama cha Mapinduzi(CCM), amefariki kwenye ajali ya helikopta iliyotokea jana usiku kwenye hifadhi ya wanyama ya Selous lililopo eneo la Kilombero mkoani Morogoro. Filikunjombe ni mmoja wa abiria watatu waliokuwa ndani ya chopa hiyo ambao imethibitishwa kupoteza maisha. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jerry Silaa, Meya wa Manispaa ya Ilala anayemaliza muda wake, kapteni William Silaa baba mzazi wa Jerry ndiye aliyekuwa rubani...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amekitumia Chama cha Siasa cha National League for Democracy (NLD) salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Mheshimiwa Dkt. Emmanuel Makaidi ambaye ameaga dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Lindi . Katika salamu zake hizo rais kikwete amesema kwa hakika, NLD imepoteza mhimili wake lakini pia Taifa limepoteza kiongozi mzuri na shupavu wa siasa katika kipindi ambacho alihitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote....
VIJANA wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kuwa mitandao ni jukwaa zuri lenye mitaji mingi ya biashara na endapo ubunifu utatumika vizuri kuna nafasi kubwa ya kutengeneza na kutoa ajira nyingi kwa kuwa ulimwengu unaendeshwa na TEHAMA katika Nyanja mbalimbali. Akizungumza na Efm Mjumbe wa Vijana Afrika Mashariki, na Mwenyekiti kutoka Mtandao wa Vijana Tanzania TYN Agness Mgongo amesema kuwa Vijana wa Kitanzania wanapata nafasi chache ya kushiriki katika midahalo ya kimataifa kwa kutofahamu au kuwa na matumizi sahihi...
MMOJA wa Viongozi Wakuu wa kiroho wa waislam Dhehebu la shia Ithnasheriya Tanzania SHEIKH HEMED JALALA amewataka watanzania kuendeleza mila na desturi za kistaarabu alizoziacha mwasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hasa katika kipindi hiki cha chaguzi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dare s salaam katika kumbukumbu ya mwaka mpya wa 1,437 H wa kiislamu amesema mwaka uliopita ulimwengu wa kiisalamu ulikumbana na changamoto nyingi hivyo kwa mwaka huu mpya ipo haja ya kujifunza na kujirekebisha kutokana...
BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limevishauri vyama vya siasa kuzungumza na kuwasihi wafuasi wao kutii sheria bila shuruti ili kuendeleza amani iliyopo nchini. Aidha Baraza hilo limeviomba Vyama kuwaeleza wafuasi na wapenzi wao kurudi majumbani na kuendelea na shughuli zao mara baada ya kupiga kura siku ya uchaguzi mkuu kama ilivyokuwa kwa hatua za uandikishwaji. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu...
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa ametoa wito wa kufanyika kwa mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa Umoja wa Mataifa ili kukidhi mahitaji ya sasa ya dunia. Mkapa ameyasema hayo jana katika mdahalo wa juma la Umoja wa Mataifa ambalo unakamilika leo sambamba na maadhimisho ya miaka 70 tangu kuundwa kwa umoja huo. Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa akimshukuru Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo amezindua mtambo wa kufua Umeme uliopo Kinyerezi one Jijini Dar es salaam wenye uwezo wa Megawati 150. Katika uzinduzi huo Rais Kikwete amesema kuwa uzinduzi huo ni mojawapo ya mikakati ya kufikia lengo la mpango wa maendeleo wa miaka mitano unaoishia mwakani wa kufikisha megawati 2780 ambapo hadi sasa zipo megawati 1490 na kubakia megawati 1390. Mbali na hayo amesema kuwa Tanzania inaanza mpango mpya mwakani wa kuifanya...
OFISI ya Msajili wa Vyama Vya Siasa imewaasa na kuwataka viongozi wote wa vyama vya siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi wao na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa amani. Hayo yamesemwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dares Salaam. Jaji Mutungi amesema kuwa Dhamana ya nchi ipo mikononi mwa wananchi hivyo ushawishi wowote ule wa uvunjifu wa Amani...