Global News

HUKUMU YA KIFO KWA MAGAIDI KUREJESHWA PAKISTAN
Global News

PAKISTAN imesema itaondoa marufuku ya kutolewa adhabu ya kifo katika kesi zinazohusiana na ugaidi. Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa tangazo hilo leo, siku moja baada ya wapiganaji wa Taliban kuwaua watu 141 katika shambulizi lililofanyika kwenye shule moja inayoendeshwa na jeshi. Shambulizi hilo la kigaidi lililofanyika kwenye mji wa Peshawar, ni baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Pakistan. Hukumu za kifo ziko katika amri za kitabu cha Pakistan na majaji wameendelea kutoa adhabu hiyo, lakini amri ya kusitisha adhabu...

Like
300
0
Wednesday, 17 December 2014
SIERRA LEONE KUSAKA WAGONJWA WA EBOLA NYUMBA KWA NYUMBA
Global News

RAIS Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa msako wa nyumba kwa nyumba unaanza kote nchini humo kuwatambua watu walio na ugonjwa hatari wa ebola, na amepiga marufuku biashara kufanyika siku ya Jumapili. Katika hotuba yake aliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, Rais Koroma ametoa amri ya kuzuia usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka shirika la afya Duniani WHO, Sierra Leone ni taifa ambalo limeathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa wa ebola...

Like
225
0
Wednesday, 17 December 2014
JOHN KERRY AELEZEA MCHAKATO WA UCHAGUZI ISRAEL
Global News

WAZIRI WA MAMBO ya Nje wa Marekani, JOHN KERRY, ameelezea upinzani wa nchi yake dhidi ya juhudi zozote alizodai zinahujumu mchakato wa uchaguzi wa Israel, huku akisema Marekani inatarajia kutakuwa na njia ya kuendeleza mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati na kuondoa wasiwasi wa Wapalestina. Mkutano wa KERRY umewajumuisha Mkuu wa ujumbe wa wapatanishi wa Palestina, SAEEB ERAKAT, na mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, NABIL El-ARABI. Kabla ya hapo, KERRY amekutana na Waziri Mkuu wa Israel, BENJAMIN...

Like
248
0
Wednesday, 17 December 2014
PAKISTAN BADO WAOMBOLEZA VIFO VYA WATOTO 141
Global News

Pakistan imeingia siku yake ya pili ya maziko na maombolezo, baada ya kundi la wanamgambo wa Taliban kuivamia Shule moja ya Kijeshi na kuwauwa watu 141, wengi wao watoto. Mashambulizi hayo ya kikatili zaidi kuwahi kutokea katika siku za karibuni, yamelaaniwa na viongozi na watu kadhaa mashuhuri duniani. Aidha kundi la Taliban katika nchi jirani ya Afghanistan limeyaita mauaji hayo kuwa ni ya kinyama na yasiyo na uhalali wowote kidini. Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif, ametangaza siku tatu za...

Like
275
0
Wednesday, 17 December 2014
TALIBAN WAVAMIA SHULE NA KUUA 100 PAKISTAN
Global News

TAKRIBAN watu 100 wakiwemo wanafunzi 80 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wapiganaji wa Taliban kuvamia shule moja inayosimamiwa na jeshi huko Peshawar kaskazini – magharibi mwa Pakistan. Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana kujeruhiwa japo idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka zaidi. Maafisa mjini Peshawar wanasema kuwa wanaume watano ama sita waliokuwa na silaha waliingia shuleni hapo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi . Wanafunzi mia tano na waalimu walikuwa katika shule hiyo ya umma ya kijeshi...

Like
256
0
Tuesday, 16 December 2014
NHIF YANYAKUWA TUZO 3 ZA UBUNIFU BARANI AFRIKA
Global News

SHIRIKISHO la Kimataifa la Taasisi za hifadhi ya jamii-ISSA,l imekuwa na utaratibu wa kushindanisha mifuko ya hifadhi ya jamii duniani kwenye masuala ya ubunifu katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji yakiwemo uboreshaji wa huduma, uwekezaji, uhamasishaji wa afya sambamba na uepushaji wa hatari makazini. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano uliowashirikisha waandishi hao kuhusu tuzo za ubunifu barani Afrika zilizotolewa na shirikisho hilo kwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa...

Like
266
0
Tuesday, 16 December 2014
MBABAZI AFIKIRIWA KUWANIA URAIS UGANDA
Global News

WAJUMBE wa chama tawala cha National Resistance Movement nchini Uganda wamepitisha mapendekezo ya kubadili katiba yao na hivyo kumfanya katibu mkuu Amama Mbabazi kuwa hana kazi. Mbabazi anafikiriwa kuwa ana nia ya kuwania Urais mwaka wa 2016 nchini Uganda dhidi ya rais wa sasa Yoweri Museveni. Moja wa wajumbe walioshiriki ni mbunge wa Soroti mjini Mashariki mwa Uganda na pia Makamu Mwenyekiti wa wa NRM kanda ya mashariki Mike Mukula ambaye anasema katika marekebisho ya katiba ya chama hicho, sasa...

Like
231
0
Tuesday, 16 December 2014
129 WAFARIKI DUNIA BAADA YA KIVUKO KUZAMA CONGO
Global News

MIILI ya watu wapatao 129 imepatikana kutoka Ziwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya feri kupinduka na kuzama mapema siku ya Ijumaa. Waziri wa Uchukuzi nchini humo Laurent Sumba Kahozi amesema bado zoezi la kuwatafuta watu waliopotea katika ajali hiyo linaendelea. Maafisa katika jimbo la Katanga wamesema upepo mkali na kujaza abiria na mizigo kupita kiasi kumesababisha boti ya MV Mutambala, kupinduka.Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu waliokumbwa na ajali hiyo ambayo ilitokea mapema Ijumaa asubuhi....

Like
259
0
Monday, 15 December 2014
WANAHARAKATI KUHOFIA SHERIA ZA USALAMA KENYA
Global News

MAKUNDI YA KUTETEA Haki za Binaadamu yamesema kuwa Mapendekezo ya Serikali ya Kenya, kuimarisha Sheria za Usalama yanahatarisha nchi hiyo kuwa Dola inayotawaliwa na polisi. Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya mashirika ya kutetea haki za binaadamu ya Kimataifa, HUMAN RIGHTS WATCH na AMNESTY International, iwapo marekebisho ya sheria za usalama yanayopendekezwa yatapitishwa, yatazibana haki za watu waliokamatwa na watuhumiwa na kudhibiti Uhuru wa kujieleza na kukusanyika. Mapendekezo hayo ambayo huenda yakapitishwa na wabunge wa Kenya kabla ya...

Like
213
0
Monday, 15 December 2014
ISRAEL YAGOMA KUTOKA JERUSALEM
Global News

WAZIRI MKUU wa Israel BENJAMIN NETANYAHU amekataa kuwa na mazungumzo juu ya kujiondoa kwa Israel mjini Jerusalem na katika Ukingo wa Magharibi kwa kipindi kisichozidi miaka miwili. Bwana NETANYAHU ametoa kauli hiyo kabla ya kukutana na Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani JOHN KERRY hii leo. Israel imeteka maeneo ya Jerusalem, Gaza na Ukingo wa Magharibi wakati wa Vita vya Siku Sita mwaka wa 1967 na kujiondoa mjini Gaza mwaka wa 2005. Bwana NETANYAHU amebainisha kuwa kujiondoa katika maneno hayo kwa sasa...

Like
247
0
Monday, 15 December 2014
MATAIFA TAJIRI NA MASKINI YABISHANA JUU YA NJIA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
Global News

MAZUNGUMZO ya Umoja wa Mataifa kuhusu ongezeko la joto duniani yanakamilika leo mjini Lima, Peru, huku mataifa tajiri na maskini ulimwenguni yakibishana kuhusu aina ya hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi wanazostahili kuwasilisha katika mkutano wa kilele utakaoandaliwa mjini Paris Ufaransa, mwaka ujao. Katika ziara fupi aliyofanya kwenye mazungumzo hayo yanayoendelea kwa mjini Lima, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry amezitaka serikali kumaliza kulumbana kuhusu ni nani anayestahili kufanya nini katika juhudi za...

Like
297
0
Friday, 12 December 2014