Global News

SHERIA MPYA YA USALAMA YASITISHWA KWA MUDA KENYA
Global News

Mahakama Kuu nchini Kenya imesimamisha kwa muda matumizi ya baadhi ya vipengee vya Sheria ya usalama yenye utata iliopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Rais UHURU KENYATTA. Wanasiasa wa upinzani wamewasilisha kesi Mahakamani kupinga uhalali wa Sheria hiyo Kikatiba, huku wakisema inahujumu haki ya raia wa...

Like
217
0
Friday, 02 January 2015
MELI YENYE WAHAMIAJI HARAMU WAPATAO 400 YANASWA ITALI
Global News

Askari wanaolinda Pwani ya Italia wamejaribu kuwasaidia watu waliokwama ndani ya Meli ya Kibiashara, iliyotelekezwa katika Pwani ya Kusini Mashariki mwa nchi hiyo. Meli hiyo ina zaidi ya wahamiaji haramu wapatao mia nne. Taarifa zinasema hakuna mhudumu wala nahodha kwenye meli hiyo.  ...

Like
204
0
Friday, 02 January 2015
UTAFITI UNAONYESHA KUWA UGONJWA WA SARATANI NI MATOKEO YA BAHATI MBAYA
Global News

Utafiti mpya umeeleza kuwa aina nyingi za Ugonjwa wa Saratani ni matokeo ya bahati mbaya, kuliko malezo ya Vinasaba, Mazingira na Mtindo wa maisha. Watafiti nchini Marekani wamechunguza aina 31 za Saratani na kugundua kwamba Theluthi Mbili zimesababishwa na mgawanyiko holela wa Seli. Taarifa zaidi zimefafanua kuwa kwa mgawanyiko wa kila seli kuna hatari ya mabadiliko yanayoweza kusababisha...

Like
295
0
Friday, 02 January 2015
2015 YAPOKELEWA KWA KISHINDO
Global News

MWAKA MPYA wa 2015 umepokewa kwa kishindo katika maeneo mbali mbali duniani na barani Afrika. Nchini Nigeria kumekuwa shamra shamra ambapo kwa mara ya kwanza mafataki yalirushwa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lenye waislamu wengi. Shamra shamra hizo zimefanyika katika kituo cha michezo katika mji wa Kano ambapo waliohudhuria ni wale waliopata mwaliko pekee....

Like
227
0
Thursday, 01 January 2015
WAKZI WA SHANGHAI WAUPOKEA MWAKA MPYA KWA MAJONZI
Global News

SHEREHE ZA KUUPOKEA mwaka mpya 2015 zimegeuka kuwa majonzi baada ya watu35 kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye msongamano wakati wakiiupokea mwaka mpya. Maafa hayo yametokea katika mji Shanghai ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika ili kuupokea mwaka mpya. Chanzo cha taharuki hiyo bado haijafamika lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimenukuliwa vikisema imetokana na maelfu ya watu kuzuiwa kugombea fedha bandia zilizotupwa eneo hilo kutoka katika jengo...

Like
213
0
Thursday, 01 January 2015
WHO: IDADI YA VIFO VILIVYOTOKANA NA MARADHI YA EBOLA YAFIKIA 7842
Global News

SHIRIKA LA AFYA Duniani -WHO limesema idadi ya vifo vilivyotokana na mripuko wa ugonjwa wa maradhi ya Ebola Afrika magharibi imeongezeka na kufikia 7,842 kati ya kesi 20,081 zilizorekodiwa. Idadi ya mwisho ya vifo ilikuwa ni 7,693 na kesi 19,695 taarifa za Ebola zilizotolewa Desember mwaka huu. Takriban vifo na kesi zote za ugonjwa wa wa maradhi ya Ebola zimerekodiwa katika nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zimeathiriwa zaidi na mripuko huo yaani Sierra Leone, Liberia na Guinea....

Like
302
0
Wednesday, 31 December 2014
BOKO HARAM WAVAMIA KIJIJI NA KUUA 15
Global News

 WAPIGANAJI wanaodhaniwa kuwa ni Boko Haram wamevamia kijiji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuua watu takriban 15. Shambulizi hilo limetokea kijiji cha Kautikari katika jimbo la Borno, pale washukiwa wa Boko Haram walipowasili kijijini humo kwa magari yenye silaha, wakilenga Askari wa Ulinzi wa Jadi wa mji huo. Kijiji hicho kipo karibu na Chibok mahali ambapo kundi la Boko Haram, limewatekanyara Wasichana wa shule zaidi ya 200 mwezi Aprili mwaka...

Like
292
0
Wednesday, 31 December 2014
NDEGE YA KIVITA YA MAREKANI YAKIHUJUMU KITUO CHA AL SHABAB
Global News

Ndege ya Kivita ya Marekani imekihujumu kituo cha Wanamgambo wa Itikadi kali wa Al Shabab nchini Somalia. Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani mjini Washington, hujuma hizo zimelengwa dhidi ya kiongozi mmoja wa vuguvugu hilo la itikadi kali kusini mwa...

Like
299
0
Tuesday, 30 December 2014
PALESTINA: WAJUMBE KUTOKA NCHI ZA KIARABU WAMEUNGA MKONO NA KUHIMIZA MAKUBALIANO YA AMANI
Global News

WAJUMBE kutoka nchini za za Kiarabu katika Umoja wa Mataifa wameunga mkono pendekezo la Palastina kuhimiza makubaliano ya Amani pamoja na Israel mnamo muda wa mwaka mmoja unaokuja na kumaliza kukaliwa ardhi za Wapalastina na Israel hadi ifikapo mwaka 2017, licha ya upinzani wa Israel na Marekani. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa bado haijafahamika ni lini haswa mswaada wa azimio hilo utapigiwa kura katika Baraza la...

Like
229
0
Tuesday, 30 December 2014
UOKOAJI WA WATU KWENYE FERI ILIYOWAKA MOTO BADO UNAENDELEA
Global News

OPERESHENI ya kuwaokoa watu waliopo ndani ya Feri iliyowaka moto kwenye Bahari ya Adriatiki zinaendelea. Watu 10 wamekufa katika ajali hiyo na wengine kadhaa wanahofiwa kupotea. Feri hiyo ilikuwa na abiria 478 pamoja na wafanyakazi huku Watu 41 hawajulikani walipo na maafisa wa Italia na Ugiriki wanajaribu kuthibitisha jumla ya watu waliokuwemo...

Like
237
0
Tuesday, 30 December 2014
MAREKANI NA ISRAEL ZAPINGA AZIMIO LA PALESTINA KUTOTAWALIWA KIMABAVU
Global News

MABALOZI wa Mataifa ya Kiarabu wameidhinisha pendekezo la Palestina kuhusu marekebisho ya azimio la Umoja wa Mataifa la kutaka Israel kuacha kuikalia kwa mabavu Palestina katika kipindi cha miaka mitatu. Pendekezo hilo limepingwa na Israel pamoja na Marekani. Marekani imesisitiza kwamba lazima pawe na suluhisho la mazungumzo katika mzozo wa Israel na...

Like
233
0
Tuesday, 30 December 2014