Global News

BARAZA LA SENETI LAPIGA KURA YA MAREKEBISHO YA MSWADA WA SHERIA YA UCHAGUZI DRC
Global News

BARAZA la Seneti nchini DRC limepiga kura kufanyia marekebisho mswada uliopendekeza sheria za uchaguzi kufanyiwa mabadiliko. Mswada huo ndio uliozua vurugu na ghasia katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo kwa wiki moja. Mabadiliko hayo sasa yanafuta kipengee ambacho kingechelewesha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.  ...

Like
223
0
Friday, 23 January 2015
CHANJO YA MAJARIBIO YA EBOLA IPO NJIANI KUINGIZWA LIBERIA
Global News

CHANJO ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola iko njiani kuelekea nchini Liberia. Hii ni mara ya kwanza kwa chanjo hii kupelekwa kwenye nchi iliyoathiriwa zaidi na Ebola. Lakini Wataalamu wanasema, wakati huu maambukizi ya Ebola yakiwa yanapungua, itakuwa vigumu kubaini kama chanjo hii inatoa kinga dhidi ya Virusi vya ugonjwa huo. Chanjo hiyo ilitengenezwa na Kampuni moja ya Uingereza, na Taasisi ya kitaifa ya afya nchini Marekani GSK imesema ndege iliyo iliyobeba dozi za awali takriban 300 za chanjo...

Like
221
0
Friday, 23 January 2015
MGOMBEA WA CHAMA TAWALA AONGOZA KWENYE MATOKEO YA AWAZI ZAMBIA
Global News

MATOKEO ya kura za urais nchini Zambia sasa yameanza kukamilika katika ukumbi wa kimataifa wa Mulungushi makao makuu ya kuhesabia kura . Matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi ya Zambia Usiku wa kuamkia leo yanaonyesha kuwa Edgar Lungu mgombea wa chama tawala cha Patriotic Front mpaka sasa bado anaongoza akiwa na kura laki 670 elfu 397 huku mpinzani wake Hakainde Hachilema wa chama cha United Party for National Development akiwa karibu kwa kura laki 641 efu 343. Hivo Edgar Lungu...

Like
226
0
Friday, 23 January 2015
MFALME ABDULLAH WA SAUDIA AFARIKI DUNIA
Global News

KUNA TAARIFA kuwa mfalme wa Saudia Abdullah bin Abdulaziz amefariki dunia akiwa hospitalini . Tamko la kifo cha mfalme huyo zimetolewa na kaka wa mfalme huyo aitwaye , Salman,ambaye naye aliwahi kuwa mfalme. Kabla ya tamko hilo television ya taifa la Saudia ilikatiza matangazo yake na kuweka nyimbo za quraan ,kama ishara ya kifo cha kiongozi wa juu wa ufalme. Mfalme Abdullah, amefariki dunia akiwa na miaka 90, alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa tangu December mwaka wa jana kutokana na...

Like
252
0
Friday, 23 January 2015
MAREKANI NA CUBA ZIMEANZA MAZUNGUMZO YA KUREJESHA MAHUSIANO YAO
Global News

MAREKANI na Cuba zimeanza mazungumzo ya kihistoria leo kuhusu kurejesha mahusiano ya kidiplomasia baada ya kikao kilichojadili masuala ya uhamiaji kudhihirisha changamoto zilizopo katika kuondokana na uhasama wa nusu karne kati ya nchi hizo. Ujumbe wa ngazi ya juu wa Marekani kuwahi kwenda Cuba katika kipindi cha miaka 35 utakamilisha mazungumzo ya siku mbili leo mjini Havana, huku pande zote mbili zikionya hakuna uwezekano wa kufikia makubaliano ya haraka. Maafisa wa Marekani wanasema wana matumaini Cuba itakubali kuzifungua balozi zake...

Like
233
0
Thursday, 22 January 2015
BOMU LA KUTEGWA LAUA WATU KADHAA SYRIA
Global News

WATU wasiopungua sita wameuawa katika mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika mji wa Homs katikati mwa Syria. Gari hiyo ililipuka katika eneo lenye makazi ya watu na maduka katika kitongoji cha Akrama, ambacho kimekuwa kikishambuliwa mara kwa mara kwa sababu kinaonekana kuwa nyumbani kwa watu wa jamii ya Alawi ambao ni wafuasi wa rais wa Syria Bashar al Assad. Gavana wa mji wa Homs Talal Barrazi amethibitisha idadi ya vifo vilivyotokea akisema wengi walikuwa wanawake na watoto. Watu...

Like
204
0
Thursday, 22 January 2015
ICC YATAKA  JOSEPH KONY AKAMATWE NA KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA HIYO
Global News

MWENDESHA  Mkuu wa mashitaka katika mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu ICC Fatou Bensouda ametaka kuwepo kwa juhudi mpya za kumkamata kiongozi wa kundi la waasi la Uganda la Lord’s Resistance Army LRA Joseph Kony baada ya kamanda wa ngazi ya juu wa kundi hilo Dominic Ongwen kufikishwa katika mahakama hiyo jana  kujibu mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu. Bensouda amesema waathiriwa wa madhila yaliyofanywa na kundi la LRA linaloongozwa na Kony wamesubiri kwa muda mrefu kwa haki kutendeka....

Like
216
0
Thursday, 22 January 2015
MAKUNDI YANAYOPIGANA SUDAN KUSINI YAKUTANA TANZANIA
Global News

MAKUNDI yanayopingana nchini Sudan Kusini yamekusanyika nchini Tanzania kusaka jitihada mpya za kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja na kusababisha maelfu ya watu kuuawa. Serikali ya Tanzania ambayo inasimamia mazungumzo ya Arusha kupitia chama tawala cha CCM nchini, imesema Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na aliyekuwa naibu wake na sasa kuwa kiongozi wa waasi nchini humo Riek Machar walikutana Jumatano na kutiliana saini mkataba mpya wa amani. Pande mbili hizo zilitiliana saini mkataba...

Like
240
0
Thursday, 22 January 2015
VIONGOZI WA KANISA LA BAPTIST WAPIGWA NA KUTEKWA NYARA GUINEA
Global News

VIONGOZI watatu wa kanisa la Baptist nchini Guinea wamepigwa na kisha kutekwa nyara baada ya wenyeji kudhani kwamba  walikuwa  maafisa wanaohamasisha jamii dhidi ya ugonjwa wa Ebola . Viongozi hao walikuwa wametembelea kijiji cha kabac eneo la forecariah wakilenga kufukiza dawa ya wadudu kwenye kuta za vyoo vya umma  ikiwa ni sehemu pia ya kujipatia  huduma ya maji . Taarifa zimesema kuwa wanakijiji hao walipowaona waliwashuku kuwa wanataka kueneza ugonjwa wa ebola  katika eneo hilo ....

Like
173
0
Wednesday, 21 January 2015
11 WAUAWA DRC KUFUATIA MSWADA TATANISHI WA UCHAGUZI
Global News

SERIKALI ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC ,imesema  kwamba takriban watu 11 wakiwemo raia wameuawa mjini Kinshasa tangu vurugu zilizosababishwa na mswada tatanishi wa uchaguzi kuanza Jumatatu. Msemaji wa Serikali, Bwna Lambert Mende amesema Mswada huo umetajwa na wanasiasa wa upinzani kama mapinduzi ya kikatiba wakisema utamfanya Kabila kujiongeza muda madarakani kwa miaka mingine mitatu. Mswada huo unajadiliwa na baraza la seneti huku viongozi wa upinzani wakiitisha maandamano mengine hii leo kuupinga mswada huo.    ...

Like
281
0
Wednesday, 21 January 2015
KAMANDA WA KUNDI LA LRA KUFIKISHWA ICC
Global News

KIONGOZI wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Uganda, Lord’s Resistance  Army, LRA amekabidhiwa kwa wawakilishi wa Mahakama  ya Kimataifa ya ICC, na sasa ameshawasili mjini The Hague ambako atafunguliwa kesi. Kiongozi huyo Dominic Ongwen atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu  wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Kundi la kigaidi la LRA kwa muda mrefu limekuwa linafanya vitendo vya kinyama katika nchi za  Afrika mashariki na kati. Ongwen alijisalimisha mwenyewe kwa majeshi ya Marekani katika  Jamhuri ya Afrika...

Like
201
0
Wednesday, 21 January 2015