Global News

UBELGIJI YAFANYA OPERESHENI KUSAKA MAGAIDI
Global News

  SERIKALI ya Ubelgiji imefanya operesheni kali ya ugaidi ikiwasaka watuhumiwa wanaodaiwa ni wapiganaji wa kiislamu waliorejea kutoka Syria. Watuhumiwa wawili wa ugaidi wameuawa na mmoja anashikiliwa na vyombo vya usalama katika mji wa Vere viee , baada ya Watu hao kuwashambulia polisi kwa bomu. Meya wa mji huo anasema sasa hali ni shwari na inaelezwa kuwa Polisi iliwashuku kuwa watu hao walikua na mipango ya kutekeleza shambulio la kigaidi dhidi ya maafisa wa polisi na kwenye vituo vya Polisi....

Like
226
0
Friday, 16 January 2015
PAPA FRANCIS AWASILI UFILIPINO
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa FRANCIS, amewasili nchini Ufilipino kwa ziara ya siku tano katika taifa la tatu kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waumini wa Kikatoliki duniani. Maelfu ya Wafilipino wamemiminika barabarani katika mji mkuu Manila kumlaki Papa FRANCIS huku ulinzi ukiwa...

Like
375
0
Thursday, 15 January 2015
SENEGAL YAPIGA MARUFUKU USAMBAZAJI WA GAZETI LA CHARLIE HEBDO
Global News

GAZETI MOJA nchini Kenya, la The Star limeomba radhi kwa kuchapisha ukurasa wa kwanza wa jarida la Charlie Hebdo uliokuwa na kibonzo kinachomkejeli Mtume MUHAMMAD S.A W. Wahariri wa gazeti hilo wamesema kuwa wanaomba radhi ikiwa wamekera mtu yoyote kwa kuchapisha ukurasa huo. Taarifa zaidi zimebainisha kuwa Malalamiko kutoka kwa viongozi wa Kiisilamu yamepelekea Wahariri wa gazeti hilo kuomba radhi, pia nchini Senegal imepiga marufuku usambazaji wa jarida hilo nchini...

Like
219
0
Thursday, 15 January 2015
MAGAIDI KUCHUKULIWA HATUA UFARANSA
Global News

SERIKALI ya Ufaransa imewataka waendesha mashtaka kuchukua hatua thabiti dhidi ya Watu waliotekeleza vitendo vya kigaidi.Waziri wa Sheria nchini humo,Christiane Taubira amesema maneno au vitendo vya chuki dhidi ya mwingine vinavyotolewa kwa sababu ya imani ya dini vikomeshwe. Zaidi ya Kesi 50 zimefunguliwa dhidi ya Watu wanaotuhumiwa kuhusika na shambulio la kigaidi wiki iliyopita na kusababisha watu 17 kupoteza maisha. Wakati hayo yakijiri,kumekuwa na mapokeo hasi kwa Waumini wa kiislamu baada ya kuchapishwa kwa Jarida lenye kibonzo...

Like
213
0
Thursday, 15 January 2015
KAMANDA MKUU WA LRA ALIEJISALIMISHA AKABIDHIWA KWA WANAJESHI WA UGANDA
Global News

 KAMANDA MKUU wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda, aliyejisalimisha wiki jana, Dominic Ongwen , amekabidhiwa kwa wanajeshi wa Uganda walio katika Jamuhuri ya Afrika ya kati. Muasi huyo, Dominic Ongwen, anasemekana kuwa Naibu kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony na alikamatwa na wanajeshi wa Marekani wiki jana ingawa waasi wa Seleka wanasema wao ndio waliomkamata. Waasi hao wanasema kwamba walimkatama Ongwen baada ya makabiliano ya muda ingawa jeshi la Marekani lilisitiza kuwa alijisalimisha na tangu hao wamekuwa...

Like
211
0
Wednesday, 14 January 2015
KANSELA ANGELA MERKEL AMESEMA SERIKALI YAKE ITATUMIA NJIA ZOTE KUPAMBANA NA UBAGUZI
Global News

SIKU  baada ya kuuita Uislamu kuwa ni sehemu ya Ujerumani, Kansela ANGELA MERKEL amesema serikali yake itatumia njia zote ilizonazo kupambana na ukosefu wa uvumilivu na ubaguzi, akitaja kutoshirikishwa kwa baadhi ya makundi ya kijamii kuwa ni jambo la kulaumiwa. Matamshi yake yamekuja siku moja baada ya waandamanaji 25,000 wanaoupinga Uisilamu kuandamana katika mji wa Mashariki wa Dresden kutaka sheria kali zaidi za uhamiaji na kukomesha sera ya kukubali utamaduni...

Like
214
0
Wednesday, 14 January 2015
GAZETI LA VIBONZO LACHAPISHA KIBONZO CHA MTUME MUHAMMAD
Global News

GAZETI la Charlie Hebdo leo limeanza kusambaza toleo la gazeti lake ambalo limechapisha kibonzo cha Mtume MOHAMMAD kwenye ukurasa wake wa mbele. Imeelezwa kuwa zaidi ya Nakala Milioni za gazeti hilo zimeanza kusambazwa na nyingine zitafuata iwapo wanunuzi wataongezeka....

Like
427
0
Wednesday, 14 January 2015
KANSELA ANGELA MERKEL AJIANDAA KUJIUNGA NA JAMII YA WAISLAMU
Global News

KANSELA wa Ujerumani ANGELA MERKEL anajiandaa kujiunga na Jamii ya Waislamu katika maandamano ya Maridhiano na Kuvumiliana nchini Ujerumani na kulaani mashambulio yaliyofanywa na vijana wenye itikadi kali mjini Paris nchini Ufaransa wiki iliyopita. Maandamano hayo pia yamelenga kutuma ujumbe wa kupinga vuguvugu lililooongezeka nchini Ujerumani dhidi ya Waislamu....

Like
185
0
Tuesday, 13 January 2015
KAMANDA WA WA LRA AJISALIMISHA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI
Global News

SERIKALI ya Uganda imeeleza kuwa  Kamanda wa Kundi la Waasi la Lord Resistance Army-LRA DOMINI ONGWEN amejisalimisha Jamuhuri ya Afrika ya Kati, hivyo atakabidhiwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya ICC. Kamanda huyo ni miongoni mwa watu wa kundi la LRA wanaosakwa na viongozi wa Mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC kwa kutenda uhalifu dhidi ya...

Like
246
0
Tuesday, 13 January 2015
WABUNGE WARUMBANA DRC
Global News

mvutano umetokea katika Bunge la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya wabunge wa upinzani kupinga sheria mpya ambayo ina kipengele kinachotaka uchaguzi wa Rais na wabunge ufanyike baada ya sensa kufanyika. Wapinzani wamesema hatua hiyo haikubaliki kwani hatua hiyo itamfanya Rais wa nchi hiya JOSEPH KABILA kubakia Madarakani hadi mwaka 2016 ambao ni mwaka wa...

Like
211
0
Tuesday, 13 January 2015
GAZETI LA VIBONZO LINATARAJIWA KUCHAPISHA KIBONZO KESHO
Global News

GAZETI la kila Wiki la Vibonzo la CHARLIE HEBDO la Ufaransa toleo la January 14 linatarajiwa kuchapisha Kibonzo cha MTUME MOHAMED S.A.W katika ukurasa wake wa mbele chenye kichwa cha habari kisemacho“YOTE YAMESHASAMEHEWA” Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Walioona kibonzo hicho wamesema MTUME MOHAMMAD S.A.W ataonekana ameshikilia bango lililoandikwa “JE SUIS CHARLIE” maneno yenye tafsiri “mimi ni Charlie, yaliyotumika kuonyesha mshikamano, baada ya shambulizi katika ofisi za gazeti hilo Jumatano wiki iliyopita ambapo...

Like
234
0
Tuesday, 13 January 2015