Global News

265 WAOKOLEWA KATIKA FERI ILIYOWAKA MOTO HUKU WENGINE 200 WAKISALIA
Global News

Wafanyakazi wa shughuli za uokozi wamefanikiwa kuwaokoa watu 265 kutoka ndani ya feri inayowaka moto ikiwa kwenye bahari kati ya Italia na Ugiriki na bado watu wengine 200 wamebaki ndani ya feri hiyo iitwayo Norman Atlantic. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Helikopta zimekuwa zikiwavuta watu kutoka feri hiyo iliyoshika moto Desember 28 mwaka huu...

Like
297
0
Monday, 29 December 2014
NDEGE ILIYOPOTEA YAENDELEA KUTAFUTWA
Global News

Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo imepotea Desember 28 imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda. Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia....

Like
233
0
Monday, 29 December 2014
UPEPO MKALI NA MAWIMBI VYAKWAMISHA JUHUDI ZA UOKOAJI MELI ILIYOZAMA
Global News

IMEELEZWA KUWA Waokoaji wameendelea kupambana na upepo mkali pamoja na mawimbi ya bahari gizani kuwakoa abiria 300 ambao wamekwama ndani ya Ferry ya Italia iliyokuwa imeshika moto kwenye Bahari ya Adriatic. Maofisa nchini Italia  meeleza kuwa oparesheni ya uokoaji itandelea ambapo mpaka sasa watu 190 wamekolewa kutoka kwenye Ferry...

Like
250
0
Monday, 29 December 2014
INDONESIA YAFANYA KUMBUKUMBU YA MIAKA KUMI TANGU KUTOKEA KWA TSUNAMI
Global News

Wananchi wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa Kumi tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha Mawimbi makubwa katika bahari ya Hindi, Tsunami na kusababisha Vifo vya watu zaidi ya laki mbili. Umati wa watu umekusanyika karibu na jengo la makumbusho la Tsunami katika eneo la Banda Aceh katika kisiwa cha...

Like
272
0
Friday, 26 December 2014
MWANAFUNZI ATIWA MBARONI KWA KUMTUKANA RAIS
Global News

Polisi nchini Uturuki wamemkamata Mwanafunzi wa Sekondari mwenye umri wa 16 kwa tuhuma za kumtukana Rais RECEP TAYYIP ERDOGAN. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, kijana huyo amepelekwa mahabusu baada ya kumtuhumu Bwana ERDOGAN na chama chake tawala cha AK kwa vitendo vya rushwa wakati wa Mkutano wa hadhara katikati ya mji wa...

Like
263
0
Friday, 26 December 2014
EBOLA: SIERRA LEONE YAPIGA MARUFUKU MIKUSANYIKO
Global News

SERIKALI YA SIERRA LEONE imetangaza siku tatu za marufuku Kaskazini mwa taifa hilo, ili kuruhusu jitihada za kukabiliana na kuenea zaidi kwa ugonjwa hatari wa Ebola. Msemaji wa Serikali amesema kuwa maduka na masoko yatafungwa na hakuna magari ya abiria au pikipiki zitakazokubaliwa kupita kwenye barabara za eneo hilo. Sherehe Makanisa kuadhimisha sherehe za siku ya Krismasi pia zimepigwa...

Like
212
0
Thursday, 25 December 2014
PAPA FRANCIS AWATAKA WAKRISTU DUNIANI KUMRUHUSU MUNGU KUINGIA KATIKA MAISHA YAO
Global News

KIONGOZI WA KANISA Katoliki Duniani Papa FRANCIS, amewataka Wakristu duniani kumruhusu Mungu kuingia katika maisha yao kusaidia kupambana na giza na rushwa. Papa FRANCIS ametoa wito huo wakati akiongoza Ibada ya Mkesha wa Krismas, iliohudhuriwa na Maelfu ya Waumini katika kanisa la mtakatifu Petero mjini Rome. Hiyo ni Krismas ya pili kwa Papa FRANCIS , aliechaguliwa mwaka uliyopita na raia wa kwanza asiyetoka Bara la Ulaya katika kipindi cha Miaka 1,300...

Like
182
0
Thursday, 25 December 2014
DRC: WATU KADHAA WANAHOFIWA KUFA BAADA YA BOTI KUZAMA
Global News

Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya boti kuzama kwenye Mto Kongo. HUBERT MOLISO waziri katika Mkoa wa Kaskazini wa Orientale, amesema kuwa abiria walikuwa wamelala wakati ajali hiyo imetokea karibu na mji wa Lombolombo. Watu wasiopungua 100 wamenusurika kifo huku watu Wanne wamefariki...

Like
237
0
Wednesday, 24 December 2014
IS YAANGUSHA NDEGE YA KIJESHI SYRIA
Global News

Kundi linalojiita Dola la Kiislamu Islamic State-IS, limeiangusha ndege ya kivita katika anga ya Syria ambayo, kwa mujibu wa shirika la kuchunguza Haki za Binadamu nchini humo, ni ya Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani. Shirika hilo lenye makao nchini Uingereza limesema IS imeidungua ndege hiyo karibu na mji wa Raqqa ulipo Kaskazini Mashariki mwa Syria, kwa kutumia kombora la kudungulia ndege. Taarifa zaidi kutoka shirika hilo zimeeleza kuwa rubani wa ndege hiyo amekamatwa.  ...

Like
389
0
Wednesday, 24 December 2014
TAKRIBANI WANAHABARI 60 DUNIANI WAMEUAWA MWAKA 2014
Global News

IMEELEZWA kuwa takribani waandishi wa habari 60 kote ulimwenguni waliuawa katika mwaka wa 2014 wakiwa kazini au kwa sababu ya kazi zao, na asilimia 44 ya wanahabari waliuawa kwa makusudio. Ripoti mpya ya Kamati ya Kuwalinda Waandishi wa Habari yenye makao yake mjini New York, Marekani, imesema idadi kubwa ya wale waliouawa ni waandishi wa habari wa kimataifa, japo kuwa idadi kubwa zaidi ya wanahabari wanaotishiwa inaendelea kuripotiwa katika nchi mbalimbali. Karibu wanahabari 17 wameuawa nchini Syria ambako mgogoro wa...

Like
253
0
Tuesday, 23 December 2014
WAZIRI MKUU WA UFARANSA ATOA TAHADHALI DHIDI YA MASHAMBULIO
Global News

  WAZIRI MKUU wa Ufaransa Manuel Valls ametoa wito wa kuwepo uangalifu baada ya nchi hiyo kukumbwa na mashambulizi matatu ya ajabu mfululizo, na kuzusha hofu ya kutokea mashambulizi mengine kama hayo. Katika tukio la hivi karibuni lililotokea katika mji wa magharibi wa Nantes, dereva aliliendesha gari lake na kuwagonga watu waliokuwa katika soko la Krismasi jana jioni, na kuwajeruhi kumi kabla ya kujichoma kisu mara kadhaa kabla ya kukamatwa. Tukio hilo lilikuja siku moja baada ya shambulizi jingine sawa...

Like
236
0
Tuesday, 23 December 2014