Global News

SIERRA LEONE KULIPA FIDIA KWA WAHANGA WA EBOLA
Global News

SERIKALI ya Sierra Leone imesema italipa dola elfu tano za kimarekani kama fidia kwa familia ya kila mfanyakazi wa afya ambaye amefariki baada ya kuambukizwa Ebola wakati akihudumia wagonjwa wa Ebola. Kituo cha taifa cha kupambana na Ebola nchini humo kimesema fidia hiyo ya mara moja pia itatolewa kwa ndugu wa wafanyakazi wa afya zaidi mia moja ambao wamekufa kwa ugonjwa huo hapo awali. Virusi vya ugonjwa huo vimekuwa vikisambaa kwa kasi nchini Sierra Leone ambapo katika muda wa siku...

Like
275
0
Wednesday, 12 November 2014
WANAHARAKATI WACHINJWA DERNA
Global News

WANAHARAKATI watatu wa kisiasa nchini Libya wameuawa kwa kuchinjwa baada ya kuandika katika mitandao ya kijamii juu ya maisha chini ya utawala wa dola ya kiislam. Miili yao ilipatikana mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna karibu na Benghazi. Tukio hilo lilianzia kwa wanaharakati hao kutekwa mapema mwezi huu. Mji huo wa Derna uko chini ya mamlaka ya kikundi cha dola ya kiislam tangu mwaka 2012 ambacho kimekiri kuwa sehemu ya kundi la IS. Mnamo mwezi August mwaka huu...

Like
280
0
Wednesday, 12 November 2014
SYRIA YATAFAKARI KUSITISHA MAPIGANO ALEPPO
Global News

RAIS wa  Syria Bashar al-Assad  amesema anatafakari  mpango  wa Umoja  wa  Mataifa kusitisha  mapigano  katika  mji  wa  kaskazini wa  Aleppo. Mjumbe  wa  Umoja  wa  Mataifa  nchini  Syria  Staffan de Mistura , amependekeza  wazo  hilo mwezi  wa  Oktoba  wakati  wa  ziara yake  katika  eneo  la  vita. de Mistura  ameshauri kufanya  majadiliano na  kupata usitishaji  wa mapigano ndani ya eneo hilo ili kuruhusu upelekaji wa misaada na kuweka mpango kwa ajili  ya  mazungumzo  ya  amani....

Like
227
0
Tuesday, 11 November 2014
SATA AWEKWA KWENYE MAKAZI YA MILELE
Global News

RAIS wa Zambia MICHAEL SATA amezikwa leo mjini Lusaka baada ya mwili wake kuwekwa kwa muda wa Wiki Moja na wananchi kutoa heshima zao za mwisho. Viongozi wa Kidini kutoka Makundi mbalimbali ya Waumini wamefanya Sala katika jengo la Bunge, katika tukio lililohudhuriwa na Wanadiplomasia, Wanasiasa , ikiwa ni pamoja na Rais wa kwanza wa nchi hiyo KENNETH KAUNDA na mtangulizi wa SATA RUPIAH BANDA. Wananchi wametoa heshima zao za mwisho hadi siku ya Jumapili kwa kupita mbele ya Jeneza...

Like
477
0
Tuesday, 11 November 2014
MKUTANO WA APEC KILELE CHAKE LEO
Global News

VIONGOZI wa nchi za Asia na Pacific wanaendelea na Mkutano wao leo kwa siku ya pili ya mkutano wa kilele wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pacific APEC ambao unafikia kilele chake leo. Viongozi hao wanatarajiwa kuangazia suala la kutanua biashara huru miongoni mwao na kutafuta njia za makubaliano. China inazitaka nchi 21 wanachama wa jumuiya hiyo ya APEC kuidhinisha kujitolea kuunga mkono mpango wa biashara huru wa maeneo ya Asia na pacific ujulikanao FTAAP...

Like
229
0
Tuesday, 11 November 2014
IDADI YA WANAWAKE WANAOFARIKI WAKATI WA KUJIFUNGUA YAZIDI AFRIKA MAGHARIBI
Global News

IDADI ya wanawake wanaofariki wakati wa kujifungua katika nchi za magharibi mwa Afrika zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola inazidi kupanda huku mwanamke mmoja kati ya saba katika nchi hizo akiwa katika hatari ya kufa kutokana na kutopokea usaidizi wakati wa kujifungua, watu wakihofia kuambukizwa Ebola kwa kushika damu na maji maji ya miili ya wajawazito. Mashirika ya kutoa misaada 13 kutoka Uingereza yakiwemo Save the children,Action Aid na hata shirika la umoja wa Mataifa kuhusu idadi ya watu yanakisia kuwa...

Like
273
0
Tuesday, 11 November 2014
SHAMBULIO LAUA WANAFUNZI 47
Global News

IMEELEZWA kuwa, shambulizi limetokea katika shule moja ya upili wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Duru zinasema kuwa wanafunzi 47 wameuawa katika shambulizi hilo linalosemeklana kufanywa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alikuwa amevalia sare za shule. Shambulizi lilitokea wakati wanafunzi wakiwa wamekusanyika wakati wa asubuhi. Mji wa Potiskum ambapo shule hiyo ipo, umekuwa kitovu cha mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na Boko Haram.  ...

Like
252
0
Monday, 10 November 2014
CHINA NA JAPAN ZABORESHA MAHUSIANO
Global News

RAIS wa China, Xi Jinping na waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe wamefanya mazungumzo kwa mara ya kwanza tangu wote washike madaraka. Mkutano wao unaonekana kama hatua ya ufanisi ya juhudi za kutatua mgogoro uliokuwepo kati ya nchi hizo kutokana na madai ya Japan kuthibiti visiwa katika bahari ya kaskazini mwa China. Baada ya dakika thelathini za mazungumzo Bwana Abe aliondoka na kusema kuwa hiyo ndiyo hatua ya kwanza ya kuboresha mahusiano. Mkutano huo ulifanyika Beijing wakati viongozi kutoka katika...

Like
252
0
Monday, 10 November 2014
OBAMA AWASILI ZIARANI BEIJING
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amewasili mjini Beijing,China hii leo ambako yuko katika ziara itakayomfikisha katika nchi tatu za Asia na Pacifiki. Obama yuko nchini humo kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nchi za Asia na Pacifiki, APEC ambao unahudhuriwa pia na viongozi wengine wa nchi akiwemo Rais wa Urusi Vladimir Putin na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe. Rais Obama atafanya mazungumzo na rais mpya wa Indonesia Joko Widodo na waziri mkuu wa Australia...

Like
276
0
Monday, 10 November 2014
MABEDUI WAPATIWA URAIA WA KIUCHUMI COMORO
Global News

MAELFU YA WATU wasiokuwa na Uraia wanaoishi nchini Kuwait,wanatarajia kupatiwa uraia katika visiwa vya Comoro vilivyoko katika bahari ya Hindi.Taarifa hiyo imetangazwa na serikali ya Kuwait . Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Watu wasiokuwa na uraia wanaojulikana kama “MABEDUI” watapatiwa kile kinachojulikana kama “Uraia wa kiuchumi”. Naibu katibu wa Wizara ya mambo ya ndani ya Kuwait,Meja Jenerali MAZEN AL-JARRAH amesema Mpango huo unatarajiwa kuanza mara tu baada ya visiwa vya Comoro kufungua ofisi yake ya Ubalozi mjini...

Like
354
0
Monday, 10 November 2014
WANAJESHI WAZIDI KUTEKETEA AFGHANSTAN
Global News

KATIBU MKUU wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg, amesema idadi ya wanajeshi wa Afghanistan wanaokufa imeongezeka zaidi kwa sababu ya kuchukuwa kwao dhima ya juu katika vita dhidi ya wanamgambo wa Taliban. Takwimu zilizotolewa wiki hii zinaonesha kuwa hadi kufikia sasa, wanajeshi wa Kiafghani waliouawa mwaka huu pekee ni 4,634. Stoltenberg ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza nchini Afghanistan tangu achukue wadhifa huo mwanzoni mwa mwezi Oktoba, alikutana na Rais Ashraf Ghani hapo jana na leo anaelekea...

Like
249
0
Friday, 07 November 2014