Global News

MFANYAKAZI WA UN ALIEAMBUKIZWA EBOLA AFARIKI UJERUMANI
Global News

Madaktari katika hospitali ya Leipzig wamesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 56, alifariki dunia mapema Jumanne asubuhi. Mlipuko huo umeua zaidi ya watu 4,000 tangu mwezi Marchi, mwaka huu hususan katika nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria. Shirika la Afya Duniani limeuelezea ugonjwa huo kama tatizo la dharura la kiafya kuwahi kuonekana katika maisha ya sasa ya binadamu. Marekani na Uingereza ni miongoni mwa nchi zilizoanzisha utaratibu wa upimaji afya za abiria kuhusiana na ugonjwa wa Ebola...

Like
319
0
Tuesday, 14 October 2014
GERRIE NEL AMPINGA MARINGA KWENYE KESI YA PISTORIUS
Global News

Idara ya kurekebisha tabia nchini Afrika Kusini inataka Oscar Pistorius apewe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu kwa kumpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp. Bwana Joel Maringa afisa anayehusika na masuala ya urekebishaji tabia aliiambia mahakama mjini Pretoria kuwa hawamuadhibu tu Pistoruiis bali pia wanataka kumbadili kitabia akisema kuwa anaweza kutoa huduma za jamii kwa saa 16 kwa mwezi. Awali daktari wa Pistorius anayehusika na matatizo ya akili Lore Hartzenberg aliiambia mahakama kuwa mwanariadha huyo mlemavu amevunjika moyo...

Like
286
0
Monday, 13 October 2014
HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI
Global News

Uongozi wa rais Barack Obama wa Marekani umetoa wito wa kuwepo hali ya utulivu kufuatia kupatikana kwa mgonjwa wa ebola nchini kwake. Taarifa zinasema Marekani inajiandaa kupambana na mzozo wa ugonjwa wa ebola kote nchini mwake na katika eneo. Milipuko wa ugonjwa wa ebola kwa miaka 40 iliyopita ilidhibitiwa. Marekani inatuma vikosi elfu mbili nchini Liberia kusaidia kupambana na mlipuko wa ebola ambao umeuwa takriban watu elfu tatu katika bara la Afrika magharibi. Marekani pia inajaribu kuondoa hofu kuhusu kuzuka...

Like
252
0
Thursday, 09 October 2014
HATIMAE KENYATTA AIKABILI ICC LEO NA KUWEKA REKODI
Global News

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu. Yeye ni kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo. Kenyatta amefika mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya kukata kuwasilisha ushahidi muhimu. Kenyatta amekanusha madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008. Kikao cha leo kitatathmini ombi...

Like
262
0
Wednesday, 08 October 2014
PAPA APOKEA TAARIFA YA KUJIHUZURU KWA ASKOFU KUFUATIA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAPENZI
Global News

Baba Mtakatifu Francis amekubali kujiuzulu kwa Askofu Kieran Conry kutoka majimbo ya Arundel na Brighton baada ya kupokea barua ya Askofu huyo alieomba radhi mara baada ya taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari Conry, mwenye umri wa miaka 64, aliomba radhi katika barua kwa kutokuwa mwaaminifu kwa ahadi yake kama kuhani Katoliki lakini alisisitiza matendo yake yalikuwa si ​​kinyume cha sheria na hawakuwa kuhusisha watoto. Kanisa katoliki limekuwa likipata shinikizo juu ya kubadilisha tamaduni hivyo kuwaruhusu watumishi hao kuingia kwenye...

Like
674
0
Tuesday, 07 October 2014
RAIS KENYATTA NIPO RADHI KWENDA ICC
Global News

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema yuko radhi kwenda katika mahakama ya kimataifa ya ICC kwa kikao maalum kuhusu kesi inayomkabili. Akiwahutubia wabunge mjini Nairobi,aliwaambia kuwa yuko tayarti kuhudhuria kikao maalum alichotakiwa kuhudhuria mjini Hague bila wasiwasi wowote. Kenyatta alitakiwa na majaji wa mahakama hiyo kufika ICC tarehe 8 mwezi huu kufafanua madai kuwa serikali yake imekataa kushirikiana na mahakama hiyo hasa upande wa mashitaka kwa kukataa kuipatia ushahidi unaohitajika katika kesi inayomkabili. Anakabiliwa na tuhuma za...

Like
356
0
Tuesday, 07 October 2014
MGONJWA WA EBOLA ABAINIKA HISPANIA
Global News

Uchunguzi unaendelea katika hospitali ya Madrid nchini Hispania kutokana na muuguzi mmoja nchini humo kuwa mtu wa kwanza kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola anaodaiwa kuwa aliambukizwa virusi vya ugonjwa huo kutoka nchi za Afrika Magharibi. Muuguzi huyo alikuwa miongoni mwa kikosi cha madaktari waliowatibia raia wamisionari wawili waliokufa kutokana na ugonjwa huo baada ya kurejeshwa nyumbani kwao wakitokea nchi za Afrika Magharibi. Hata hivyo hospitali hapo kwa sasa kuna uangalizi mkubwa huku vifaa vya kujikinga na vifaa...

Like
298
0
Tuesday, 07 October 2014
Uchaguzi kuingia duru ya pili Brazil
Global News

Huku zaidi ya asilimia 97 ya kura zilizopigwa zikiwa zimehesabiwa kwenye uchaguzi mkuu nchini Brazil, rais Dilma Roussef ameshinda awamu ya kwanza ya kura hizo, lakini bado hajapa ushindi unaohitajika ili kuzuia kuwepo duru ya pili. Mpinzani wake wa karibu Aecio Neves amechukua nafasi ya pili. Matokeo haya hata hivyo yanamaanisha kuwa mgombea mwingine ambaye ni waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva ameondolewa kwenye kinyanganyiro hicho hata baada ya kuonekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwa rais wa Brazil....

Like
297
0
Monday, 06 October 2014
WANAFUNZI 40 MEXICO WAPOTEA
Global News

Mamia ya wanafunzi nchini Mexico katika jimbo la Guerrero wameandamana katika mji mkuu wa jimbo la Chilpancingo kulalamikia kutoweka kwa zaidi ya wanafunzi wenzao arobaini wiki iliyyopita. Wanafunzi hao wanasemekana kuwa mwisho walionekana kusombwa katika magari ya polisi kufuatia maandamano walioshiriki wakilalamikia ubaguzi katika ajira ya walimu wa maeneo ya vijijini. Polisi walifyatua rissasi kwenye basi na kwa waandamaji na kuua watu sita na wengine 17 kujeruhiwa. Maafisa ishirini na wawili wa polisi wanashikiliwa na kwa kutuhuma za...

Like
298
0
Friday, 03 October 2014
WANAFUNZI KUMSHTAKI MKE WA RAIS MUGABE
Global News

Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zimbabwe al maarufu Zinasu, umesema kwamba unawasilisha kesi mahakamani hii leo kutafuta ufafanuzi zaidi wa namna mkewe rais Grace Mugabe alivyopata shahada ya udaktari wa falsafa. Mwanafunzi mmoja mwanaharakati amesema kuwa ni muhimu kwa taifa hilo kuhifadhi hadhi yake ya elimu. Baadhi ya watu wamehoji kasi aliyosomea shahada hiyo huku wengine wakidai ni njama za kumuandaa kwa urithi wa kiti cha rais baada ya rais Mugabe. Gazeti moja linalomilikiwa na serikali , the...

Like
288
0
Wednesday, 01 October 2014
HOFU YA EBOLA YATANDA MAREKANI
Global News

Hali hiyo imekuja mara baada ya Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola kugundulika nchini Marekani, na kuthibitishwa katika mji wa Dallas, Texas. Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo. Jumatatu, maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo. Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka...

Like
246
0
Wednesday, 01 October 2014