Global News

BURKINA FASO: JESHI LAIPUUZA AU
Global News

KIONGOZI wa mpito wa Burkina Faso ametupilia mbali muda wa wiki mbili wa kukabidhi madaraka uliotolewa na Umoja wa Afrika wa kukabidhi madaraka kwa Raia. Luteni Kanali Isaac Zida amesema haogopi vikwazo , na kuwa wanajali zaidi kuhusu uimara wa nchi yao.Zida alifanya mazungumzo na upinzani na asasi za kiraia na kukubaliana kuitisha uchaguzi mwakani. Jeshi lilishika madaraka baada ya kifo cha Rais Blaise Compaore ambaye alishinikizwa kujiuzulu baada ya kutokea maandamano wiki iliyopita.  ...

Like
283
0
Friday, 07 November 2014
UTATA JUU YA KIFO CHA OSAMA BIN LADEN
Global News

UTATA  umetanda miongoni mwa wananchi nchini Marekani kutaka kujua ni askari yupi hasa aliyefyatua risasi iliyomuua Osama Bin Laden, zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, baada ya kuibuka madai mbalimbali. Askari wa zamani wa kikosi cha Seal cha wanamaji wa Marekani, Robert O’Neill, mwenye umri wa miaka 38, ameliambia gazeti la Washington Post katika mahojiano mapya kuwa ndiye alifyatua risasi iliyomuua Osama. Maelezo hayo yanapingana na yale ya Matt Bissonnette,...

Like
814
0
Friday, 07 November 2014
UHARIBIFU MSITU WA AMAZON KUIGHARIMU BRAZIL
Global News

  TAKWIMU zinaonyesha kuwa ukame umekuwa na madhara makubwa katika mji mkubwa nchini Brazil wa Sao Paulo. Dokta ANTONIO NOBRE ambaye ni Mtaalamu wa hali ya Hewa amesema vyanzo vya maji vinaweza kutoweka na kusababisha madhara kwa zaidi ya watu Milion 20 iwapo hali hiyo ya uharibifu katika msitu wa Amazon hautadhibitiwa. Baada ya kuwa ndani ya ukame kwa zaidi ya miaka nane mfululizo kina cha maji kwa sasa mjini Sao Paulo kipo katika hali ya hatari. Serikali nchini humo...

Like
602
0
Friday, 07 November 2014
EBOLA: RAIS OBAMA ALIOMBA BUNGE DOLA BILIONI 6.2 KWA AJILI YA MFUKO WA DHARURA
Global News

RAIS BARACK OBAMA wa Marekani ameliomba Bunge la nchi hiyo Dola Bilioni 6 nukta 2 kwa ajili ya Mfuko wa Dharura wa kupambana na maradhi ya Ebola katika eneo la Magharibi mwa Afrika, na kuzuia uwezekano wa Ugonjwa huo kusambaa hadi Marekani. Sehemu ya mfuko huo Dola Bilioni Mbili zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Shirika la Marekani la Msaada wa Kimataifa – USAID, huku Dola Bilioni 2 nukta 4 zikienda Idara ya Afya na Huduma za Binadamu nchini humo. Taarifa zaidi zimebainisha...

Like
209
0
Thursday, 06 November 2014
WANAFUNZI VYUO VIKUU KENYA WAAGIZWA KUTUMIA FACEBOOK NA TWITTER
Global News

WASIMAMIZI wa Vyuo Vikuu nchini Kenya wameagizwa kufungua Mitandao ya Twitter na Facebook ambayo wanafunzi watatumia kutoa malalamiko yao kwa lengo la kuzuia machafuko katika Taasisi hizo. Waziri wa Elimu nchini Kenya JACOB KAIMENYI amesema kuwa vifaa hivyo vya mawasiliano vitawasaidia wanafunzi kutoa malalamiko yao mbali na kupata majibu kutoka kwa Wasimamizi. Waziri KAIMENYI ameshtumu mbinu zinazotumiwa na Vyuo Vikuu kukandamiza upinzani mbali na kudhibiti masuala ya wanafunzi kama vile Uchaguzi wao na kuwasingizia katika masuala ya utovu wa...

Like
240
0
Thursday, 06 November 2014
BURKINA FASO KUFANYA UCHAGUZI MKUU NOVEMBER 2015
Global News

VYAMA vya siasa nchini Burkina Faso vimekubaliana kuwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba 2015 ikiwa ni harakati za kurejesha utawala wa kiraia na demokrasia.. Hata hivyo mazungumzo hayo yameisha bila kuwa na ufumbuzi kuhusiana na nani atakayekuwa kiongozi wa mpito hadi kufikia muda wa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufuatia kuangushwa kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo la Afrika Magharibi Blaise Compaore. Jeshi la nchi hiyo limekuwa likishikilia madaraka tangu aondolewe madarakani kiongozi huyo kutokana na maandamano ya...

Like
271
0
Thursday, 06 November 2014
UINGEREZA YAWATEMA WANAJESHI 300 WA LIBYA
Global News

WANAJESHI kutoka nchini Libya wamerejeshwa nchini kwao kutokana na kukosa uadilifu wakiwa mafunzoni Uingereza huku wengine wakituhumiwa kufanya vitendo vya ukatili wa kimapenzi. Wanajeshi hao waliokuwa mafunzoni nchini Uingereza, 300 kati yao wamesharejeshwa Libya kutokana na tuhuma kuhusiana na unyanyasaji wa kimapenzi. Waziri wa Ulinzi wa Libya amethibitisha kurejeshwa kwa askari hao na kuongeza kuwa wengine watarejeshwa siku chache zijazo. wanajeshi wawili wa Libya wamekiri kufanya vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanawake huko...

Like
362
0
Thursday, 06 November 2014
POLISI ISRAEL WAPAMBANA NA VIJANA WA KIPALESTINA
Global News

POLISI nchini  Israel  wamepambana  na  vijana  wa Kipalestina  waliokuwa  wakirusha  mawe ndani  ya  uwanja wa  msikiti  wa Al-Aqsa  leo  baada  ya  makundi  ya Wayahudi  wenye  msimamo  mkali  kutangaza  mipango ya  kuzuru  eneo  hilo  licha  ya  wiki  kadhaa  za  hali  ya wasi  wasi. Ziara  hiyo  iliyopangwa  na  kundi  la Wayahudi  ikiwa  ni  pamoja  na  wanasiasa  wa  siasa  za kizalendo  zaidi ilikuwa  ifanyike  wiki  moja  baada   ya jaribio  la  mauaji  dhidi ya  mmoja  kati ...

Like
239
0
Wednesday, 05 November 2014
MAREKANI: REPUBLICAN YASHIKA UDHIBITI WA BARAZA LA SENETI
Global News

MATOKEO ya  awali  ya  uchaguzi  mdogo  nchini  Marekani yanaonesha  kuwa  chama  cha  Republican  kimechukua udhibiti  wa  baraza  la  Seneti kwa  kupata  kiasi  ya  viti  51 katika  baraza  hilo  lenye  viti 100. Pia  chama  hicho kinaelekea  kupata  ushindi  wa kishindo  katika  baraza  la wawakilishi kwa  miongo  kadhaa. Warepublican wamefaidika  na  wimbi  la  kutoridhika  kwa  wapiga  kura na  kutoa  pigo  kwa  rais Barack Obama  ambalo litapunguza  uwezo  wake  wa  kupitisha  ajenda ...

Like
280
0
Wednesday, 05 November 2014
JUMUIYA YA KIMATAIFA YAONYWA KUTOLEGEZA KAMBA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA EBOLA
Global News

AFISA wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mapambano dhidI ya maradhi ya Ebola, ameionya jumuiya ya kimataifa isilegeze kamba katika harakati za kuyatokomeza maradhi hayo hatari. Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf mjni Monrovia, afisa huyo Anthony Banburry amesema ingawa zipo dalili za kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo, kila mtu anapaswa kuendelea kuwa makini. Banburry amesema Umoja wa Mataifa umejenga vituo vya kupambana na Ebola, na inahitaji watu wa kujitolea kuviendesha vituo hivyo. Wakati...

Like
259
0
Wednesday, 05 November 2014
MAREKANI KUPELEKA RASIMU YA VIKWAZO UMOJA WA MATAIFA
Global News

MAREKANI imesema itapeleka rasimu ya maazimio ndani ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo dhidi ya Watu wanaozorotesha hali ya kisiasa nchini Sudani Kusini. Rais wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia amesema baadhi ya wanachama wa baraza hilo wanaunga mkono hatua ya kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara ya silaha. Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa. Lakini Mapigano yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za kimataifa kuhakikisha makubaliano ya...

Like
230
0
Wednesday, 05 November 2014