Shirika la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International limesema watu 52 walikufa wakiwa kizuizini Madagascar mwaka uliopita kabla kesi zao hazijasikilizwa wakati nchi hiyo inakabiliwa na mfumo mbovu wa mahakama. Hayo yameelezwa katika ripoti ya Amnesty International iliyotolewa leo ambayo imeonya kuwa asilimia 55 ya watu 11,000 waliofungwa magerezani nchini Madagascar walikuwa wakisubiri kesi zao zisikilizwe kwa mwaka uliopita wa 2017, licha ya wengi wao kukabiliwa na uhalifu wa makosa madogo, ambapo kwa mujibu wa sheria za kimataifa,...
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anasema mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi yalipangwa siku kadhaa kabla ya kutekelezwa. Erdogan amesema hayo alipokua akiwahutubia wabunge chama tawala nchini Uturuki. Amesema Uturuki ina ushahidi mkubwa wa kuthibitisha kuwa mauaji ya Khashoggi yalikuwa yamepangwa na kutekelezwa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2. Erdogan pia anataka washukiwa wafunguliwe mashtaka mjini Istanbul. Anataka Saudi Arabia kutoa majibu kuhusu ulipo mwili wa Khashoggi na ni nani aliyeamuru oparesheni hiyo....
Hong Kong-Zhuhai: Daraja refu zaidi duniani lafunguliwa rasmi, mambo muhimu kulihusu Rais wa China Xi Jinping amefungua rasmi daraja refu zaidi duniani, ambalo limekuwa likijengwa kwa miaka tisa. Daraja hilo, ukijumuisha pia barabara zinazolinganisha pamoja, lina urefu wa 55km (maili 34) ana linaunganisha Hong Kong na Macau na jiji la China bara la Zhuhai. Ujenzi wa daraja hilo umegharimu $20bn (£15.3bn) na umecheleweshwa mara kadha. Kwa kulinganisha, gharama hiyo ni zaidi ya bajeti ya mwaka huu ya Tanzania ambayo ilikuwa...
Ufalme wa Saudi Arabia umetoa rambirambi kwa familia ya mwandishi habari Jamal Khashoggi, aliyeuwawa ndani ya ubalozi mdogo wa falme hiyo mjini Istanbul, huku kadhia hiyo ikizidi kuuandama. Utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia mapema leo ulitoa rambi rambi zake kwa familia ya mwandishi habari Jamal Khashoggi aliyeuawa kwenye ubalozi wake mdogo huko mjini Istanbul,Uturuki. Mrithi wa ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman amezungumza na mtoto wa Khashoggi kwa njia ya simu. Mfalme Salman pia ametoa rambirambi kwa familia...
Rais donald Trump amesema siku ya Jumamosi(20.10.2018) kwamba Marekani itajitoa kutoka mkataba wa enzi za vita baridi ambao unafuta aina ya silaha za nyuklia kutokana na ukiukaji unaofanywa na Urusi. Hatua hiyo imeelezwa na afisa mmoja wa Urusi kuwa ni jaribio hatari la kuibana nchi hiyo. Mkataba unaojulikana kama Intermediate-Range Nuclear Forces Treaty, uliojadiliwa na kufikia makubaliano wakati wa utawala wa rais Ronald Reagan na kiongozi wa Urusi wakati wa enzi za Umoja wa kisovieti...
Nchi tatu zenye ushawishi mkubwa barani Ulaya, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimelaani vikali mauaji ya mwandishi Jamal Khashoggi na kuitaka Saudi Arabia kutoa ufafanuzi wa kina haraka iwezekanavyo. Taarifa ya pamoja ya mataifa hayo yanaitaka Saudia kutoa vielelezo vya kina juu ya madai kuwa Khashoggi aliuawa wakati akijaribu kupigana ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul, Uturuki. Rais wa Marekani Donald Trump pia amebainisha kuwa “hakuridhishwa” na maelezo hayo ya Saudia. Rais wa Uturuki Racep Tayyip...
Rais wa Marekani Donald Trump amekiri huenda mwaandishi habari wa Saudi Arabia Jamal Kashoggi amefariki na kutishia kuchukuwa hatua kali iwapo itathibitika viongozi wa Saudi Arabia walihusika na kifo chake. Onyo la Rais huyo wa Marekani limekuja wakati serikali yake ikizidisha ukali juu ya kupotea kwa Mwaandishi Habari Jamal Khasoggi kulikoibua ghdhabu ya Kimataifa. Trump amesema kwa sasa wanasubiri majibu ya uchunguzi kabla ya kutoa taarifa ya aina yoyote. Kabla ya Trump kuzungumza siku ya Alhamisi utawala wake ulitangaza kuwa...
Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri na kumteua Dkt Richard Sezibera kuwa waziri mpya wa mashauri ya nchi za nje. Jenerali James Kabarebe aliyekuwa mtu wa karibu sana na Rais Kagame amepoteza wadhifa wake kama waziri wa ulinzi na badala yake akateuliwa mshauri wa rais katika masuala ya usalama. Katika mabadiliko makubwa na ya kushtukiza aliyofanya Rais Kagame wizara 8 kati ya 23 zimepata mawaziri wapya zikiwemo wizara nyeti tatu, wizara ya ulinzi...
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameamua kuuweka kando mpango wao wa kuitisha mkutano maalum juu ya mkataba wa kupeana talaka na Uingereza uliokuwa umepangwa kufanyika katikati ya mwezi ujao. Mjumbe mkuu wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungunzo na Uingereza Michel Barnier amesema pande hizo mbili zinahitaji muda zaidi. Barnier amesema muda zaidi unahitajka ili kuweza kupiga hatua muhimu. Kwenye mkutano wao wa siku ya Jumatano viongozi wa Umoja wa Ulaya walisema, licha ya kufanyika mazungumzo ya kina, hatua...
Maafisa nchini Urusi wamesema mwanafunzi mmoja amefanya mashambulizi katika chuo kimoja cha ufundi katika eneo la Crimea, wanafunzi 19 wameuwawa katika kadhia hiyo huku watu wengine na zaidi ya 40 walijeruhiwa. Taarifa ya Sergei Aksyonov, kiongozi wa kikanda huko Crimea, ndio kauli ya hivi karibuni katika mfululizo wa maelezo yanayo badilika badilika kutok kwa maafisa wa Urusi kuhusu nini hasa kilichotokea katika Chuo cha ufundi kilicho katika mji wa pwani ya bahari nyeusi wa Kerch. Maafisa hao kwanza waliripoti kwamba mlipuko...
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, Staffan De Mistura, ametangaza siku ya Jumatano kwamba atajiuzulu mwishoni mwa mwezi ujao wa Novemba kutokana na sababu za kibinafsi. De Mistura amesema anajiuzuku ili awe na muda na familia yake. “Sababu za kibinafsi za kujiuzulu si afya, ni familia kimsingi,” alisema de Mistura wakati alipozungumza na waandishi wa habari mjini New York. “Kwa hiyo hakuna haja ya kubahatisha kuhusu hilo. Mimi ni mzima sina neno na hata sijachoka, kwa...