Global News

Habari Kwa Picha Mazishi ya King Majuto
Global News

...

1
2155
0
Friday, 10 August 2018
Shambulizi la Skripal: Marekani kuiwekea vikwazo Urusi, kuanzia Agosti
Global News

Marekani imepanga kuweka vikwazo vipya kwa Urusi ikiwa ni kujibu kitendo cha shambulizi la sumu la afisa wa zamani wa usalama wa Urusi Sergei Skripal na mtoto wake wa kike nchini Uingereza. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Heather Nauert, amesema nchi yake imegundua kuwa Urusi ilitumia kemikali hatari kumshambulia Skripal na binti yake wa kike jambo ambalo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Hii ni mara ya tatu Marekani inaiwekea vikwazo nchi fulani kwa kukiuka sheria...

Like
416
0
Thursday, 09 August 2018
Tarehe kama ya leo na mwezi kama wa leo, Agost, 4 , 1961 alizaliwa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Hussein Obama
Global News

Tarehe kama ya leo na mwezi kama wa leo, Agost, 4 , 1961 alizaliwa Rais wa 44 wa Marekani, Barack Hussein Obama, huko Honolulu, Hawaii, Marekani. Obama alikuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika kushika nafasi hiyo ya urais nchini Marekani ambapo aliongoza taifa hilo kubwa Duniani kuanzia Januari 20, 2009 mpaka Januari 20, 2017 kupitia Chama cha Democratic Party, akichukua nafasi ya Rais George W Bushi. Obama alishawai kuwa Senate wa Jimbo la Illinois kuanzia January 3, 2005...

Like
491
0
Saturday, 04 August 2018
Emmerson Mnangagwa ashinda uchaguzi wa urais Zimbabwe
Global News

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zimbabwe kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo. Katika majimbo 10 yote yalioyotangazwa, Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 50.8 ya kura kwa asilimia 44.3 alizopata mgombea wa chama cha upinzani Nelson Chamise. Polisi waliwaondoa upinzani wakati wa kutangazwa matokeo baada ya kukataa kuyakubali matokeo hayo. Mwenyekiti wa chama cha MDC Alliance, Nelson Chamisa amesema kuhesabiwa kwa kura hakukufanyiwa uhakiki. Kwa ushindi wa asilimia 50 wa Mnangagwa umesababisha aepuke...

Like
409
0
Friday, 03 August 2018
Uchaguzi Zimbabwe: Ghasia zazuka kati ya upinzani na maafisa wa usalama
Global News

Ghasia zimezuka nchini Zimbabwe kati ya wafuasi wa upinzani na vikosi vya usalama katika mji mkuu wa Zimbabwe huku kukiwa na maandamano dhidi ya kucheleweshwa kwa matokeo ya uchaguzi Magari yaliobeba maji ya kuwatawanya waandamanaji na vitoa machozi yalitumiwa katika barabara muhimu za mji wa Harare baada ya wafuasi wa chama cha upinzani cha MDC Alliance kuweka vizuizi katikati ya mji huo. Mtu mmoja aliyekuwa miongoni mwa waandamanaji ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi. Muungano wa Ulaya umeonyesha wasiwasi wake...

Like
391
0
Thursday, 02 August 2018
Mtoto Mchanga Ajeruhiwa Na Chui Nchini India
Global News

Mtoto mchanga wa miezi minne katika jimbo la Magharibi mwa India la Gujarat amejeruhiwa baada ya chui kumnyakua kutoka mikononi mwa mama yake. Mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu kwa majeraha aliyoyapata, pamoja na Mama yake kwani na yeye pia alijeruhiwa. Mama huyo alikuwa amembeba mtoto wake huku akiwa ameketi nyuma ya mumewe ndani ya gari wakati waliposhambuliwa na chui huyo. Kilio cha baba yake cha kuomba msaada kilisikika kwa wanakijiji kilichopo jirani ambao walikimbia na kumuondoa mnyama huyo. “Walianza kupiga...

Like
771
0
Tuesday, 31 July 2018
Wengi Wajitokeza Kwnye Vimbabwe
Global News

Milolongo mirefu imeshuhudiwa katika vituo vya kupigia kura, kwenye uchaguzi ambao chama cha upinzani kinatarajia ushindi dhidi ya chama cha ZANU PF ambacho kimeitawala Zimbabwe tangu ijipatie...

Like
433
0
Tuesday, 31 July 2018
Moto mkubwa waunguza msitu na kuua watu 20 Ugiriki
Global News

Moto mkubwa uliozuka na kuunguza msitu nchini Ugiriki umeua watu 20, huku mamlaka nchini humo zikisema kuwa zinahitaji msaada wa kimataifa ili kukabiliana na moto huo. Mamia ya wafanyakazi wa vikosi vya zima moto,wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo,huku watu wakiwa wameyakimbia makazi yao katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa taifa hilo Athens. Kikosi cha uokoaji kinaendelea na jitihada za kuwapata watalii 10 ambao walitoweka katika harakati za kujiokoa na moto huo. Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis...

Like
603
0
Tuesday, 24 July 2018
Trump aionya Iran ‘isiijaribu Marekani’, ajibizana na Hassan Rouhani
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani wamejibizana vikali na kutoa vitisho huku uhasama baina ya mataifa hayo mawili ukizidi. Bw Trump ameandika kwenye Twitter, kwa herufi kubwa, kwamba “Iran itapata madhara ambayo ni wachache sana wamewahi kukumbana nayo katika historia” iwapo itaitishia Marekani. Bw Rouhani awali alikuwa amesema kwmaba vita na Iran vitakuwa “vita zaidi ya vita vingine vyote”. Mwezi Mei, Marekani ilijitoa kutoka kwa mkataba wa nyuklia na Iran ambao ulikuwa umehusisha Iran...

Like
661
0
Monday, 23 July 2018
Rais Trump kumualika Putin Washington
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump anakusudia kumwalika Washington, Rais wa Urusi Vladmir Putin baadaye mwaka huu, licha ya kuendelea kuwepo ukosoaji juu ya mkutano wao uliofanyika Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Finland Helsinki. Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sara Sanders amesema majadiliano kuhusiana na ziara hiyo tayari yameanza. Hata hivyo, Kiongozi wa maseneta kupitia chama cha Democrat nchini humo Chuck Schumer ameupinga mualiko huo mara moja kwa kusema kuwa Rais Trump hapaswi tena kukutana ana kwa ana na...

Like
358
0
Friday, 20 July 2018
Kenya kuanzisha usafiri wa magari ya nyaya angani
Global News

Serikali ya Kenya ina mpango wa kuanzisha usafiri wa magari ya nyaya angani mwakani. Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la huduma za kivuko cha feri nchini Kenya – Bakari Gowa. Gowa ameeleza kwamba tayari magari hayo yataanza kutengenezwa mwezi ujao huko Ujerumani. “Itachukua kama mwaka mmoja hivi magari hayo kutengenezwa kisha yataletwa Kenya mwaka ujao yaanze kazi ya kubeba watu angani kuwavukisha katika kivuko cha Likoni,” anasema Gowa. Je, magari haya ya nyaya yatasafirisha watu vipi?...

Like
502
0
Thursday, 19 July 2018