Marekani na Korea Kusini zimekubaliana kuweka mfumo wenye utata wa ulinzi dhidi ya makombora, kama njia ya kukakabiliana na vitisho vinayoendelea kutoka kwa Korea kaskazini. Mfumo huo wa ulinzi unaowekwa katika maeneo yenye milima mirefu kudhibiti mashambulizi ya makombora utawekwa kujibu vitisho tisho kutoka Pyongyang, ilieleza taarifa. Haijabainika wazi ni wapi mtambo huo utawekwa na hatimae ni nani ataudhibiti. Uchina, ambayo imekuwa ikipinga mara kwa mara mpango huo, imepinga mfumo huo tena kupitia wajumbe wa korea Kusini na Marekani....
Maafisa watano wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi. Maafisa wengine sita wanauguza majeraha. Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha. Mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema amesema maafisa wa polisi bado wanakabiliana na mshukiwa mmoja ambaye anadaiwa kujibanza katika jumba linalotumiwa kuegesha magari. “Mshukiwa huyo ambaye tunawasiliana naye amewaambia maafisa wetu...
Ile Setelite ya Juno iliiyosafiri kwa miaka mitano kwenda katika sayari ya Jupita sasa inakaribia kufika kwenye sayari hiyo.Wanasayansi wanakadiria setelite hiyo itafika muda mfupi ujao majira ya saa 12:15 asubuhi hii kwa saa za afrika mashariki. Setilite hiyo kama itafanikiwa kufika ilipokusudiwa kwenye sayari hiyo inatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja na nusu kuchunguza sayari jinsi...
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametua nchini Uganda katika ziara ya kwanza kabisa kwa kiongozi wa taifa hilo la kiyahudi kuzuru Afrika tangu mwaka wa 1987. Ziara hiyo ya siku 5 imeanzia Uganda, na kisha waziri Netanyahu anatarajiwa kuzuru Kenya, Rwanda na kisha Ethiopia. Ilikuwa kihoja kwa wageni waalikwa kuingia kwenye uwanja huo wa ndege kwani usalama uliimarishwa huku maafisa wa usalama wa Israeli wakishika doria na mbwa na walenga shabaha, mbali na upekuzi wa kawaida wa maafisa wa...
Saudia inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea Mecca kwa Hajj ya mwaka huu ambalo ni kongomano kubwa la Waislamu kutoka kote duniani. Hatua hiyo inafuatia mkanyagano uliotokea mwaka uliopita ambapo zaidi ya mahujaji 750 wanaaminikia kuuawa huku wengine 900 wakijeruhiwa. Bangili hizo zitakuwa na habari za kibinafsi za kila hujaji pamoja na zile za matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji hao. Takriban kamera 1000 pia zimewekwa. Bangili hiyo ya utambulisho itukuwa na habari muhimu kama vile...
Uingereza imezuia kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ulaya ambapo itakuwa mara ya kwanza kufanyiwa hivyo kwa miaka 40. Waziri Mkuu, David Cameron, hatakuwa mezani wakati viongozi wengine 27 wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya watakuwa wakihudhuria mkutano usio rasmi juu ya hatma ya muungano huo baada ya kuondoka kwa Uingereza. Uingereza imeambiwa ianzishe mpango wake wa kuondoka katika jumuiya hiyo bila kuchelewa. Rais wa Jumuiya ya Ulaya, Jean-Claude Junker, amesema kuwa shughuli za kutegua kujiondoa kwa Uingereza...
Profesa mmoja wa chuo kikuu amesifiwa nchini Ivory Coast kwa kumbeba mtoto wa mmoja wa wanafunzi wake mgongoni wakati wa masomo. Picha za Honore Kahi wa chuo cha Bouake, zimesambaa pakubwa kwenye mitandao ya kijamii. Alisema aliamua kumsaidia mwanamke katika darasa lake wakati mtoto alianza kulia. Picha zilizochukuliwa na mwanafunzi mwingine zinamuonyesha, bwana Kahi akifunza huku mtoto akiwa...
Korea Kusini, Marekani na Japan zimefanya zoezi la ushirikiano la kukabiliana na makombora katika maji ya jimbo la Hawaii. Hatua hiyo inajiri kufuatia msururu wa majiribio ya makombora ya masafa mafupi katika miezi ya hivi karibuni inayofanywa na Korea kaskazini. Majaribio mengi hatahivyo hayakufanikiwa lakini ufanisi wa kombora la sita hivi majuzi ulilishangaza eneo hilo. Korea Kaskazini ambayo imefanya majaribio manne ya mokombora ya kinuklia imesema kuwa zoezi hilo ni la uchokozi wa kijeshi. Vyombo vya habari vimesema kuwa Marekani...
Uchina inasema kuwa itaanza kuwatembeza kwa meli raia wanaotaka kuzuru visiwa vinavyozozaniwa vilivyoko kusini mwa bahari ya China. Vyombo vya habari vya serikali vinasema kuwa miaka minne ijayo, ziara hizo zitakuwa zikitoka kisiwa cha Hainan kabla ya kuelekea katika kisiwa chengine cha Nansha na kisha Spratley. Mapema juma hili, kampuni kubwa ya meli, Cosco, ilitangaza kuwa itaanzisha ziara za meli katika visiwa vingine vilivyoko katika eneo la kusini mwa bahari ya China, Paracels. Kutokana na shughuli kadhaa za kijeshi na...
Baadhi ya vituo vya redio na runinga katika mji mkuu Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimefunga matangazo yake kuanzia leo, ikiwa ni ishara ya kuanza mgomo kufutia makampuni ya simu za mikononi kupandisha gharama za huduma za intaneti. Ni karibu majuma matatu sasa, tangu gharama ya huduma hiyo muhimu ilipoongezwa ghafla kwa asilimia mia moja. Na ili kushinikiza serikali na makampuni hayo kupunguza gharama za intaneti, raisi wa muungano wa wandishi wa habari nchini humo alitoa mwito kwa...
Mtoto aliyezaliwa mwezi mmoja baada ya baba yake kufariki amegusa hisia za mamilioni ya watu ulimwenguni katika mitandao ya kijamii kupitia picha inayomuonyesha mtoto huyo akitabasamu akiwa amekumbatiwa na gloves za marehemu baba yake na pembeni yake amewekewa kofia ambavyo vyote vilikuwa vikitumiwa na baba wa mtoto huyo kujikinga wakati anaendesha pikipiki katika enzi za chai wake. Katika chapisho la Facebook lilitolewa na mpiga picha Kim Stone limeelezea jinsi ambavyo baba wa mtoto huyo alivokuwa na mapenzi makubwa ya kuendesha...