Waandamanaji wanapanga kutumia panya 200 katika maandamano katika mji wa Nyeri mkoa wa kati nchini Kenya kulingana na gazeti la the Star nchini humo. Gazeti hilo limemnukuu mshirikishi wa maandamano hayo John Wamagata akisema ”tutaleta panya 200 na kuwatembeza katikati ya mji”. Gazeti hilo linaongezea kwamba maandamano hayo yanayopangwa kufanyika wiki ijayo yanapinga mapendekezo ya bunge la kaunti hiyo kutumia shilingi milioni 75 kujenga klabu ya kuimarisha afya. Klabu hiyo itakuwa na eneo la kunyosha misuli,eneo la kuoga kwa...
Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshtumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu wasiruhusiwe kuingia Marekani. Obama amesema hiyo ‘si marekani wanayohitaji.’ ”Kuwabagua Waislamu wa Marekani kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama,na kuongeza tofauti iliopo kati ya nchi za magharibi na zile za kislamu”, Obama alisema Siku ya Jumatatu bwana Trump, aliongezea kuhusu mpango wa kupiga marufuku nchi zote ambazo zina historia ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya...
Kamati ya dharura ya shirika la afya duniani imetoa tathmini kuwa kuna uwezekano mdogo kidogo cha maambukizi ya virusi ZIKA kuenea katika mataifa mengine ,hivyo mashindano ya Olympic hayana haja ya kuhamishwa nchini Brazil.Ingawa tayari kulikuwa na wito wa michuano hiyo ya Rio kuahirishwa au kuhamisha mashindano hayo. Shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa mara nyingine limetoa angalizo la awali kukataza watu kutosafiri au kufanya biashara katika maeneo ambayo kwa sasa yana virusi vyua ZIKA. Hata hivyo shirika hilo limewataka...
Wabunge sita nchini Kenya wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani kufuatia madai ya kutoa matamshi ya chuki. Siku ya Jumapili mbunge mmoja anayegemea upande wa serikali alidaiwa kutaka kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga. Wabunge hao ni Moses Kuria, Kimani Ngunjiri na Ferdinand Waititu kutoka kwa upande wa serikali na Junet Mohammed Aisha Jumwa,Johnson Muthama na Timothy Bosire upande wa upinzani. Bw Kuria anadaiwa kuitisha kuuawa kwa Raila kupitia lugha ya kikikuyu.Hathivyo amekana kutoa matamshi...
Ripoti kutoka Orlando Marekani zasema Omar Mateen, mtu aliyewafyatulia risasi na kuwaua watu 49 katika klabu moja ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, alikuwa akitembelea klabu hiyo iitwayo Pulse mara kwa mara. Wahudumu na meneja wa klabu hiyo amenukuliwa na magazeti ya Marekani akisema kuwa, ameshawahi kumuona Mateen, hata akinywa pombe katika eneo hilo. Naye mkewe wa zamani Sitora Yusufiy, amemwelezea Mateen kama mtu aliyekuwa na tabia za ugomvi wa mara kwa mara na kutaka kupigana na watu na...
Eritrea imeishtumu Ethiopia kwa kutekeleza shambulio katika mpaka wake ambao una ulinzi mkali. Wakazi katika eneo la Tsorona wanasema wamesikia milio ya risasi na kuona wanajeshi wakielekea katika mpaka. Hata hivyo Waziri wa habari wa Ethiopia amesema hafahamu lolote kuhusu vita hivyo. Zaidi ya watu laki moja walifariki katika mapigano yaliyodumu mika miwili na nusu katika ya mataifa yote mawili. Kamati ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa eneo linalozozania linapaswa kuwa la Eritrea, lakini Ethiopa haijawahi kukubali uamuzi huo. Mwandishi...
Takriban maafisa 302 wa polisi wamefutwa kazi nchini Kenya kwa kukataa kukaguliwa tangu mpango huo wa kutaka kukabiliana na ufisadi kuanzishwa mwaka 2013,kulingana na tume inayotekeleza ukaguzi huo. Hayo yalibainishwa na Jonhston Kavuludi ,anayeongoza tume hiyo ya huduma za maafisa wa polisi huku maafisa wa polisi wakijiandaa kuhojiwa na jopo katika mji wa magharibi wa Kisumu. Ukaguzi huo ni mpango wa uma na hufanywa mbele ya kamera ambapo maafisa uhojiwa kuhusu mali na fedha wanazomiliki huku mgongano wowote wa maslahi...
HILLARY CLINTON amejitangazia rasmi ushindi kwenye kura za mchujo za chama chake cha Democratic baada ya kushinda majimbo kadhaa muhimu kwenye chaguzi za jana na hivyo kujiimarishia nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa kwanza mwanamke wa urais wa Marekani. Hata hivyo mpinzani wake, Bernie Sanders, amekataa kujitoa kwenye kinyang’anyironi na badala yake ameapa kusonga mbele hadi dakika za mwisho. Kwa upande mwengine, mgombea mteule wa chama cha Republican, Donald Trump, amejizolea ushindi mkubwa kwenye majimbo ya New Mexico,...
ampuni ya kuzalisha umeme nchini Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya habari ikiomba radhi kwa ukosefu wa umeme Kwa hapo jana. Hilo sio jambo geni. Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani Afrika Hata hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban saa nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa ! Nyani. Amini usiamini, KENGEN imempata nyani mmoja katika eneo maalum lenye...
wa aliyekuwa bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali, umewasili mjini Louisville, Kentucky, ambako atazikwa siku ya Ijumaa. Mwili wa bondia huyo wa zamani ulisafirishwa kwa msafara wa magari kutoka uwanja wa ndege wa Louisville . Mazishi yake yanatarajiwa kuwa hafla kubwa ya umma. Ali alikuwa mmoja wa wanamichezo maarufu zaidi duniani katika karne hii ya...
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limewahimiza watu wanaotoka katika sehemu zilizoathirika na virusi vya Zika kuzingatia mbinu za kujikinga endapo mtu anafanya mapenzi au kujiepusha na ngono kwa muda wa wiki nane. WHO imeongeza kwamba ni muhimu kwa wanawake kuepuka kupata ujauzito kwa miezi sita iwapo mwenzake wa ndoa amekuwa na dalili za virusi vya ugonjwa huo. Wiki iliyopita shirika hilo lilisema kuwa hakuna sababu ya kujiepusha na michezo ya Olimpiki mjini Rio mwezi...