KANDA ya video iliyotumwa kwa maafisa wa serikali ya Nigeria kutoka kwa kundi la wapiganaji wa Boko Haram imewaonesha baadhi ya wasichana waliotekwa eneo la Chibok wakiwa hai. Taarifa zaidi zinaeleza kwamba ni kipindi cha miaka miwili sasa tangu kutekwa kwa wasichana 276 kutoka shule moja katika mji wa Chibok nchini humo. Hata hivyo ni wasichana 15 tu, wanaoonekana kwenye kanda hiyo ya video ambayo inaaminika ilipigwa Siku ya sikukuu ya Krismasi mwaka...
KITUO cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) kimethibitisha kwamba virusi vya Zika husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa. Hayo yamejiri kufuatia kuwepo kwa mjadala mkubwa na sintofahamu kuhusu uhusiano kati ya virusi hivyo na watoto kuzaliwa na vichwa vidogo tangu kuongezeka kwa visa vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil. Mkurugenzi mkuu wa CDC Tom Frieden amesema hakuna shaka kwamba virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzalwia na vichwa vidogo, tatizo ambalo kwa Kiingereza hujulikana kama...
MUUNGANO wa ulaya umelaani hatua ya rais wa Macedonia, Gjorge Ivanov, kuwasamehe wanasiasa waliohusishwa na ufisadi. Kamishna anayehusika na upanuzi wa muungano huo Johannes Hahn, amesema kuwa msamaha huo hauambatani na uelewa wake wa sheria na hivyo, unahatarisha lengo la Macedonia kuwa mwanachama wa muungano huo. Taifa hilo limekumbwa na mzozo unaohusiana na madai kwamba chama tawala na wakuu wa idara ya ujasusi , walidukua simu za zaidi ya watu alfu ishirini wakiwemo waandishi wa habari na maafisa wa idara...
KESI ya serikali ya Afrika Kusini inayopinga kuachiliwa awali kwa muuaji wa shujaa aliyepinga ubaguzi wa rangi Chris Hani imeanza kusikilizwa katika mahakama kuu mjini Pretoria nchini Afrika kusini. Waziri wa sheria Michael Misutha anaamini kuwa mahakama ilifanya makosa wakati ilipotoa uamuzi kuwa raia wa Poland Janusz Walus aachiliwe huru. Kuachiliwa kwake kulizua ghadhabu sehemu nyingi nchini Afrika Kusini huku Mkewe Hani akiutaja uamuzi huo kuwa ni huzuni kubwa kwa Afrika Kusini.....
WAZIRI wa mambo ya nje wa Italia amewasili mjini Tripoli Libya, kwa mazungumzo na kiongozi wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa nchini Libya Fayez Seraj. Paolo Gentiloni ni afisa mkuu wa kwanza wa bara la Ulaya kufanya ziara rasmi nchini Libya tangu utawala mpya unaoungwa mkono na Umoja wa mataifa kuwekwa katika mji mkuu wa Libya majuma mawili yaliyopita. Italia pamoja na mataifa kadhaa ya dola za kimagharibi yaliyoitawala Libya miaka iliyopita yameahidi kuisaidia serikali hiyo mpya kwa imani...
AFISA mmoja wa kijeshi wa cheo cha juu nchini Korea Kaskazini, ambaye alikuwa akisimamia masuala ya ujasusi ameihama nchi hiyo na kuelekea Korea Kusini. Afisa huyo hajatajwa jina lakini wizara ya ulinzi nchini Korea Kusini imesema kuwa alikuwa afisa wa cheo cha juu na aliondoka nchini Korea Kaskazini mwaka uliopita. Shirika la habari la Yonhap nchini Korea Kusini, limenukuu taarifa zilizosema kuwa kanali huyo alitajwa kuwa shujaa sambamba na wale walioihama Korea...
RAIS wa Marekani Barack Obama amekiri kwa mara ya kwanza kwamba serikali yake imefeli katika kutatua mzozo wa Libya. Amesema hilo huenda ndilo “kosa kubwa” zaidi alilolitenda wakati wa utawala wake. Obama pia amesema Marekani haikuwa na mpango mahususi wa jinsi Taifa hilo litakavyotawaliwa baada ya kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar...
MWANAHABARI aliyesaidia kundi la al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa. Hassan Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema asubuhi ya leo baada ya kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi nchini humo. Hassan Hanafi, alipatikana na hatia ya kuwaua Sheikh Noor Mohamed Abkey (mhariri wa shirika la habari la SONNA), Sa’id Tahlil Warsame (mkurugenzi wa HornAfrik), na Mukhtar Mohamed Hirabe (mkurugenzi wa Radio Shabelle), na wanahabari wengine...
JIMBO la magharibi mwa Sudan Darfur, leo linapiga kura ya maoni, miaka 13 baada ya kuanza kwa mzozo wa wenyewe kwa wenyewe uliosababisha watu laki 3, kupoteza maisha. Kura ya maoni itaamua kama Darfur itakuwa na majimbo matano au jimbo moja, ambapo raia watakuwa na siku mpaka ya jumatano kuamua. Marekani imeeleza hofu yake kuwa kura hiyo haitakuwa ya haki, lakini Rais Omar al-Bashir amesisitiza kuwa itakuwa huru na haki. Ikiwa ni hatua ya mwisho ya mchakato wa...
KUNDI la pili la wahamiaji wanatarajiwa kurejeshwa nchini Uturuki kutoka Ugiriki baadaye hii leo, kama sehemu ya mkataba ulioafikiwa na Muungano wa Ulaya, wa kupunguza idadi wa wakimbizi wanaofika Ulaya. Kundi la kwanza liliwasili Uturuki, siku ya Jumatatu, lakini tangu wakati huo mpango huo umekwama kwa sasa ambapo idadi kubwa ya wahamiaji wanaomba hifadhi nchini Ugiriki. Inaaminika kuwa boti zingine mbili zitawasili leo, Ijumaa, ikiwa na wahamiaji waliofukuzwa kutoka Ugiriki chini ya mkataba huo wa...
VIKOSI vya waasi wa Syria wamevirejesha nyuma vikosi vya wanamgambo wa dola ya kiislamu wa Islamic State nje ya mji ambao pande zote mbili wanauwinda kuwa chini ya himaya yake upande wa Kaskazini mwa Syria, baada ya siku kadhaa za mapambano makali. Mji wa Al-Rai,ulioko jirani na jimbo la Aleppo ,ni ngome ya wanamgambo hao wa IS ambao uko kwenye mpaka unaoingia nchini Uturuki hadi kuingia Syria. Waasi hao wa Syria wamewahi kuhusika na matukio ya kukera ingawa...