Global News

UTAWALA WA SERIKALI YA KIDINI TRIPOL WAKABIDHI MAMLAKA KWA VIONGOZI WANAUNGWA MKONO NA UN
Global News

UTAWALA wa serikali ya kidini katika mji mkuu wa Tripol nchini Libya umekabidhi mamlaka kwa viongozi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Uamuzi huo ulichapishwa katika mtandao wa wizara ya sheria. Mamlaka mpya ya Libya wiki iliyopita imehamia mji mkuu,Tripoli katika harakati za kutaka kutawala nchi nzima, huku kukiwa na ngome nyingine mbili tofauti za utawala Mashariki mwa nchi hiyo. Hatua hii ni matokeo ya jitihada za umoja wa mataifa kuunda serikali ya pamoja ili kuweza kuondoa mgawanyiko wa utawala...

Like
250
0
Wednesday, 06 April 2016
TED CRUZ AMBWAGA TRUMP JIMBO LA WISCONSIN
Global News

MGOMBEA urais wa chama cha Republican nchini Marekani Ted Cruz ameshinda mchujo wa chama hicho katika jimbo la Wisconsin, hilo likiwa pigo kubwa kwa Donald Trump. Katika chama cha Democratic, Bernie Sanders alipata ushindi mkubwa dhidi ya Hillary Clinton anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa. Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na katika kura za maoni chama cha Republican, lakini kuna wasiwasi kwamba huenda akashindwa kupata wajumbe wa kumuwezesha kuidhinishwa moja kwa moja kuwa...

Like
289
0
Wednesday, 06 April 2016
RAIS WA YEMEN AWATIMUA KAZI WAZIRI MKUU NA MAKAMU WA RAIS
Global News

RAIS wa Yemen Abedrabbo Mansour Hadi amemfukuza kazi Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Khaled Bahah kutokana na kile alichoeleza utendaji mbovu ndani ya serikali. Mabadiliko haya yanakuja ikiwa ni wiki moja kabla ya kuanza kwa hatua ya kusimamishwa mapigano kati ya pande mbili zinazohasimiana katika mgogoro nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la serikali nchini humo, Rais Hadi amemteua Ahmed Obaid bin Daghr kuwa waziri mkuu huku akimteua Meja Jenerali Ali...

Like
255
0
Monday, 04 April 2016
SYRIA:VIKOSI VYADHIBITI MJI WA AL-QARYATAIN
Global News

VIKOSI vya Jeshi nchini Syria na washirika wake vimedhibiti tena mji wa Al-Qaryatain kutoka mikononi mwa Islamic State, ukiwa ni muendelezo wa mapambano dhidi ya kundi hilo. Hatua hiyo imekuja siku kadhaa baada ya kundi la IS kuondolewa katika eneo la karibu na mji wa Palmyra. Wanamgambo wa IS waliuteka mji wa Al-Qaryatain mwezi Agosti, na kuwateka mamia ya wakazi wa mji huo wakiwemo Wakristo ambao wengi wao waliachiwa huru...

Like
219
0
Monday, 04 April 2016
VIONGOZI 72 DUNIANI WAHUSIKA NA KAMPUNI YA SIRI
Global News

STAKABADHI za siri za shirika moja la kisheria la Panama zilizopatikana na gazeti moja la Ujerumani zimeonyesha viongozi zaidi ya 72 wakuu wa nchi wa zamani na wale waliopo madarakani wanahusika na kampuni hiyo ya kisiri iliyowasaidia wateja wao kukwepa kulipa kodi, utakatishaji fedha, kukiuka mikataba na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa. Kwa mujibu wa nyaraka za siri zilizopatikana na gazeti moja la Kijerumani, kampuni hiyo ya Mossack Fonseca imewasaidia watu duniani kote kufungua kampuni kwenye visiwa ambavyo havitozi kodi....

Like
278
0
Monday, 04 April 2016
JESHI LA NIGERIA LAMNASA KINGOZI WA KUNDI LA ANSARU
Global News

JESHI la Nigeria limesema kuwa limemkamata kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye uhusiano pia na kundi la kigaidi la Al Qaeda. Taarifa ya msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo. Kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kundi la Ansaru tawi la Boko Haram kunafuatia kusakwa kwa muda mrefu ambapo Marekani walitoa ahadi ya zawadi ya dola millioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kutiwa nguvuni kwa...

Like
231
0
Monday, 04 April 2016
UGANDA: BESIGYE KUACHILIWA HURU
Global News

MKUU wa kikosi cha polisi nchini Uganda amesema kuwa atawaondoa maafisa wake nje ya nyumba ya kiongozi wa Upinzani Kizza Besigye mara moja. Besigye amekuwa akihudumia kifungo cha nyumbani tangu tarehe 20 mwezi Februari,siku ambayo rais Museveni alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa taifa hilo. Hapo jana Alhamisi, Mahakama ya juu nchini Uganda ilitupilia mbali kesi inayopinga uchaguzi wa rais...

Like
251
0
Friday, 01 April 2016
MJADALA WA USALAMA WA NYUKLIA KUFANYIKA WASHINGTON
Global News

VIONGOZI zaidi ya 50 wa mataifa na serikali pamoja na wawakilishi wa mashirika kadhaa ya kimataifa wanakutana mjini Washington kuzungumzia usalama wa nyuklia. Hofu ya kutokea mashambulio ya kigaidi kutokana na kuibiwa vifaa vya nyuklia na kutapakaa silaha hizo ndio chanzo cha mkutano huo wa kilele ulioitishwa na Rais Barack Obama wa Marekani. Pia kitisho cha nguvu za nyuklia za Korea Kaskazini ni miongoni mwa mada kwenye mazungumzo...

Like
240
0
Friday, 01 April 2016
MAREKANINA CHINA KUSHIRIKIANA DHIDI YA KOREA KASKAZINI
Global News

CHINA imesema mazungumzo baina ya Rais wa nchi hiyo Xi Jinping na Rais wa Marekani Barack Obama yalikuwa yenye manufaa, licha ya kuwa pande hizo mbili hazikuweza kukubaliana juu ya masuala ya udhibiti wa China wa bahari ya China Kusini, pamoja na mpango wa Marekani wa ulinzi wa kutumia makombora dhidi ya Korea Kaskazini. Wakati wa mazungumzo hayo yaliyofanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele juu ya usalama wa silaha za nyuklia, viongozi hao wawili wamekubaliana kuongeza mshikamano utakaohakikisha usalama wa...

Like
249
0
Friday, 01 April 2016
INDIA: 23 WAPOTEZA MAISHA KWA KUANGUKIWA NA DARAJA
Global News

MAMIA ya waokoaji wakiongozwa na majeshi, wahandisi na matabibu wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha katika mji wa India wa Calcutta kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye barabara ya juu iliyoanguka wakati ikijengwa. Maafisa wanasema hadi sasa watu 23 wamekufa na mamia kujeruhuwa na wengine wakiwa bado wamefukiwa na kifusi. Inasadikiwa watu wengi wamefukiwa ambapo hadi sasa tayari watu 23 wamethibitishwa kufariki na mamia wengine kujeruhiwa ambao wanapatiwa...

Like
223
0
Friday, 01 April 2016
TRUMP ABADILI MSIMAMO WAKE JUU YA KUTOA MIMBA
Global News

MGOMBEA urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amebadili msimamo wake muda mfupi baada ya kusema wanawake wanaotoa mimba wanafaa kuadhibiwa, utoaji mimba ukiharamishwa.   Alikuwa ametoa tamko lake katika hafla iliyopeperushwa moja kwa moja na kituo cha runinga cha MSNBC kauli ambayo ilimfanya kushutumiwa vikali.   Lakini muda muda mfupi baadaye, alibadili msimamo wake na kusema ni wahudumu wa afya wanaosaidia wanawake kutoa mimba pekee wanaofaa kuadhibiwa. Utoaji mimba umekuwa halali nchini Marekani tangu 1973...

Like
264
0
Thursday, 31 March 2016