Global News

Bosi ashtakiwa kwa ‘Kujamba’ ofisini
Global News

Mfanyakazi mmoja nchini Australia amefungua mashtaka kwenye mahakama ya rufaa ya nchi hiyo akidai bosi wake alikuwa akimbughudhi ofisini kwa kujamba sana. Awali, mahakama moja ya chini ilifikia uamuzi kuwa hakukuwa na bughudha yeyote katika suala hilo. Hata hivyo, David Hingst anadai kuwa bosi wake wa zamani Greg Short alikuwa “akinyanyuka na kumjambia” karibu mara sita kwa siku. Mwaka jana mashtaka dhidi ya kampuni yake ya zamani na kudai dola milioni 1.28 yalitupiliwa mbali na Mahakama Kuu ya Victoria iliyohukumu...

Like
788
0
Wednesday, 27 March 2019
Trump ‘hakusuka njama na Urusi’ kushinda uchaguzi
Global News

Kampeni iliyoendeswa na rais wa Marekani Donald Trump ‘haikushirikiana na Urusi wakati wa uchaguzi wa 2016, kwa mujibu wa muhtasari wa ripoti ya ya mwanasheria mahususi Robert Mueller iliyowasilishwa kwenye bunge la Congress ,Jumapili. Muhtasari wa ripoti haukuelezea ikiwa Bwana Trump alizuia utekelezwaji wa sheria – lakini pia haikumuhusisha rais na madai hayo. Ripoti hiyo iliwekwa kwa muhtasari kwa ajili ya Congresi na Mwanasheria Mkuu, William Barr. Trump alituma ujumbe wa twitter kujibu muhtasari wa ripoti yake akisema: ”...

Like
533
0
Monday, 25 March 2019
Basi la shule latekwa na kuteketezwa kwa moto
Global News

Basi lililokuwa limebeba watoto wa shule wapatao 51 lilitekwa na dereva wake na kisha kutiwa moto karibu na Milan nchini Italia. Watoto hao wa shule, baadhi yao walifungwa kamba, waliokolewa baada ya kuvunjwa vioo vywa basi hilo upande wa nyuma na hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa vibaya.Watu kumi na wanne waliathiriwa na moshi uliotokana na kuteketea kwa basi hilo. Dereva wa basi hilo alikuwa na umri wa miaka arobaini na saba mwenye uraia wa nchini Italia ingawa ana asili ya kutoka...

Like
633
0
Thursday, 21 March 2019
Janga kubwa’ Msumbiji na Zimbabwe kuathiri Afrika mashariki
Global News

Kimbunga Idai kimesababisha “janga kubwa” katika mataifa ya kusini mwa Afrika na kuathiri laki kadhaa za watu kama sio mamilioni, Umoja wa mataifa unasema. Eneo hilo limekabiliwa na mafuriko katika sehemu nyingi na uharibifu katika nchi za Musmbiji Zimbabwe na Malawi. Huku kukiwa na ripoti kwamba takriban angalau watu 400,000 wameachwa bila ya makaazi Msumbiji ya kati, shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linaonya kwamba huenda ikachukua siku kadhaa kabla ya athari kamili ya “janga la kibinaadamu” kujulikana...

Like
745
0
Wednesday, 20 March 2019
Watu 1000 wahofiwa kufariki kutokana na kimbuga Msumbiji
Global News

Idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Idai nchini Msumbiji sasa huenda ikawa ya juu na kufikia watu 1000 rais Filipe Nyusi amesema. Bwana Nyusi alisafiri kwa ndege katika maeneo yalioathirika zaidi siku ya Jumatatu. Alielezea kuona miili ikielea juu ya mito. Tayari kuna hatari ya maisha ya zaidi ya watoto 100,000 na watu wazima kufuatia kikmbunga hicho huku mito katika maeneo yaliothirika zaidi ikivunja kingo zake , kulingana na shirika la Save the Children. Mafuriko yaliofanyika mapema mwezi huu...

Like
1127
0
Tuesday, 19 March 2019
Watu 10 wamefariki kutokana na uhaba wa chakula
Global News

Zaidi ya watu 10 wameripotiwa kufariki kutokana na ukame katika kaunti ya Turkana nchini Kenya, Wengine zaidi ya 800,000 wakiendelea kuumia kwa makali ya njaa na kiu kwa mujibu wa wizara ya kudhibiti majanga na utumishi wa umma ya kaunti ya Turkana. Serikali ya kaunti hiyo wiki iliyopita ilitoa hakikisho kwamba imeidhinisha mpango wa usaidizi kuwakinga wakaazi kutokana na madhara ya ukame uliopo. Katika kijiji cha Kakwanyang’ Turkana ya Kati, mizoga ya wanyama iliyotapakaa, na miti yaliyokauka inaashiria hali inayoshuhudiwa...

Like
800
0
Monday, 18 March 2019
Watu 49 wauawa katika shambulio kwenye misikiti New Zealand
Global News

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern anasema watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand. Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa mojawapo lililotanda ‘kiza kikubwa’ siku ya leo nchini humo. Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa, kamishna wa polisi Mike Bush anasema, lakini ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo. Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini...

Like
858
0
Friday, 15 March 2019
Tshisekedi na Kabila watangaza serikali ya Muungano
Global News

Kiongozi mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wamesema wameamua kuunda serikali ya muungano kufuatia mazungumzo, shirika la habari la AFP linaripoti. Licha ya ushindi wa rais Tshisekedi — kiongozi huyo amejikuta akilazimika kugawanya uongozi tangu uchaguzi huo wa urais. Mpaka sasa hajafanikiwa kumteua waziri mkuu kutokana na kwamba muungano wa Kabila – Common Front for Congo (FCC) una uwingi katika bunge la taifa. Mkwamo huo umeweka kizuizi kwa maazimio ya Tshisekedi...

Like
872
0
Thursday, 07 March 2019
Auawa na simba aliyemfuga nyumbani kwake
Global News

Mwanamume mmoja ameshambuliwa na simba aliyemfuga nyumbani kwake mashariki mwa Jamhuri ya Czech Michal Prasek alimmiliki simba huyo mwenye miaka 9 na simba jike aliyemfuga kwa ajili ya kuzalisha , hatua inayoarifiwa kuzusha wasiwasi kutoka kwa wakaazi. Babake Prasek aliupata mwili wake ndani ya kizuizi cha simba huyo na kuambia vyombo vya habari kwamba kilikuwa kimefungwa kwa ndani. Wanyama hao waliokuwa wanaishi katika vizuizi tofuati, walipigwa risasi na kuuawa na polisi walioitwa katika eneo hilo. Msemaji wa polisi amewaambia waandishi...

Like
811
0
Wednesday, 06 March 2019
Rubani wa naibu rais William Ruto afariki baada ya helikopta kuanguka Kenya
Global News

Rubani wa naibu rais William Ruto amefariki katika jali ya ndege baada ya helikopta aliyokuwemo kuanguka nchini Kenya. Taarifa katika vyombo vya habari nchini zinaeleza kwamba ndege hiyo ilianguka Jumapili mwendo wa saa mbili usiku katika eneo la Turkana. Inaarifiwa kwamba Kapteni Mario Magonga amefariki pamoja na abiria wengine wanne. Polisi inasema helikopta hiyo imeanguka katika eneo la Labolo, kisiwa chenye milima ya volcano katikakati ya ziwa Turkana – Central Island National Park kaskazini magharibi mwa Kenya. “Taarifa...

Like
968
0
Monday, 04 March 2019
Wanawake walio na maumbo makubwa  nchini Uganda wamewasilisha  malalamiko yao kwa  spika wa Bunge
Global News

Waandalizi wa shindano la wanawake walio na maumbo makubwa nchini Uganda wamewasilisha malalamiko yao kwa spika wa bunge kufafanua madhumuni yao. Wamesema kuwa lengo lao sio kutumia shindano la ‘Miss Curvy Uganda” kuvutia watalii kuja nchini humo. ”Haya ni mashindano ya urembo wa wanawake wanene”alisema Annie Mungoma, mkurugenzi mkuu wa mashindano hayo. Bi. Mugoma aliongeza kuwa mtazamo wao itaondosha fikra za kimagharibi kuwa urembo unamaanisha mtu kuwa mwembamba. ”Tunataka kuwapatia motisha wanawake wenye maumbo...

Like
2074
0
Thursday, 28 February 2019