WAZIRI wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi. Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa hospitali baada ya kuugua. Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa...
BUNGE la Ukraine limeidhinisha hii leo hatua ya kujiuzulu kwa mwendesha mashtaka mkuu nchini humo Viktor Shokin mtu ambaye amekuwa akionekana na nchi za magharibi zinazoiunga mkono Ukraine kama kizingiti katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Marekani imekuwa mara zote ikitaka pafanyike mageuzi kuanzia ngazi za juu katika ofisi hiyo ya mwendesha mashaka. Hata hivyo Wanaharakati wanaopinga rushwa wamekuwa wakisema kwamba ofisi ya mwendesha mashitaka huyo mkuu imekuwa na dhima muhimu katika kuyalinda maslahi ya wala rushwa na kuruhusu...
RIPOTI zimesema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir amedai kuwa anahitaji kuongea na mkewe waliyetengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege. Rais wa Cyprus NicosAnastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi na kwamba wanahakikisha kuwa kila mtu anaachiliwa akiwa salama. Shirika la habari la Cyprus-CYBC limesema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake...
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atachukua nafasi ya Louis van Gaal. Kwa mujibu wa jarida la Don Balonna Mourinho anataka kusajili nyota watatu. Kocha huyo ameshaanza mipango ya usajili kwa kuweka wachezaji kadhaa nyota katika orodha yake akiwemo mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain, kiungo wa Real Madrid James Rodriguez na mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata. Mourinho ameshawahi kufanya kazi na Higuain wakati akiwa Madrid na United wameonyesha kuwa tayari ingawa watalazimika...
WIZARA ya Sheria ya Marekani imesema imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone, mali ya mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple. Wakili wa Marekani Eileen Decker amesema kuna mtu aliisaidia idara hiyo kuifungua Simu hiyo ya iPhone bila kuathiri data zilizohifadhiwa. Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye pamoja na mke wake wanatuhumiwa kuwaua watu kumi na nne kusini mwa California Desemba...
NDEGE ya Misri iliyotekwa nyara imefanikiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus. Taarifa za uchunguzi kutoka kwenye ndege hiyo zimeeleza kuwa ndege hiyo ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Alexandria kuelekea Cairo ilitekwa nyara na watu waliojihami. Msemaji wa shirika la ndege la Misri amenukuliwa akisema kwamba Watekaji hao waliiamrisha ndege hiyo kutua Cyprus baada ya...
MWANAMUME mmoja kutoka Uchina amekiri kuhusika katika njama ya kuiba siri kuu kuhusu mifumo ya kijeshi ya Marekani. Su Bin anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita, ndege za kubeba mizigo na silaha. Bw Su, mwenye umri wa miaka 50, alikiri kufanya kazi na watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la Marekani kuunda ndege...
MAAFISA wa Ufaransa na Ubelgiji wanasema mmoja wa walipuaji wa kujitoa mhanga waliotekeleza mashambulio ya Brussels alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mabomu. Wamesema mshukiwa huyo alihusika katika kuunda mabomu yaliyotumiwa kutekeleza mashambulio ya Paris Novemba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 130. Wakizungumza, bila kutaka kunukuliwa, maafisa hao walisema chembe nasaba za DNA za mshukiwa huyo Najim Laachraoui zilipatikana katika mikanda ya kujilipua iliyotumiwa...
LICHA ya kuongoza kwa mbali kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Marekani kwa chama cha Republican, bilionea Donald Trump ameangushwa na hasimu wake Ted Cruz kwenye kura za mchujo za jimbo la Utah. Wakati zaidi ya nusu ya kura zikiwa zimeshahesabiwa, Seneta Cruz anaongoza kwa takribani asilimia 70, huku Gavana John Kasich wa Ohio na Trump wakiwa nyuma yake. Wiki iliyopita, Gavana Kasich alimshinda pia Trump kwenye uchaguzi wa...
KIONGOZI wa muda mrefu nchini Kongo, Denis Sassou Nguesso, ametangazwa na Tume ya Uchaguzi nchini humo kushinda tena urais, na hivyo kumpa nafasi ya kuendeleza utawala wake wa zaidi ya miongo mitatu sasa. Huku matokeo ya mji mkuu wa kiuchumi na ngome ya upinzani, Pointe-Noire, yakiwa hayajajumuishwa, mkuu wa tume ya uchaguzi, Henri Bouka, amesema Nguesso tayari ana asilimia 67 ya kura. Mwanajeshi huyo wa zamani wa kikosi cha miamvuli kwenye jeshi la Ufaransa na mwenye umri wa...
IDARA ya Haki ya Marekani imesema huenda shirika la upelelezi la FBI limegundua njia ya kufungua simu ya mkononi ya muuaji Syed Rizwan Farook aliyewapiga risasi watu eneo la San Bernardino. Idara hiyo imeiomba mahakama kuahirisha kusikilizwa kwa kesi kati ya shirika hilo dhidi ya kampuni ya utengenezaji wa simu, Apple.ya iPhone Idara hiyo imekuwa ikiishawishi mahakama ilazimishe Apple kufungua simu ya Farook, ambaye yeye na mkewe wanatuhumiwa kufanya shambulizi la bunduki na kuwaua zaidi ya watu 14 katika jimbo...