WAZIRI wa mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders amesema mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya kigaidi ya Paris, Salah Abdeslam, alikuwa anapanga kufanya mashambulizi katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels. Reynders amesema wamepata silaha nyingi, nzito na katika chunguzi za awali tangu kukamatwa kwa mshukiwa huyo, wamegundua mtandao mpya mjini Brussels unaohusishwa naye. Abdeslam anazuiwa katika gereza lenye ulinzi mkali huku akiwa amefunguliwa mashitaka ya mauaji ya kigaidi kwa kuhusika katika mashambulizi ya Novemba 13 mwaka jana mjini Paris...
RAIS wa Marekani Barack Obama ameanza ziara ya kihistoria nchini Cuba, akiwa ndiye rais wa kwanza wa Marekani kuzuru Taifa hilo katika kipindi cha miaka 88 iliyopita. Ziara hiyo ya siku tatu ndiyo kilele cha mazungumzo ya miaka miwili yaliyonuia kurekebisha uhusiano kati ya Marekani dola kubwa zaidi duniani na jirani yake yenye mfumo wa ujamaa. Katika ziara yake Rais Obama atakutana na Rais wa Cuba Raul Castro Pia ameahidi kuangazia masuala ya haki za binadamu, kuwepo mageuzi ya kisiasa...
TAIFA la Korea Kaskazini limerusha makombora mawili ya masafa marefu katika bahari ya mashariki ya pwani yake, siku chache baada ya kiongozi wake Kim Jong-un kuagiza majaribio ya mabomu zaidi ya kinyuklia na silaha nyingine. Marekani imejibu kwa kutoa wito kwa Pyongyang kutozua wasiwasi katika eneo hilo ambao umekua juu tangu Korea Kaskazini ifanye jaribio la nne la mabomu yake ya kinyuklia mnamo mwezi Januari. Korea Kusini imeelezea jaribio hilo la hivi karibuni kama tishio kubwa la usalama na udhibiti...
DONALD TRUMP amepiga hatua katika kukaribia kutwaa tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani baada ya kushinda mchujo katika majimbo matatu makubwa, likiwemo jimbo la Florida. Bilionea huyo kutoka New York ameshinda majimbo ya Illinois na North Carolina.Hata hivyo ameshindwa na John Kasich katika jimbo la Ohio. Mgombea anayeongoza chama cha Democratic Hillary Clinton naye amepanua uongozi wake kwa kupata ushindi majimbo ya Florida, Ohio, Illinois na North...
RAIS wa Urusi Vladimir Putin ametoa amri kwa wanajeshi wake waliopo Syria kurejea nyumbani haraka kwa sababu tayari wametekeleza asilimia kubwa ya malengo yao. Tangazo lake hilo limewaacha wachambuzi wengi wakiwa na mshangao kwani hakukuwa na dalili zozote za kuwepo kwa tukio kama hilo. Aidha Putin ametangaza hilo katika siku ambayo mazungumzo ya amani yameanza upya mjini Geneva Uswisi....
KIONGOZI wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametangaza kwamba Taifa hilo litafanya majaribio ya silaha zake za nyuklia na makombora ya masafa marefu hivi karibuni. Kim Jong-un ametoa Tangazo lake alipokuwa akiongoza maonesho ya teknolojia ambayo inahitajika kuwezesha kombora lenye kilipuzi cha nyuklia kuingia tena ardhini baada ya kurushwa anga za juu. Shirika hilo limemnukuu kiongozi huyo akisema kuwa majaribio hayo yatafanyika na yataisaidia Korea Kaskazini kujiimarisha katika utekelezaji wa mashambulio ya...
CHAMA cha Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kimeshindwa katika uchaguzi wa majimbo, matokeo ya utafiti wa baada ya uchaguzi yanaonesha. Chama cha AfD kinachowapinga wahamiaji, kimeimarika kwa kiwango kikubwa katika majimbo yote matatu. Uchaguzi huo ulitazamwa na wengi kama kigezo cha uungwaji mkono wa sera ya kansela Merkel ya kuwapokea wakimbizi, ambapo zaidi ya wakimbizi na wahamiaji milioni moja waliingia Ujerumani mwaka 2015....
ISRAEL imetoa wito kwa mataifa yenye nguvu duniani kuiadhibu Iran kwa jaribio lake la hivi karibuni la kurusha makombora ya masafa marefu. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Israel inapeleka dai hilo kwa Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani-mataifa ambayo yamesaini mpango wa kuiondoshea Iran vikwazo kwa makubalino ya taifa hilo kuachana na mpango wake wa nyuklia. Netanyahu amesema Iran imekwenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu majaribio ya makombora, na mataifa hayo yenye...
Thomson Joseph Mloyi ambae ni afisa wa polisi nchini Zimbabwe amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yake kwa kusema Rais Mugabe ni mzee sana kuwa kiongozi, Afisa huyo pia anadaiwa kumtusi mke wa Rais Mugabe, Grace kuwa kahaba kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti binafsi nchini humo Tuhuma dhidi yake zilianza asubuhi ya Machi 5 alipoingia katika moja ya kambi katika kambi ya Craneborne na kukuta maafisa wengine wakifanya maandalizi kwa ajili ya kazi . ndipo afisa huyo...
KOREA KASKAZINI imerusha makombora mawili ya masafa mafupi kuelekea Bahari ya Japan, kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini. Mkuu wa majeshi wa Korea Kusini amesema makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 500 kutoka kusini mwa Korea Kaskazini, kabla ya kuangukia pwani ya mji wa kusini mashariki mwa Japan, mapema leo. Tayari Japan imetuma rasmi malalamiko yake dhidi ya Korea Kaskazini kupitia ubalozi wake uliopo mjini Beijing, China, kwa mujibu wa shirika la habari la Japan, Kyodo. Korea...
WAGOMBEA wa urais kupitia chama cha Demokrat nchini Marekani Hillary Clinton na mwenzake Bernie Sanders wamekabiliana vikali kuhusu swala la uhamiaji pamoja na maswala mengine katika mjadala mjini Florida. Mjadala huo uliokuwa moja kwa moja kupitia runinga mjini Miami ulifanyika siku chache tu kabla ya uteuzi wa jimbo la Florida. Huku wajumbe 246 wakiwa watapiganiwa na vigogo hao wawili wa chama cha Demokrat jimbo hilo la Kusini linaelezwa kuwa ni muhimu...