Global News

MUSEVENI: WANAOKOSOA UCHAGUZI HAWAIJUI UGANDA
Global News

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema uchaguzi uliofanyika nchini humo Alhamisi wiki iliyopita ulikuwa wa haki na akasema wanaoutilia shaka hawaielewi Uganda.   Aidha, ametetea hatua ya maafisa wa usalama kumzuilia mgombea mkuu wa upinzani Dkt Kizza Besigye wa chama cha FDC.   Tume ya Uchaguzi ilisema Jumapili kwamba Bwana Museveni alipata ushindi wa asilimia 60.75 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Dkt Besigye aliyepata asilimia 37.35, lakini upinzani umedai kuwepo wizi wa kura na waangalizi wa kimataifa wamesema pia kwamba...

Like
215
0
Monday, 22 February 2016
WANAFUNZI WAPONGEZA MFUMO WA DIVISHENI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
Global News

BAADA ya  Baraza la mitiani Tanzania NECTA kutangaza Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 ,Wanafunzi wa shule ya sekondari pamba jijini Mwanza wameeleza kufurahishwa kwa mfumo wa ufaulu wa divisheni tofauti na mfumo uliokuwepo wa GPA . Wakizungumza na Efm baadhi ya wananfunzi hao wamesema kuwa matokeo hayo yanaonyesha namna mfumo wa divisheni unavyo pima uwezo wa wanafunzi darasani. Wakizungumzia mfumo wa GPA wamesema mfumo huo ulikuwa unawafanya wanafunzi kuzembea katika masomo yao wakiamini kuwa watafaulu hali ambayo imekuwa kinyume na...

Like
350
0
Friday, 19 February 2016
JAMII IMEOMBWA KUSAIDIA WATU WENYE ULEMAVU KUHAKIKISHA WANAPATA ELIMU
Global News

SERIKALI imeombwa kuisaidia jamii ya watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kuhakikisha wanapata elimu kwani hadi sasa ni asilimia 10 pekee ndiyo wanaopata elimu.   Akizungumza na kituo hiki Katibu wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) amesema kuwa Tanzania ina zaidi ya watu million sita wenye ulemavu mbalimbali hivyo ni vema wakasaidiwa kupata elimu ili kuondokana na tatizo la kuitegemea jamii na serikali kuwasaidia kuyaendesha maisha...

Like
319
0
Friday, 19 February 2016
ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA BOUTROS-GHALI AFARIKI DUNIA
Global News

UMOJA wa Mataifa umetangaza kuwa aliyekuwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Boutros Boutros-Ghali amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 93. Mmisri huyo, aliyekuwa katibu mkuu wa kwanza kutoka Afrika pamoja na Ulimwengu wa Kiarabu, alifariki dunia jana mjini Cairo, kutokana na maradhi yasiyojulikana. Wakati akisifiwa kwa operesheni ya kwanza kubwa ya msaada wa dharura kuwahi kufanywa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwaisaidia waathiriwa wa baa la njaa nchini Somalia, uongozi wake ulikosolewa kutokana na Umoja wa...

Like
323
0
Wednesday, 17 February 2016
OBAMA: TRUMP HATAKUWA RAIS
Global News

RAIS Barack Obama wa Marekani amesema  anaamini mgombea urais wa Chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani. Bwana Trump, Mfanyabiashara tajiri kutoka New York, anaongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea wa chama cha Republican na tayari ameshindakatika Uchaguzi wa mchujo jimbo moja. Akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa Kiuchumi wa nchi za Kusini Mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California, alitoa kauli hiyo baada ya mwandishi wa Habari Mmoja kumuuliza swali lililomhusu...

Like
226
0
Wednesday, 17 February 2016
KENYA KUJENGA JELA YA WAHALIFU WA MAKOSA YA UGAIDI
Global News

RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema Nchi hiyo itajenga jela mpya ya kuwafunga wafungwa wenye makossa ya itikadi kali. Kiongozi huyo amesema hatua hiyo itazuia wafungwa hao kutoeneza itikadi hizo kwa wafungwa wengine. Kwa sasa ni wafungwa waliohukumiwa pekee ambao hutengwa na wafungwa wengine gerezani nchini...

Like
237
0
Wednesday, 17 February 2016
UTURUKI YAENDELEZA MASHAMBULIZI DHIDI YA WAKURDI SYRIA
Global News

UTURUKI imeendelea kuyashambulia maeneo ya Wakurdi nchini Syria kwa siku ya pili, licha ya kuongezeka shinikizo la kimataifa kuitaka nchi hiyo isitishe mashambulizi yake kwenye eneo la mpakani. Uturuki inataka wapiganaji wa Kikurdi waondoke kwenye eneo hilo la mpaka. Akizungumza kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu amesema vikosi vya usalama vya nchi yake havitowaruhusu Wakurdi wafanye vitendo vya uchokozi. Syria imeyalaani mashambulizi ya Uturuki, huku ikiutolea wito Umoja wa Mataifa...

Like
230
0
Monday, 15 February 2016
WANADIPLOMASIA KUANDAA RIPOTI YA USALAMA ISRAEL NA PALESTINA
Global News

WANADIPLOMASIA wa mataifa manne wapatanishi katika amani ya Mashariki ya Kati wamesema wataandaa ripoti kuhusu hali ya sasa ya usalama kati ya Israel na Palestina huku wakiangazia zaidi kuanza tena kwa mazungumzo ya amani. Baada ya kukutana mjini Munich, Marekani, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Urusi, zimesema ripoti hiyo itajumuisha mapendekezo ambayo yanaweza kusaidia kuyajulisha mazungumzo ya kimataifa kuhusu njia bora ya kupatikana kwa suluhisho la mataifa hayo...

Like
202
0
Monday, 15 February 2016
MUSEVENI: NINA IMANI NITASHINDA UCHAGUZI
Global News

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni amesema ana imani atashinda urais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika siku ya Alhamisi wiki hii. Hata hivyo, amesema yuko tayari kukabidhi madaraka kwa mtu mwingine iwapo chama chake kitashindwa. Akijibu maswali ya waandishi wa Habari  wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu jana Jumapili, Bwana Museveni amesema kwa sasa haoni chama chochote ambacho kinaweza kuondoa chama cha National Resistance Movement (NRM)...

Like
419
0
Monday, 15 February 2016
KURA ZAHESABIWA AFRIKA YA KATI
Global News

MAAFISA wa uchaguzi wanaendelea kuhesabu kura baada ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kuandaa jana awamu ya pili iliyocheleweshwa ya uchaguzi wa rais na wabunge, ikiwa na matumaini ya kupatikana amani baada ya kutokea machafuko makubwa ya kidini kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu uhuru mwaka wa 1960. Upigaji kura ulifanywa chini ya ulinzi mkali huku maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwekwa kote nchini humo, lakini uchaguzi huo ulikamilika kwa amani. Matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kutangazwa...

Like
210
0
Monday, 15 February 2016
SYRIA: MATAIFA YAAFIKIANA KUSITISHA MAPIGANO
Global News

MATAIFA yenye ushawishi duniani yameafikiana kuhusu mkataba wa kusitisha mapigano nchini Syria ambao utaanza kutekelezwa katika kipindi cha wiki moja ijayo. Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungumzo nchini Ujerumani. Mwafaka huo hata hivyo hautahusisha makundi ya kijihadi ya Islamic State (IS) na al-Nusra Front. Aidha, Mawaziri wa mataifa wanachama wa Kundi la Kimataifa la Kusaidia Syria pia wamekubaliana kuharakisha na kuongeza juhudi za kutoa...

Like
229
0
Friday, 12 February 2016