Global News

ICC: HATMA YA RUTO KUFAHAMIKA LEO
Global News

MAHAKAMA ya jinai ya kimataifa -ICC leo inatarajiwa kutoa uamuzi ambao huenda ukakuwa na athari kwa kesi inayomkabili naibu rais wa Kenya William Ruto. Bwana Ruto na mushtakiwa mwenzake, mwana Habari, Joshua Arap Sang wameshitakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na ghasia zilizotokea nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa 2007. Mashtaka kama hayo yaliyomkabili rais Uhuru Kenyatta yalifutiliwa mbali na mwendesha mkuu wa mashataka ya ICC, Fatou Bensouda kwa ukosefu wa...

Like
283
0
Friday, 12 February 2016
JENERALI SEJUSA AFIKISHWA MAHAKAMANI
Global News

JENERALI mwenye utata nchini Uganda David Sejusa amewasili katika mahakama moja ya kijeshi katika mji mkuu wa Kampala nchini Uganda tayari kujibu mashitaka yanayomkabili ambayo hata hivyo bado hayajawekwa hadharani. Siku ya jumatatu chombo cha habari cha Bloomberg kilimnukuu msemaji wa serikali Ofwono Opondo akisema kuwa Uganda inachunguza ripoti zinazomuhusisha jenerali mtoro David Sejusa na makundi yenye mipango ya kuzua ghasia. Jenerali Sejusa aliwekwa katika kifungo cha nyumbani siku ya jumapili mjini...

Like
216
0
Tuesday, 02 February 2016
UGANDA YAZINDUA BASI LINALOTUMIA UMEME WA JUA
Global News

UGANDA imefanikiwa kuzindua rasmi basi linalotumia nguvu ya umeme wa jua ambalo limedaiwa kuwa watengezaji wake wanatoka nchini humo na ni la kwanza kama hilo kutengenezwa barani Afrika. Basi hilo la kielektroniki aina ya Kayoola linalomilikiwa na kampuni ya Kiira Motors limeonyeshwa kwa waganda katika uwanja wa Uganda mjini Kampala. Mojawapo ya betri zake zinaweza kuwekwa chaji na vibamba vya umeme wa jua katika paa la nyumba ambazo huongeza kasi ya gari hilo hadi kilomita 80 kwa saa....

Like
243
0
Tuesday, 02 February 2016
AU KUPELEKA UJUMBE MAALUM BURUNDI
Global News

UMOJA wa Afrika umeamua utapeleka ujumbe maalum nchini Burundi kujaribu kuishinikiza serikali ya nchi hiyo kuridhia jeshi la kulinda amani baada ya rais Nkurunzinza kuipinga hatua hiyo.   Taarifa hizo zimetolewa na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Afrika baada ya kumalizika mkutano wa kilele wa Umoja huo hapo jana.   Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka nchi za Magharibi aliyefuatilia mkutano wa jana ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba viongozi wa Umoja wa Afrika waliokutana kwa...

Like
235
0
Monday, 01 February 2016
WHO YAKUTANA KWA DHARURA KUJADILI ZIKA
Global News

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) leo linafanya mkutano wa dharura kujadili kuenea kwa virusi vya Zika. Mkutano huo mjini unaofanyika Geneva utajadili iwapo mlipuko wa virusi hivyo unafaa kutangazwa kuwa dharura ya kimataifa. Katika matukio mengi, watu walioambukizwa virusi hivyo vya Zika huwa hawaonyeshi dalili zozote, lakini virusi hivyo vinadaiwa kusababisha maelfu ya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo Amerika...

Like
261
0
Monday, 01 February 2016
70 WAUAWA KWA MABOMU SYRIA
Global News

WATU zaidi ya  70 wameuawa kutokana na mashambulio  ya mabomu ambayo kundi la magaidi wanaoitwa Dola  la  Kiislamu limedai kuyafanya karibu  na sehemu takatifu ya Washia nje ya mji mkuu wa Syria, Damascus.   Kwa mujibu  wa  taarifa  iliyotolewa  na kituo kilichopo mjini London, kinachofuatilia haki za binadamu nchini  Syria, watu  hao waliuawa kutokana  na miripuko miwili ya mabomu karibu na  sehemu hiyo takatifu, Sayyida Zeinab.   Watoto kadhaa walikuwamo miongoni mwa walioangamizwa huku Watu wengine zaidi ya 100...

Like
394
0
Monday, 01 February 2016
NIGERIA YAOMBA MKOPO WA DHARURA
Global News

NIGERIA imeomba mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu na nusu kutoka Benki ya Dunia ili kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake. Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani. Waziri wa fedha nchini humo Kemi Adeosun amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia. Hata hivyo, hatua ya Nigeria kuomba mkopo wa dharura inashangaza ikizingatiwa kwamba siku chache zilizopita Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema haihitaji usaidizi wa...

Like
290
0
Monday, 01 February 2016
MAKABURI YA WATU WENGI YAGUNDULIKA BURUNDI
Global News

SHIRIKA la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema limeona picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa Burundi kuuawa na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi. Amnesty limesema sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi yapatayo matano katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa Bujumbura. Shirika hilo limeongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku...

Like
217
0
Friday, 29 January 2016
MAOMBI YA RUHUSA YA KUTOA MIMBA KWA WENYE ZIKA YATUMWA BRAZIL
Global News

KUNDI la mawakili, wanaharakati na wanasayansi nchini Brazil limewasilisha ombi kwa mahakama ya juu nchini humo likitaka wanawake wenye virusi vya Zika waruhusiwe kutoa mimba. Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo, na kudumaza ubongo. Utoaji mimba nchini Brazil hauruhusiwi kisheria, ila tu wakati wa dharura ya kiafya au iwapo mimba imetokana na ubakaji hali ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama...

Like
253
0
Friday, 29 January 2016
KENYA: WAWILI WAPANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU MASHTAKA YA MAUAJI
Global News

MAHAKAMA Kuu mjini Mombasa imeamua kwamba washukiwa wawili walioshitakiwa kwa mauaji ya watu 60 eneo la Mpeketoni miaka miwili iliyopita wana kesi ya kujibu. Jaji Martin Muya amesema upande wa mashitaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashitaka wawili hao. Diana Salim Suleiman na Mahadi Suleiman Mahadi ajulikanaye kama Jesus wanadaiwa kuhusika katika uvamizi uliopelekea kuuawa kwa watu 60 mwezi Juni mwaka 2014 katika vijiji vya Mpeketoni na Kaisairi, Kaunti ya Lamu.nchini Kenya....

Like
205
0
Thursday, 28 January 2016
UFISADI: WAZIRI WA UCHUMI JAPAN AJIUZULU
Global News

WAZIRI wa uchumi nchini Japan Akira Amari amejiuzulu kutokana na madai ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili. Bwana Amari ametoa tangazo hilo ghafla katika mkutano na waandishi wa habari jana ambapo mbali na hayo amekanusha kupokea hongo kutoka kwa kampuni moja ya ujenzi kama ilivyodaiwa na jarida moja la Japan. Hatua hiyo imechukuliwa kama pigo kubwa kwa waziri mkuu Shinzo Abe kwani Amari alitarajiwa kusafiri hadi New Zealand wiki ijayo kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya mataifa ya ng’ambo ya pili ya...

Like
233
0
Thursday, 28 January 2016