SHIRIKA la kukabiliana na ufisadi nchini Malaysia limesema kuwa litakata rufaa kuhusu uamuzi wa kuondoa tuhuma za ufisadi dhidi ya waziri mkuuu, Najib Razak. Siku ya jumanne, mkuu wa sheria amesema kuwa uchunguzi haukupata ushahidi kwamba Najib alivunja sheria. Kesi hiyo imeitikisa nchi ya Malaysia na kutishia kumwondoa madarakani ikichangiwa na Uamuzi wa kumuondelea mashtaka hali iliyozua hisia kali kwa...
WAPIGANAJI wa kundi la Al-Shabab wameingia na kudhibiti miji ambayo majeshi ya Kenya yaliondoka jana nchini Somalia. Wakazi wa maeneo ya jirani na miji hiyo wamewaambia waandishi wa habari kwamba wapiganaji wa kundi hilo la Kiislamu wameingia kwenye miji ya Al-Adde, Hosingoh na Badhaadhe. Katika mji wa Hosingoh, mamia ya wapiganaji wanaripotiwa kuingia na kuhutubia wakazi na kisha wakamteua kiongozi wa kusimamia eneo...
Wanaume nchini Elitrea wamepewa amri ya kuoa angalau wake wawili au zaidi kwa kila mwanaume huku adhabu ya kifungo cha maisha jela kutolewa kwa atakaekaidi amri hiyo ya serikali. Kwa mujibu wa serikali agizo hilo limetolewa kufuatia uwepo wa idadi ndogo ya wanaume ikilinganishwa na idadi ya wanawake ikiwa ni matokeo ya vita kati ya taifa hilo na Ethiopia. Serikali nchini humo imewathibitishia raia wake kuwa itagharamia sherehe za harusi na nyumba kwa wanandoa Kwa mujibu wa tovuti ya Afkinsider.com ...
POLISI nchini Senegal wamewakamata watu wapatao mia tisa katika kamata kamata ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na ugaidi. Zoezi hilo limefanyika mwishoni mwa juma lililopita katika mji mkuu wa Dakar karibu na mtaa wa Thies huku Jeshi la ulinzi likitoa angalizo tangu shambulio lililowahi kutokea mapema mwezi huu katika hoteli iliyoko mji mkuu wa Burkina Faso. Hata hivyo wiki iliyopita waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Abdoulaye Daouda Diallo amezitaka hoteli zote nchini humo kuongeza ulinzi ili kuzuia matukio...
WAZIRI mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau amemshutumu katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-Moon kwa kuunga mkono ugaidi, baada ya kusema kuwa ni jambo la kawaida kwa watu wanaotawaliwa au kukandamizwa, kukabiliana na walowezi. Hayo yamejiri kufuatia Zaidi ya Wapalestina 155, Waisraeli 28, Mmarekani na Raia wa Eritrea kuuawa kwa kushambuliwa kwa risasi na visu tangu mwezi Oktoba mwaka jana. Akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Ban amesema visa hivyo vimeongezeka kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza miongoni...
MAHAKAMA ya kikatiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imefuta matokeo yote ya uchaguzi wa ubunge kutokana na kasoro nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi. Mbali na hayo Mahakama hiyo pia imeidhinisha matokeo ya uchaguzi wa urais, ambao ulifanyika katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita. Hata hivyo imethibitisha kwamba mawaziri wakuu wa zamani Anicet- Dologuele na Faustin Touadere watakutana kwenye duru ya pili ya uchaguzi Februari 7 mwaka...
IKIWA ni hatua ya kujumuisha umoja wa kikristo duniani, Kiongozi mkuu wa Kanisa katoliki Ulimwenguni, Papa Francis amewaomba radhi waumini wa Kiprotestanti kutokana na unyanyasaji walioupata kutoka kanisa Katoliki miaka iliyopita. Papa Francis amewataka waumini wa kanisa Katoliki pia kuwasamehe wale ambao waliwakosea ili wasiruhusu makosa yaliyotendeka kuwa sumu ya mahusiano ya sasa. Kufuatia tamko hilo msemaji wa Vatcan ametangaza kuwa Papa Francis atazuru mji wa Lund uliopo Swedish eneo ambalo jumuiya ya Kilutheri ilianzishwa na kuanzisha...
RAIS wa Myanmar anayemaliza muda wake, Thein Sein, ameamuru kuachiwa huru kwa wafungwa 101 wakiwemo takribani 25 waliohukumiwa kwa makosa ya kisiasa. Maafisa nchini humo wamesema msamaha huo unawahusu pia wafungwa 77 waliokuwa wamehukumiwa kifo na adhabu yao kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha. Kwa mujibu wa chama cha wafungwa wa kisiasa nchini humo, miongoni mwa wafungwa 25 wa kisiasa, yumo raia wa New Zealand, Philip Blackwood, ambaye alihukumiwa mwezi Machi kwa kosa la kwenda kinyume na misingi ya...
IMEELEZWA kuwa Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia walionywa kuhusu shambulizi la kundi la Alshabaab siku 45 kabla ya kundi hilo kuvamia mojawapo ya kambi zao. Jenerali Abas Ibrahim Guery ameiambia BBC kuwa , Kenya ilipewa ripoti ya kiintelijensia kuhusu tishio la uvamizi huo ambapo Wapiganaji hao wa kiislamu wanasema kuwa waliwaua zaidi ya wanajeshi 100 katika shambulio hilo likiwa ni baya zaidi kuwahi kufanyika kwa jeshi la Kenya. Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewatambelea baadhi ya wanajeshi waliojeruhiwa katika hospitali...
RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajia kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa baada ya wanamgambo wa Al-Shabab kushambulia kambi ya wanajeshi nchini Somalia Ijumaa iliyopita. Rais Kenyatta atawatembelea majeruhi hao katika hospitali ya Forces Memorial iliyopo Nairobi na baadaye kujumuika na ndugu, marafiki na maafisa wakuu wa Jeshi kwa ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa. Serikali ya Kenya bado haijatoa idadi kamili ya wanajeshi wake waliouawa baada ya kambi hiyo iliyoko El-Ade kushambuliwa ingawa Mkuu wa Majeshi nchini humo Jenerali...
WAZIRI wa Mambo ya Usalama wa Ndani nchini Somalia amesema watu 20 wamefariki baada ya hoteli mbili maarufu za ufukweni kushambuliwa mjini Mogadishu. Waziri Abdirisak Omar Mohamed ameviambia vyombo vya habari kuwa watu wengine 20 wamejeruhiwa baada ya hoteli za Lido Sea Food na Beach View kushambuliwa jana jioni. Hata hivyo tayari Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Al-Shabaab limekiri kuhusika kwenye shambulio hilo ambalo limetajwa kuwa ni miongoni mwa mashambulio ya...