Global News

VATCAN YATHIBITISHA MOTHER TERESA KUWA MTAKATIFU
Global News

MAKAO MAKUU ya Vatican yemedhibitisha kwamba mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na mtawa Marehemu ‘Mother Teresa’ atatangazwa mtakatifu. Taarifa ya Vatican inasema Papa Francis ameridhia utaratibu wa kumtangaza mtakatifu mtawa huyo baada ya kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake....

Like
251
0
Friday, 18 December 2015
AU YATANGAZA KUTUMA WALINDA AMANI BURUNDI
Global News

MUUNGANO wa Afrika umetangaza mpango wa kutuma walinda amani nchini Burundi kuzuia machafuko zaidi nchini humo. Muungano huo umepanga kutuma walinda Amani elfu 5,000 wa kulinda raia.   Umoja wa Mataifa unakadiria watu 400 wameuawa tangu machafuko kuzuka mwezi Aprili  baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.   AU huenda ikalazimika kutuma walinda amani bila kupewa idhini na taifa mwenyeji, muungano huo utatumia kwa mara ya kwanza kifungu kwenye mkataba wake, kinachouruhusu kuingilia kati...

Like
197
0
Friday, 18 December 2015
UN KUKATA MIFUMO YA FEDHA KWA IS
Global News

BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lenye lengo la kukata mifumo ya fedha kwa kundi la Islamic State. Mkutano wa kwanza wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa mawaziri wa fedha umeafiki juu ya azimio hilo lililobuniwa kwa ajili ya kuzuia fedha kuwafikia wanamgambo wa Islamic State. Mkutano huo umeyataka mataifa kufanya juhudi za haraka kukata mifumo ya udhamini wa fedha kwa kundi hilo kwa kuzuia wizi wake wa mafuta na raslimali nyingine.  ...

Like
151
0
Friday, 18 December 2015
EU: YAJADILI UANACHAMA WA UINGEREZA
Global News

VIONGOZI wa muungano wa Ulaya wamesema wako tayari kufikia mapatano ya kuiwezesha Uingereza kusalia katika Muungano huo. Hata hivyo viongozi hao wanaokutana mjini Brassels, wamesisitiza kuwa makubaliano yoyote hayapaswi kuvunja kanuni za muungano wa Ulaya. Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kumekua na mafanikio, lakini akasema bado kuna kazi ngumu inayowasubiri mbele...

Like
181
0
Friday, 18 December 2015
ETHIOPIA YATANGAZA KUYAKABILI MAKUNDI YANAYOHUJUMU AMANI
Global News

WAZIRI MKUU wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amesema serikali yake itakabiliana vikali na makundi yanayohujumu amani baada ya watu kadha kuuawa kwenye maandamano eneo la Oromia. Serikali inasema watu watano wameuawa kwenye makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama lakini makundi ya upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu yanasema idadi ya waliofariki inakaribia 40. Akihutubu kupitia runinga ya taifa ya Ethiopia, Bw Desalegn amesema umma pia una jukumu la kutekeleza katika kukabiliana na makundi hayo.  ...

Like
197
0
Thursday, 17 December 2015
MKUTANO WA UN KUIJADILI BURUNDI WAENDELEA GENEVA
Global News

MKUTANO maalum wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaendelea mjini Geneva kujadili hali nchini Burundi.   Kabla ya mkutano huo kufanyika mjini Geneva, Uswizi, Katibu Mkuu wa umoja UN Ban Ki-moon alikuwa ameonya kuwa taifa hilo limo hatarini ya kutumbukia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yanaweza kuathiri kanda yote.   Amesema machafuko yaliyotokea nchini Burundi siku za hivi majuzi yanatisha  na kwamba atamtuma mshauri wake maalum kwenda Burundi kwa mashauriano ya dharura na serikali....

Like
185
0
Thursday, 17 December 2015
KIMBUNGA CHAUKUMBA MJI WA SYDNEY AUSTRALIA
Global News

KIMBUNGA  kilichokuwa  na  kasi  ya  kilometa 200  kwa  saa kimeukumba  mji wa  Sydney  nchini  Australia  leo , na kuezuwa  mapaa  ya  nyumba  katika  kitongoji  cha  kusini ya  pwani  ya  mji  huo na  kusababisha  mafuriko  na mvua  ya  mawe.   Kimbunga  hicho , kilichokuwa  na  upepo mkali  kuwahi kuonekana  katika  mji  wa  Sydney , kilikuwa  sehemu  ya kimbunga  kikubwa  kilicholikumba  eneo  la  pwani  ya kusini  ya  New South Wales  na  Sydney  kabla  ya kuelekea  upande  wa ...

Like
274
0
Wednesday, 16 December 2015
MHUBIRI WA CANADA APIGWA KIFUNGO CHA MAISHA KOREA KASKAZINI
Global News

MAHAKAMA ya juu zaidi Korea Kaskazini imemhukumu mhubiri kutoka Canada kifungo cha maisha jela na kazi ngumu. Hyeon Soo Lim, mwenye umri wa maika 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru taifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.” Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la...

Like
274
0
Wednesday, 16 December 2015
DONALD TRUMP AKOSOLEWA VIKALI
Global News

WAGOMBEA wa Republican wanaowania nafasi ya urais nchini Marekani wamejibizana kuhusu njia bora zaidi za kudumisha usalama wa taifa na kukabiliana na Islamic State (IS) kwenye mdahalo wa kwanza tangu kutokea kwa mashambulio ya California na Paris. Mgawanyiko mkubwa umetokea kati ya wale wanaotetea kuwepo kwa upeelezi zaidi na wale wanaotetea haki za kiraia. Mgombea anayeongoza, Donald Trump, amelazimika kujitetea kutokana na pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani, huku Mgombea mmoja anayempinga vikali, Jeb Bush, akimwita Trump...

Like
178
0
Wednesday, 16 December 2015
MIILI YA WATU 19 YAPATIKANA MEXICO
Global News

MIILI ya watu wapatao 19 imepatikana katika jimbo la mexico la Guerrero, ambako wanafunzi 43 walitoweka mwaka jana. Polisi wanasema miili hiyo ilitupwa kwenye mto mwembamba, wenye kina cha mita mia tano katikati ya miamba na miti karibu na kijiji cha Chichi-hua-lco. Miili nane kati ya hiyo ilikuwa inaonekana kuchomwa baadhi ya viungo....

Like
169
0
Wednesday, 16 December 2015
MATAIFA 34 YA KIISLAM KUUNGANA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UGAIDI
Global News

SAUDI ARABIA imetangaza kuunda muungano mpya wa kijeshi wa nchi 34 za kiislamu kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya ugaidi. Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia limesema kazi ya muungano huo itaratibiwa katika kituo cha pamoja mjini Riyadh. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, waziri wa ulinzi wa Saudia, Mwanamfalme Mohammed bin Salman, amesema kuwa muungano huo utaratibu juhudi za mapigano dhidi ya makundi yenye itikadi kali katika mataifa ya Syria, Iraq, Libya, Misri na...

Like
148
0
Tuesday, 15 December 2015