Global News

BAN KIN MOON AZITAKA NCHI ZENYE NGUVU KUTIMIZA AHADI ZAO
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani lazima zitimize ahadi zao za kuchangisha kiasi cha dola bilioni 100 kufadhili juhudi za kulinda mazingira ifikapo mwaka 2020. Ban Ki-moon amewaambia wanahabari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa nchi zinazostawi zinataka msimamo thabiti kuhusu ufadhili huo uliokubalika katika mkutano wa kilele wa mazingira mjini Copenhagen, Denmark mwaka 2009. Nchi maskini zinatafuta mabilioni ya fedha ili kuepusha athari za kutolewa kwa gesi chafu...

Like
170
0
Friday, 04 December 2015
MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE URUSI NA UTURUKI WAKUTANA BELGRADE
Global News

MAWAZIRI wa mambo ya nje wa Uturuki na Urusi wamekutana mjini Belgrade, katika mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kati ya viongozi wa nchi hizo mbili tangu kudunguliwa kwa ndege ya Urusi na Uturuki wiki iliyopita. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alikutana na mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglu pembezoni mwa mkutano wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE. Lavrov amesema alikutana na Cavusloglu baada ya kumuomba mara kadhaa kukutana naye lakini hakuna jipya...

Like
127
0
Friday, 04 December 2015
UINGEREZA YATHIBITISHA KUHUSIKA NA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS
Global News

WIZARA ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa ndege za kijeshi za Uingereza zimetekeleza mashambulio ya angani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria saa chache baada ya bunge kuidhinisha mashambulio hayo, Duru za serikali zimesema ndege hizo tayari zimerejea kambini katika visiwa vya Cyprus. Awali, wabunge nchini Uingereza walikuwa wamepiga kura kwa wingi kuunga mkono mashambulio hayo, wabunge 397 wakiunga mkono dhidi ya 223, baada ya mjadala mkali uliodumu saa 10 katika bunge la...

Like
144
0
Thursday, 03 December 2015
WASHUKIWA WA MAUAJI WAUAWA MAREKANI
Global News

POLISI katika jimbo la California wametaja majina ya washukiwa wawili ambao wameuawa na polisi baada ya watu 14 kuuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa San Bernardino.   Mwanamume Syed Rizwan Farook, mwenye umri wa miaka  28, na mwanamke Tashfeen Malik, mwenye umri wa miaka 27, wameuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi na polisi.   Mkuu wa polisi wa San Bernardino Jarrod Burguan amesema kuwa Farook alikuwa ameajiriwa na baraza la mji kwa miaka mitano. Mmoja ya ndugu wa wafiwa...

Like
171
0
Thursday, 03 December 2015
UGAIDI: RAIA WA UINGEREZA AHUKUMIWA KENYA
Global News

MTU mmoja raia wa Uingereza, anayetuhumiwa kupanga mashambulio ya kigaidi, amefungwa jela miaka tisa na mahakama mjini Mombasa nchini Kenya. Jermaine Grant Mwingereza aliyekamatwa mwaka 2011, amefungwa jela kwa makosa tisa yanayohusiana na kujaribu kujipatia uraia wa Kenya kwa njia haramu. Bado anakabiliwa na mashtaka ya “kupanga kuunda vilipuzi” kwenye kesi ambayo bado inaendelea mjini Mombasa lakini Grant amekanusha mashtaka hayo....

Like
145
0
Wednesday, 02 December 2015
IDADI YA WAKIMBIZI WANAOINGIA ULAYA YAPUNGUA
Global News

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa idadi ya wakimbizi wanaoingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterenia imepungua kwa mara ya kwanza mwezi wa Novemba ikilinganishwa na mwezi mmoja kabla.   Inakadiriwa kuwa wakimbizi laki moja na elfu 40 wameingia Ulaya mwezi uliopita wakipitia baharini.   Habari hizo zimetangazwa na shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia wakimbizi UNHCR mjini geneva jana....

Like
202
0
Wednesday, 02 December 2015
WAFANYABIASHARA WAKUBWA WAINGIA KWENYE ORODHA YA WATU MAFISADI ZAIDI
Global News

WAFANYIBIASHARA wakubwa wametajwa kuwa ni miongoni mwa watu mafisadi zaidi sawa na maafisa wa polisi Barani Afrika.   Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa na shirika la kuchunguza ufisadi duniani “Transparency International”.   Ni mara ya kwanza kwa wafanyabiashara kutajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani na Shirika hilo limeongeza kwamba matumizi mabaya ya mamlaka yanasababisha ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji...

Like
280
0
Wednesday, 02 December 2015
VIONGOZI WAMETAKIWA KUTIMIZA AHADI ZAO KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
Global News

RAIS wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa ahadi zinazotolewa na viongozi zinahitaji kutekelezwa ili kuuokoa ulimwengu kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Hollande ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa viongozi wa dunia mjini Paris kwa lengo la kujadili juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Katika mkutano huo Viongozi hao wameahidi kupunguza uzalishaji wa hewa chafu ya mkaa inayosababisha viwango hivyo vya joto...

Like
186
0
Tuesday, 01 December 2015
BURKINA FASO YAPATA RAIS MPYA
Global News

ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Burkina Faso ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu wa Zamani wa nchi hiyo Uroch Christian Kabore ameshinda kwa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku chache zilizopita. Waziri Mkuu huyo wa zamani amepata alisimia 53.5 katika Uchaguzi huo unaoaminika kuwa ni wa kwanza tangu maandamano yaliyomuondoa madarakani Rais wa miaka mingi Blaise Compaore. Uchaguzi Mkuu ulitarajiwa kufanyika mwezi uliopita lakini ukacheleweshwa na jaribio la mapinduzi ambalo halikufaulu mwezi Septemba mwaka...

Like
166
0
Tuesday, 01 December 2015
UFARANSA YAELEZA MSIMAMO WAKE SYRIA
Global News

WAZIRI wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema kufanya kazi na jeshi la Syria sio jambo wanalolizingatia hadi Rais wa Syria Bashar Al Assad atakapoondolewa madarakani. Fabius amesema ni dhahiri kuwa Rais Assad hawezi kufanya kazi na waasi wenye misimamo ya wastani nchini Syria na kwamba iwapo hataliongoza jeshi la Syria, huenda kukawa na ushirikiano baina yao wa kupambana dhidi ya ugaidi. Ufaransa inataka Assad aondolewe madarakani ikimtaja kuwa ni kiongozi  anaye wauwa watu wake...

Like
207
0
Tuesday, 01 December 2015
KENYA: SHAMBULIO BANDIA LALETA MAAFA
Global News

MWANAMKE mmoja amefariki huku zaidi ya wanafunzi 20 wakijeruhiwa katika oparesheni ya kuiga shambulio la kigaidi ilioendeshwa nchni kenya, katika chuo kikuu cha Strathmore. Oparesheni hiyo imepangwa na chuo hicho pamoja na maafisa wa polisi bila kuwaarifu wanafunzi na wafanyakazi, ili kubaini ikiwa chuo hicho kiko tayari kukabiliana na tukio la kigaidi. Kauli rasmi kutoka chuo kikuu cha strathmore, imethibitisha kwamba mfanyakazi mmoja amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuruka kutoka ghorofa ya...

Like
181
0
Tuesday, 01 December 2015