Global News

SUDANI KUSINI: BASI LAVAMIWA
Global News

BASI moja lililokuwa likisafiri kutoka mjini Juba kuelekea kampala nchini Uganda limevamiwa na kufyatuliwa risasi leo majira ya saa moja asubuhi. Maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini wameeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Moli takribani kilomita 50 kutoka mji wa mpakani wa Nimule na kwamba kwa sasa bado wanaendelea kutafuta idadi kamili ya watu waliojeruhiwa. Hata hivyo maafisa hao wamebainisha kwamba wanafanya jitihada za kukutana na kujadiliana na wenzao wa Uganda ili kubaini chanzo cha tukio...

Like
217
0
Thursday, 19 November 2015
SALVA KIIR ASISITIZA KUENDELEZA MAKUBALIANO YA AMANI
Global News

RAIS  wa  Sudan  kusini  Salva  Kiir  amesisitiza  nia yake ya kuendeleza makubaliano  ya  Amani  yaliyotiwa  saini mwezi  Agosti, siku  mbili  baada  ya  serikali  na  waasi kushutumiana  kwa  kukiuka  makubaliano  hayo. Rais Kiir  ameliambia bunge  la nchi hiyo kwamba Sudan  kusini inapaswa  kufikia   maridhiano na  kufungua  kurasa mpya  na  kuitaka  jumuiya  ya  kimataifa  kusaidia nchi hiyo  kutekeleza  makubaliano  ya  amani. Mvutano  wa  kuwania  madaraka  kati  ya  rais Salva Kiir na ...

Like
243
0
Thursday, 19 November 2015
IS YATHIBITISHA KUUA MATEKA WAWILI
Global News

WAPIGANAJI wa Islamic State (IS) wamethibitisha kuwaua mateka wawili, ambao ni raia wa Norway na raia wa China. Waziri mkuu wa Norway Erna Solberg amesema hakuna sababu zozote za kutilia shaka tangazo la wapiganaji hao na kutaja kitendo chao kuwa ni “unyama”. Naye Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Hong Lei amesema kwamba tangu raia huyo nchi yake akamatwe, Taifa hilo limefanya jitihada za kumuokoa bila...

Like
229
0
Thursday, 19 November 2015
OBAMA AWASHUTUMU WAPINZANI WAKE
Global News

RAIS Barack Obama  wa  Marekani ameshambulia kile alichokieleza  kuwa ni hofu ya kupita kiasi juu ya kitisho cha usalama kinachosababishwa  na  wakimbizi kutoka  Syria. Katika hatua isiyokuwa ya kawaida Rais Obama amewashutumu  wapinzani  wake  kisiasa, kwa kuwaweka wajane  na  yatima  katika  kundi  la  wahalifu. Hata hivyo Kupatikana kwa  hati  ya  kusafiria ya  Syria  karibu  na mwili wa mshambuliaji katika mashambulizi ya mjini Paris  kumezusha  hofu miongoni mwa wabunge wa Marekani na  magavana  kwamba ...

Like
209
0
Wednesday, 18 November 2015
NIGERIA: BUHARI AAGIZA KUKAMATWA KWA AFISA ANAETUHUMIWA KWA WIZI
Global News

RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameagiza kukamatwa kwa Afisa mmoja mkuu serikalini kwa tuhuma za kuiba zaidi ya dola bilioni 2 zilizotengwa kwaajili ya vita dhidi ya kundi la Boko Haram. Kanali Sambo Dasuki ambaye alikuwa mshauri wa kitaifa kuhusu masuala ya usalama kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan, ameshtakiwa kwa kutoa kandarasi bandia za kununua helikopta 12, ndege 4 za kijeshi na silaha mbalimbali. Msemaji wa rais Buhari amesema kwamba ufisadi huo ulisababisha vifo vya maelfu ya...

Like
248
0
Wednesday, 18 November 2015
AMNESTY INTERNATIONAL: NCHI ZA ULAYA ZINAKIUKA HAKI ZA BINADAM MIPAKANI
Global News

SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International, limesema uzio wa mipakani na udhibiti mwingine unaofanywa na mataifa ya Umoja wa Ulaya vinachochea ukiukwaji wa haki za binaadamu. Mkurugenzi wa shirika hilo barani Ulaya na Asia ya Kati John Dalhuisen, amesema kutanua uzio katika mipaka ya Ulaya kumechochea changamoto za kudhibiti wimbi la wakimbizi kwa njia za kistaarabu, na utaratibu mzuri. Ripoti hiyo imeangalia athari zinazosababishwa na uzio mpya, hasa katika mpaka wa Hungary na Serbia na wajibu...

Like
245
0
Wednesday, 18 November 2015
MAPAMBANO YA RISASI YATAWALA KASKAZINI MWA MJI WA PARIS
Global News

LIMETOKEA tukio la ufyatulianaji mkali wa risasi kaskazini mwa Paris katika mtaa wa Saint Denis huku ripoti zikisema kuwa operesheni ya polisi kuhusiana na mashambulio ya Ijumaa inaendelea. Shirika la habari la AFP limeeleza kuwa Abaaoud Abdelhamid, anayedaiwa kupanga mashambulio hayo, ndiye aliyekuwa akisakwa kwenye operesheni hiyo mtaa wa Saint Denis. Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia tukio hilo wakisema kuwa milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri kwa saa za...

Like
232
0
Wednesday, 18 November 2015
UFARANSA: POLISI WAENDELEZA MSAKO WA MAGAIDI
Global News

POLISI nchini Ufaransa wameendelea na msako dhidi ya kundi la wajihadi wanaoshukiwa kusababisha mauaji yaliyotokea mjini Paris Ijumaa ya wiki iliyopita. Tayari Polisi hao wameshavamia makao zaidi ya100 huku wakiwaweka washukiwa katika kifungo cha nyumbani wakiongozwa na mshukiwa mkuu Salah Abdeslam, mwenye umri wa miaka 26. Wakati hayo yakijiri, ndege za kivita za Ufaransa zimetekeleza mashambulio mapya na makali zaidi dhidi ya ngome ya Islamic State nchini...

Like
224
0
Tuesday, 17 November 2015
NDEGE ILIYOANGUKA MISRI ILILIPULIWA
Global News

NCHI ya Urusi imethibitisha kuwa ajali ya ndege ya Metrojet iliyoanguka na kuua watu zaidi ya 200 katika rasi ya Sinai nchini Misri mwezi uliopita iliangushwa na shambulio la kigaidi. Mkuu wa idara ya usalama wa Taifa Alexander Bortnikov amemueleza rais wa nchi hiyo Vladimir Putin kuwa ndege hiyo iliangushwa na bomu lenye uzani wa kilo moja. Bortnikov alipokamilisha maelezo yake kwa rais Putin, rais huyo pamoja na mawaziri wengine wakuu wamesimama na kunyamaza kimya kwa muda kabla ya rais Putin...

Like
207
0
Tuesday, 17 November 2015
ANDY MURRAY AANZA VYEMA MICHUANO YA TENNIS
Global News

Muingereza Andy Murray anayeshika nafasi ya pili kwa ubora duniani ameanza vema michuano ya dunia ya tenesi kwa ushindi. Murray alimshinda mpinzani wake David Ferrer, wa Hispania, ambae anashikia nafasi ya saba kwa ubora wa mchezo wa tenesi kwa jumla ya seti 6-4 6-4. Nae Rafael Nadal, akamchapa Stan Wawrinka kwa jumla ya seti 6-3 na 6-2, hivyo Nadal kulipa kisasi cha kufungwa na Wawrinka katika michuano ya Paris Masters, mchezo huu ulitumia muda wa saa moja na dakika 23....

Like
212
0
Tuesday, 17 November 2015
UFARANSA YATANGAZA VITA DHIDI IS
Global News

RAIS Francoise Hollande wa Ufaransa ametangaza kwamba nchi yake ipo kwenye vita dhidi ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu( IS).   Akihutubia mabaraza mawili ya bunge jana, Rais Hollande ameapa kuwa nchi yake ipo tayari kuliangamiza kundi hilo linaloendelea kuleta madhara makubwa katika nchi mbalimbali.   Kiongozi huyo amesema ili kuhakikisha hilo linafanikiwa atahakikisha vikosi vya ulinzi vinaimarishwa na kutaundwa muungano wa kimataifa kwaajili ya kudhibiti mipaka....

Like
200
0
Tuesday, 17 November 2015