Global News

MKUTANO WA PILI WA AMANI NA USALAMA AFRIKA KUFANYIKA DAKAR
Global News

MKUTANO wa Awamu ya pili wa Amani na usalama barani Afrika unatarajia kufanyika mjini Dakar nchini Senegal kwa muda wa siku mbili zijazo. Mkutano huo utawasaidia viongozi wa nchi, mawaziri na wataalamu wa jeshi kuangalia njia bora za kuimarisha usalama na utulivu barani Afrika. Aidha Mkutano huo wa kimataifa wa awamu ya pili unalenga zaidi changamoto za bara la Afrika na athari zake katika ngazi za...

Like
301
0
Monday, 09 November 2015
UPINZANI WAELEKEA KUSHINDA UCHAGUZI CROATIA
Global News

CHAMA cha upinzani nchini Croatia kinaelekea kupata ushindi kwenye uchaguzi wa ubunge uliofanyika Jumapili ya wiki iliyopita ingawa bado hakijapata viti vya kutosha kuunda serikali. Matokeo ya awali yanaonyesha chama hicho cha -HDZ-kitapata viti 60, huku muungano unaotawala wa Social Democrats wa waziri mkuu anayeondoka Zoran Milanovic ukipata viti 50. Hata hivyo Chama hicho cha wahafidhina sasa kinatarajiwa kuanza mazungumzo ya kuunda...

Like
263
0
Monday, 09 November 2015
LIBYA: MAKUNDI HASIMU  YAMETAKIWA KUTOKWAMISHA MIPANGO YA KUGAWANA MADARAKA
Global News

MJUMBE  wa  Umoja  wa  Mataifa  nchini  Libya  ambaye anaondoka  ameyataka  makundi  hasimu  nchini  humo  kusitisha  juhudi  zao  za  kuzuwia  mpango  wa kugawana  madaraka unaolenga  katika  kumaliza  mzozo wa  kisiasa  nchini  mwao. Bernardino  Leon, ambaye  nafasi  yake  inatarajiwa kuchukuliwa  hivi  karibuni  na  mwanadiplomasia  wa  siku nyingi  wa  Ujerumani,  Martin Kobler, pia  amejitetea  dhidi ya  maelezo  kwamba  kuna  mvutano  wa  kimaslahi kwake  kukubali  kazi  katika  Umoja ...

Like
327
0
Friday, 06 November 2015
MISRI YAZUIA NDEGE ZA SHIRIKA LA UINGEREZA
Global News

SERIKALI ya Misri imesimamisha safari za shirika la ndege la Easyjet ambalo lilikuwa limepangiwa kuwasafirisha baadhi ya Waingereza waliokwama mji wa Sharm el-Sheikh leo.   Ndege za shirika la Easyjet pamoja na ndege za mashirika ya Monarch, Thomson na British Airways ndizo zilizokuwa zimepangiwa kuwasafirisha Waingereza waliokuwa Sharm el-Sheikh baada ya Uingereza kusitisha safari za ndege za kuingia na kutoka katika mji huo.   Hatua hii imekuja  baada ya kuibuka kwa uwezekano kwamba huenda ndege ya Urusi iliyoanguka baada ya...

Like
233
0
Friday, 06 November 2015
MAPIGANO YAONGEZEKA BUJUMBURA
Global News

WATU zaidi wameendelea kutoroka katika  mji wa Bujumbura nchini Burundi baada ya kuongezeka kwa mapigano. Jumatano, watu wanne waliuawa katika mitaa miwili ya mji huo mkuu na  Maafisa wa serikali wanasema watu hao waliuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi kati ya makundi ya watu wenye silaha na maafisa wa polisi usiku. Mauaji yamekuwa yakitokea nchini Burundi tangu Aprili baada ya kuanza kwa maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa...

Like
319
0
Friday, 06 November 2015
AFRIKA YA KUSINI YAPEWA SIKU 60 KUIONDOLEA VIKWAZO MAREKANI
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama ameipa Afrika ya Kusini siku 60 kuondoa vikwazo katika bidhaa za kilimo kutoka Marekani la sivyo ataiondolea msamaha wa kodi wa bidhaa. Mpango huo utaathiri karibu robo ya billion ya dollar ya bidhaa za Afrika kusini zinazosafirishwa nchini Marekani. Afrika Kusini ilipiga marufuku kuagiza mazao ya kuku mwezi Decemba kutokana na kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa mafua ya ndege na kwa miaka kadhaa imekuwa ikitoa adhabu ya kodi kwa baadhi ya bidhaa za kuku...

Like
321
0
Friday, 06 November 2015
WANAFUNZI WAFANYA MAANDAMANO KUPINGA MKUTANO WA CHINA NA TAIWAN
Global News

MAELFU ya wakazi na wanafunzi wameandamana leo nje ya jengo la Bunge la Taiwan, kutokana na kughadhibishwa na mkutano wa kihistoria ulipangwa kufanywa na viongozi wa Taiwan na China.   Rais wa Taiwan  Ma Ying-jeou anatarajiwa kukutana na rais wa China  Xi Jinping  Jumamosi mjini Singapore.   Mashirika ya habari ya umma yameripoti kwamba, mkutano huo utakuwa wa kwanza kwa viongozi wa China na Taiwan kukutana katika kipindi cha miongo...

Like
293
0
Wednesday, 04 November 2015
NDEGE YA MIZIGO YAANGUKA SUDANI KUSINI
Global News

NDEGE ya  mizigo imeanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika uwanja wa ndege nchini Sudan Kusini na kusababisha vifo vya watu takriban  41 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pamoja na waliokuwa maeneo iliko tokea ajali hiyo.   Msemaji wa ofisi ya rais Ateny Wek Ateny amesema muhudumu mmoja na mtoto wamenusurika katika ajali hiyo.   Mwandishi wa shirika la habari wa AP aliyekuwa karibu na eneo la tukio amesema alishuhudia mabaki ya ndege hiyo yalionekana yametawanyika upande wa mashariki...

Like
307
0
Wednesday, 04 November 2015
MSF YATAKA UCHUNGUZI HURU DHIDI YA MASHAMBULIZI YA NDEGE ZA MAREKANI
Global News

SHIRIKA la madaktari wasio na mipaka-MSF, limerudia kutoa ombi la kufanyika uchunguzi huru, mwezi mmoja baada ya hospitali yake nchini Afghanistan kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani.   Shirika hilo lenye makao yake mjini Paris, jana limefanya mkutano wake mjini New York na kutumia dakika moja kukaa kimya kuwakumbuka watu 30 waliouawa katika shambulizi hilo la anga, lililofanyika kwenye hospitali ya watu walioathirika na vita mjini Kunduz.   Mkurugenzi Mtendaji wa MSF Marekani, Jason Cone, amesema wamekuwa wakifanya kazi...

Like
193
0
Wednesday, 04 November 2015
MARAIS CHINA NA TAIWAN KUFANYA MKUTANO WA KIHISTORIA
Global News

RAIS wa China Xi Jinping anatarajiwa kukutana na Rais wa Taiwan, Ma Ying-Jeou siku ya Jumamosi.   Shirika la habari la China, Xinhua limesema kuwa mkutano huo utakaofanyika Singapore, utakuwa wa kwanza tangu viongozi wa nchi hizo mbili walipokutana mwaka 1949, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.   Awali serikali ya Taiwan ilitangaza kuhusu mkutano huo, ikisema viongozi hao wawili watajadiliana kuhusu masuala muhimu ikiwemo kuimarisha amani kwenye eneo la Taiwan na kwamba utafungua njia mpya ya...

Like
209
0
Wednesday, 04 November 2015
BOKO HARAM LAZINDUA KIWANDA CHA MABOMU
Global News

KUNDI la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram limezindua kiwanda wanachotumia kuunda mabomu na silaha zingine kali Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Wachunguzi wamesema kuwa picha zilizopigwa wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama. Haijabainika iwapo mashine hizo za chuo hicho zilinaswa na maafisa wa jeshi la Nigeria licha ya waasi hao kupigwa na kuondolewa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa...

Like
315
0
Tuesday, 03 November 2015