Global News

WABUNGE KUKUTANA KENYA KUJADILI UHABA WA FEDHA
Global News

WABUNGE nchini Kenya wanakutana katika kikao cha dharura ili kujadili ni kwa nini serikali haina fedha. Malipo muhimu hayajafanywa na hivyo kuathiri wizara nyingi na huduma kwa umma pamoja na bunge lenyewe ambalo umeme umekatwa kwa siku kadhaa. Hatua hiyo imesababisha huduma za maji na usafi kuzorota na wabunge wanasema kuwa hali hiyo...

Like
222
0
Thursday, 08 October 2015
SYRIA: NATO KUJADILI KUIMARISHA ULINZI
Global News

MAWAZIRI wa ulinzi wa  Jumuiya ya kujihami ya Nato leo wanajiandaa kujadili iwapo waimarishe ulinzi wa kanda ya kusini ya  ushirika huo wa kijeshi, kutokana na wasiwasi nchini Syria, baada ya  kujiingiza kwa Urusi  katika mgogoro huo hivi karibuni. Kabla ya mkutano huo mjini Brussels, Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema makanda wa kijeshi wamethibitisha kwamba jumuiya hiyo inauwezo na miundo mbinu inayohitajika kuliweka jeshi lake upande wa kusini na kubakia eneo...

Like
187
0
Thursday, 08 October 2015
URUSI YAFANYA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS
Global News

MELI  nne  za  kijeshi  za  Urusi  zimeshambulia maeneo ya  kundi  la  Dola  la  Kiislamu  nchini  Syria  kwa makombora, hii ikiwa ni moja kati ya kampeni zake  za  kijeshi kulishambulia kundi hilo. Rais Vladimir Putin  ameelezwa  na  waziri  wake wa  ulinzi Sergei Shoigu kwamba  pamoja  na ndege  za  kijeshi, meli nne za  kijeshi  kutoka  eneo  la  bahari ya  Caspian zimeshiriki  katika  hujuma  hiyo na kuongeza  kwamba  meli hizo  za  kijeshi  zimefanya  mashambulizi 26  ya makombora  dhidi  ya ...

Like
299
0
Thursday, 08 October 2015
RAIS DILMA WA BRAZIL MATATANI
Global News

MAHAKAMA nchini Brazil imebaini kuwa Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff amekiuka sheria za usimamizi wa akaunti ya bajeti ya mwaka jana. Serikali ya nchi hiyo ilishitakiwa kwa tuhuma za kuazima fedha kinyume cha sheria benki kuu kwa lengo la kuziba upungufu wa bajeti serikalini. Hata hivyo Kambi ya upinzani nchini Brazil imesema kuwa hatua hiyo ya mahakama inawasafishia njia ya kuanza kuchukua hatua za kisheria kumuondoa madarakani Rais...

Like
221
0
Thursday, 08 October 2015
UFISADI: MAJAJI 7 WASIMAMISHWA KAZI GHANA
Global News

JUMLA ya Majaji saba kati ya 12 wa mahakama ya juu nchini Ghana wamesimamishwa kazi kwa muda kufuatia madai ya kuhusika katika ufisadi. Mwezi uliopita majaji wengine 22 wa ngazi za chini walisimamishwa kazi baada ya filamu moja kuwaonesha wakipokea rushwa kutoka kwa wateja ili wapate kupendelewa katika kesi zilizowakabili. Hata hivyo Majaji wengine kadhaa wamekana kuhusika na madai hayo hali iliyowapeleka mahakamani kupinga kitendo cha wao kusimamishwa...

Like
293
0
Tuesday, 06 October 2015
WAZIRI MKUU YEMEN ANUSURIKA KIFO
Global News

WAZIRI mkuu nchini Yemeni Khaled Bahah amenusurika kifo baada ya hoteli aliokuwa akiishi pamoja na baraza lake la mawaziri kushambuliwa mjini Aden. Milipuko kadhaa imeikumba hoteli ya Qasr siku ya jumanne asubuhi pamoja na makao makuu ya vikosi vya milki za kiarabu vinavyoiunga mkono serikali. Msemaji wa serikali nchini Yemen, Rajeh Badi amekiambia chombo cha habari cha AFP kwamba roketi zilirushwa katika maeneo matatu kutoka nje ya mji huo ikiwemo eneo walilokuwepo. Hoteli ya Qasr ilioshambuliwa nyumba...

Like
248
0
Tuesday, 06 October 2015
WATU ZAIDI YA 60 WAUAWA KWA BOMU IRAQ
Global News

ZAIDI ya watu 60 wamefariki kufuatia kulipuka kwa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari katika jimbo la mashariki la Diyala nchini Iraq. Shambulio lingine la bomu limetokea katika mji wa kusini mwa Barsa ambao kwa kipindi kirefu haujakumbwa na mashambulizi ya mabomu huku maafisa usalama nchini humo wakisema bomu hilo lililotegwa katika mtaa wa Zubair limeua watu kumi. Hata hivyo kundi la kiislamu la –IS- limethibitisha kuhusika katika mashambulizi...

Like
190
0
Tuesday, 06 October 2015
SERIKALI YA KENYA YATOA SHUKRANI KWA RAIS KIKWETE
Global News

SERIKALI ya Kenya imemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dokta Jakaya mrisho Kikwete kwa kudumisha na kuboresha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. Taarifa iliyotolewa  Ikulu Jijini Dar es salaam inaeleza kuwa shukrani za Kenya zimetolewa na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta katika mazungumzo aliyoyafanya na Rais Kikwete nchini humo. Rais Kikwete yuko nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu ambapo leo anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya...

Like
167
0
Tuesday, 06 October 2015
WALIMU KENYA WATII AGIZO LA MAHAKAMA
Global News

  IKIWA leo ni Siku ya Walimu Duniani, Shule nchini Kenya zimefunguliwa tena baada ya walimu kusitisha mgomo wao uliokuwa umedumu kwa wiki tano. Vyama viwili vinavyotetea walimu nchini humo vilitangaza mwishoni mwa wiki kwamba zitatii agizo la mahakama la kuwataka walimu warudi shuleni. Walimu takriban 280,000 walikuwa wamegoma kuishinikiza serikali iwalipe nyongeza ya mishahara ya asilimia 50 hadi...

Like
230
0
Monday, 05 October 2015
WAZIRI WA ARDHI AELEZA UMUHIMU WA KUPANGA MAENEO YA MAKAZI
Global News

NAIBU waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa ANGELLAH KAIRUKI amesema kuwa ni lazima kuweka umuhimu mkubwa katika kupanga, kutenga, kupima, kuendeleza na kusimamia maeneo ya Umma kwa kuzingatia sheria na mahitaji maalum na salama kwa watumiaji wakiwemo wanawake, watoto, wazee na watu wenye ulemavu. Mheshimiwa Kairuki ameiambia EFM leo kwenye maadhimisho ya siku ya makazi duniani yaliyoadhimishwa Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa ili kuhakikisha uwepo wa utumiaji salama wa maeneo ya umma hususani sehemu za ardhi...

Like
285
0
Monday, 05 October 2015
MACHAFUKO 15 WAUAWA BURUNDI
Global News

WATU wapatao 15 wameuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji na polisi kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura. Kiongozi wa Baraza la Haki za Binaadamu la nchi hiyo, Anschaire Nikoyagize, ameliambia shirika la habari la Ujerumani, DPA, kwamba kulikuwa na milio ya risasi kwenye mitaa ya Mutakure na Cibitoke, na hadi wakati huo walishapata maiti 15, ingawa idadi ilitazamiwa kuongezeka. Ghasia zimelikumba taifa hilo dogo la Afrika Mashariki, tangu Rais Pierre Nkurunziza kutangaza azma yake ya kuwania muhula wa tatu madarakani...

Like
218
0
Monday, 05 October 2015