Global News

Wanajeshi Gabon wajaribu kupindua serikali ya Ali Bongo ambaye yuko Morocco
Global News

Kundi la wanajeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu Libreville. Shirika la habari la AFP inasema milio ya risasi imesikika jijini humo. Amri ya kutotoka nje imetangazwa. Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo linatangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali...

Like
775
0
Monday, 07 January 2019
Kuna ‘mshindi wa wazi’ uchaguzi wa urais DRC
Global News

Kanisa Katoliki, ambalo lina ushawishi mkubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limesema kuna mshindi wazi wa urais katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, kwa mujibu wa matokeo ambao wamefanikiwa kuyaona. Maaskofu wa kanisa hilo wamewataka watawala nchini humo kuwa wakweli na kutangaza matokeo hayo karibuni. Kanisa hilo lina maelfu ya wangalizi wa uchaguzi nchini humo na baadhi wamewasilisha ripoti za dosari kadha wa kadha. Tume ya uchaguzi ilitarajiwa kutangaza matokeo Jumapili lakini wiki hii ilidokeza kuwa huenda ikachelewa kufanya...

1
1401
0
Friday, 04 January 2019
Somalia yamtimua balozi wa Umoja wa Mataifa
Global News

Serikali ya Somalia imemwamuru balozi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom kuondoka baada ya kumtuhumu kuwa ameingilia masuala ya ndani ya taifa hilo. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo imesema Bw Haysom, ”hakaribishwi tena Somalia na hawezi kuendelea kuendesha shughuli zake nchini.” Hatua hiyo imetokea baada ya mjumbe huyo kuandika barua akiuliza maswali mengi kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali wakati wa makabiliano yaliyotokea Baidoa katika jimbo la Kusini Magharibi wakati wa kumakatwa kwa naibu...

Like
599
0
Wednesday, 02 January 2019
Wagombea wa upinzani walalamikia dosari uchaguzi DRC
Global News

Wagombea wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamelalamikia dosari nyingi wanazosema zilitokea wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili. Milolongo mirefu ya wapiga kura ilishuhudiwa katika vituo vingi na mitambo ikafeli kwenye baadhi ya vituo. Aidha, upigaji kura uliathiriwa katika baadhi ya maeneo baada ya mvua kubwa kunyesha, huku baadhi ya wapiga kura wakilalamikia majina yao kutokuwepo kwenye sajili katika baadhi ya vituo. Mmoja wa wagombea wa urais wanaotaka kumrithi Rais Joseph Kabila anayeondoka baada ya kuongoza...

Like
425
0
Monday, 31 December 2018
Rajoelina atangazwa mshindi uchaguzi wa Madagascar
Global News

Kiongozi wa zamani wa Madagascar Andry Rajoelina ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa taifa hilo la kisiwa cha bahari ya Hindi katika matokeo ya awali yaliotangazwa na tume ya uchaguzi Alhamisi. Rajoelina alikuwepo wakati tume ya uchaguzi ikitangaza kwamba amepata asilimia 55.66 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 44.34 ya mshindani wake Marc Ravalomanana – ambaye hakuwepo wakati wa kutangazwa matokeo. Ravalomanana, ambaye pia ni rais wa zamani, amekosoa uchaguzi katika kisiwa hicho kilichoko nje ya pwani ya Afrika kwa...

Like
675
0
Friday, 28 December 2018
Trump awatembelea wanajeshi wa Marekani nchini IraqTrump awatembelea wanajeshi wa Marekani nchini IraqTrump awatembelea wanajeshi wa Marekani nchini IraqTrump awatembelea wanajeshi wa Marekani nchini IraqTrump awatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump na mke wake Melania Trump wamefanya ziara ya ghafla ya krismasi ya kuwatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq. Walisafiri kwenda huko usiku wa siku ya Krismasi kuwashukuru wanajeshi hao kwa huduma yao, mafanikio na kujitolea kwa mujibu wa White house. Bw Trump alisema Marekani haina mpango wa kuondoka nchini Iraq. Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya waziri wa ulinzi Jim Mattis kujiuzulu kufuatia mgawanyiko wa sera za Trump eneo hilo. Marekani ina wanajeshi 5,000...

Like
531
0
Thursday, 27 December 2018
Bobi Wine aendelea kuitikisa Uganda
Global News

Nyota wa muziki wa pop na mbunge wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi Ssentamu amekataliwa kufanya tamasha lake leo Disemba 26 kama alivyokuwa amepanga hapo awali. Msemaji wa polisi nchini Uganda, Emilian Kayima amesema kwamba Bobi Wine alikuwa hajaandika barua ya kuomba ruhusa kufanya tamasha hilo ndio maana hawawezi kumruhusu. “Tutakuwa katika ufukwe wa Busabala kuzuia shughuli hiyo na kuhakikisha usalama upo.Tamasha hili halikuwa limeruhusiwa kufanyika kwa sababu ya kutokidhi vigezo”,...

Like
648
0
Thursday, 27 December 2018
Shughuli za serikali ya Marekani kukwama msimu wa Krismasi
Global News

Sehemu fulani ya shughuli za serikali ya Marekani zitaendelea kusitishwa kwa siku tano, baada ya wajumbe wa baraza la Seneti kushindwa kupiga hatua siku ya Jumamosi kutokana na mkwamo kwenye ufadhili wa ujenzi wa ukuta. Kutokana na kusitishwa kwa shughuli za serikali, ambako kumeshuhudia baadhi ya mashirika yakisitisha operesheni zake siku ya Jumamosi (Disemba 22), Rais Donald Trump amesema atasalia mjini Washington katika sikukuu za Krismasi badala ya kwenda Florida. Aliandika kupitia Twitter, “Niko Ikulu nikifanya kazi kwa juhudi....

Like
504
0
Monday, 24 December 2018
Hatua ya Trump ya kuondoa majeshi ya Marekani yashangaza washirika wake
Global News

Uamuzi wa Rais Donald Trump wa kuyaondoa majeshi ya Marekani kutoka nchini Syria umekosolewa vikali. Bwana Trump alitoa tangazo hilo siku ya Jumatano, akisema kuwa kundi la Islamic State (IS) limeangamizwa. Lakini washirika wake wakuu, wakiwemo viongozi wa chama chake cha kisiasa cha Republicans na mataifa ya kigeni, yamekanusha madai hayo, na kusema kwamba, hatua hiyo inaweza kufufua tena kundi la Islamic State (IS). Vikosi vya Marekani vimesaidia pakubwa kuangamiza wanamgambo hao wa itikadi kali ya kijihad, kutoka maeneo ya...

Like
609
0
Thursday, 20 December 2018
Grace Mugabe aingia matatani
Global News

Polisi nchini Afrika Kusini imetoa amri ya kukamatwa kwa Grace Mugabe, mke wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi mwanamitindo wa Afrika Kusini, Gabriella Engels, mwaka 2017. Mwanasheria anayefanya kazi na shirika la kutetea haki za binadamu la AfriForum la huko Afrika Kusini, Garrie Nel amesema kuwa amethibitishiwa na Polisi kuhusu kutolewa kwa amri hiyo, na kuongeza kuwa ikiwa, Grace Mugabe akikanyaga kwenye ardhi ya Afrika Kusini atakamatwa. Aidha, mwanasheria huyo vile vile ametaka ufanyike...

Like
587
0
Thursday, 20 December 2018
Jeshi la Zimbabwe lalaumiwa kwa ‘kutumia nguvu kupita kiasi’
Global News

Jeshi la Zimbabwe lilitumia “nguvu nyingi” dhidi ya waandamanaji wa upinzani baada ya uchaguzi wa kiti cha Urais. Hayo yamesemwa na tume maalum iliyoundwa kuchunguza kiini cha ghasia zilizotokea nchini humo. Watu 6 waliuwawa, baada ya vikosi vya jeshi kutumwa ili kukabiliana na waandamanaji hao waliozua ghasia katika maeneo kadhaa ya mji mkuu Harare mnamo Agosti 1. Tume huru ya uchunguzi huo, inasema jeshi lilitenda mabaya makubwa bila huruma, wakati ilipoamua kuwamiminia risasi waandamanaji waliokuwa wakitoroka. Lakini baadhi ya...

Like
545
0
Wednesday, 19 December 2018