Global News

SERIKALI YA CHILE YATANGAZA HALI YA DHARURA KATIKA MJI ULIOKUMBWA NA TETEMEKO LA ARDHI
Global News

SERIKALI ya Chile imetangaza hali ya dharura katika mji uliokumbwa na tetemeko la ardhi linaloaminika kuwa lenye nguvu zaidi. Watu 11 wamepoteza maisha na wengine milioni moja wameacha makazi yao baada ya kutokea kwa tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha ritcha 8.3 kuleta athari siku ya Jumatano usiku. Tetemeko hilo ambalo ndilo kubwa zaidi duniani na la sita kutokea nchini humo kwa kipindi cha mwaka huu lilidumu dakika...

Like
241
0
Friday, 18 September 2015
MILIONI 6 WAOKOLEWA DHIDI YA VIFO VITOKANAVYO NA MALARIA DUNIANI
Global News

RIPOTI  mpya  ya  shirika  la  afya  duniani  WHO,  na shirika  la  kuwahudumia  watoto UNICEF imesema  zaidi ya  maisha  ya  watu  milioni  6 yameokolewa  kutokana  na ugonjwa  wa  malaria  katika  muda  wa  miaka  15  iliyopita. Uingiliaji  kati  katika  afya  ya  jamii  barani  Asia  na  eneo la  mataifa  ya  kaukasus  umekuwa  na  mafanikio makubwa  katika  kuudhibiti  ugonjwa  huo. Asilimia 80 ya vifo vitakavyotokana na Malaria mwaka huu inatarajiwa kuwa katika mataifa ya Afrika kusini ya...

Like
199
0
Thursday, 17 September 2015
WALINZI WA RAIS WAIPINDUA SERIKALI YA BURKINA FASO
Global News

KIKOSI cha walinzi wa rais kimeipindua Serikali ya mpito ya Burkina faso na kimetangaza katika runinga ya taifa kwamba kimevunja kile ilichokitaja kuwa serikali ya mpito isiyoambilika. Mwanachama wa kikosi hicho jenerali Gilbert Diendere ametajwa kuwa kiongozi mpya wa mpito. Mipaka yote imefungwa huku amri ya kutotoka nje ikiwekwa na Mkuu wa bunge amelitaka jeshi kuingilia kati ili kuzuia hatua hiyo aliyoitaja kuwa ya kundi dogo la...

Like
209
0
Thursday, 17 September 2015
CHILE YAPIGWA NA TETEMEKO, HOFU YA TSUNAMI YATANDA
Global News

TETEMEKO kubwa la ardhi limeipiga Chile na kusababisha tishio la kutokea kwa tsunami, katika eneo lake la pwani na maeneo mengine ya bahari ya Pacific. Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 8.3 katika vipimo vya ritcha, lilipiga maeneo ya pwani na kuenea kwa kilomita 250 kaskazini magharibi wa mji mkuu Santiago. Nchi hiyo imewahamisha wakazi milioni moja katika eneo la pwani, ambako tayari Rais wa Chile amethbitisha watu watano wamepoteza maisha baada ya tetemeko hilo...

Like
199
0
Thursday, 17 September 2015
HALI YA WASIWASI YATANDA BURKINA FASO
Global News

WALINZI wa rais nchini Burkina Faso wamemkamata rais wa mpito Michel Kafando na waziri mkuu Isaac Zida na hivyo kuitumbukiza nchi hiyo katika hali ya wasiwasi wiki chache tu kabla uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu kuondolewa madarakani kiongozi wa zamani Blaise Compaore. Kukamatwa kwao kulisababisha maandamano ya barabarani nje ya ikulu ya rais ambako viongozi hao walikuwa wakizuiliwa. Milio ya risasi ilisikika wakati wanajeshi walipokuwa wakiwatawanya mamia ya waandamanaji na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameghadhabishwa...

Like
191
0
Thursday, 17 September 2015
MUWINDAJI ATUHUMIWA KUSAFIRISHA SWARA
Global News

 MTAALAMU wa uwindaji anayeshutumiwa kuhusika na kifo cha simba aliyepewa jina Cecil nchini Zimbabwe amekamatwa kwa tuhuma za kusafirisha swara 29 kimagendo nchini Afrika Kusini. Theo Bronkhorst anazuiliwa mjini Bulawayo na  polisi wa nchini humo wamethibitisha. Bronkhorst anatarajiwa kusimamishwa kizimbani leo kwa kosa hilo la kusafirisha swara 29 kwa...

Like
250
0
Wednesday, 16 September 2015
CONGO: UPINZANI WATISHIA MAANDAMANO
Global News

VYAMA kadhaa vya upinzani nchini Congo vimeitisha maandamano katika mji mkuu wa Taifa hilo Kinshasa juu ya kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa Urais uliotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2016. Wiki iliopita mahakama ya kikatiba nchini humo ilitaka siku ya uchaguzi huo kutangazwa upya hatua ambayo wapinzani wamesema ni ya kutaka rais Joseph Kabila kusalia madarakani zaidi hata baada ya kukamilika kwa muda wake uliowekwa kikatiba. Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani tangu baba ake aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo auwawe mwaka...

Like
194
0
Tuesday, 15 September 2015
TURNBULL AAPISHWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA AUSTRALIA
Global News

MALCOLM Turnbull ameapishwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya kuondolewa katika mamlaka kwa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Tony Abbott. Turnbull aliyekuwa waziri wa mawasiliano katika serikali ya Abbott, sasa atakuwa waziri mkuu wa nne nchini humo tangu 2013 ambaye amesema kuwa huo ndio wakati bora zaidi wa kuwa raia wa Australia. Abbott, aliyeondolewa mamlakani Jumatatu baada ya kura ya haraka kufanywa katika chama tawala cha Liberal, amesema aliondolewa kwa “uchungu” lakini ameahidi kurahisisha shughuli ya mpito...

Like
212
0
Tuesday, 15 September 2015
RAIS WA GABON AITUHUMU UFARANSA
Global News

RAIS wa Gabon Ali Bongo amesema kuwa kukamatwa kwa mkuu wa majeshi wa Taifa hilo mjini Paris mnamo mwezi Agosti mwaka huu ni jaribio la kuifedhehesha Gabon. Rais Bongo alikuwa akizungumza katika makao rasmi ya rais Francois Hollande baada ya kukutana naye mjini Paris. Mkuu huyo wa majeshi aliyekamatwa Maixent Accrombessi alizuiliwa kwa muda katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle kwa tuhuma za ufisadi baada ya kandarasi ya sare za kijeshi nchini Gabon kupewa kampuni moja ya Ufaransa...

Like
157
0
Tuesday, 15 September 2015
GHANA: MAJAJI 34 MASHAKANI
Global News

JAJI mkuu wa Ghana . Georgina Theodora Wood amehutubia nchi kuhusu kashifa kubwa ya rushwa dhidi ya majaji na kuahidi kuchukua hatua na maamuzi ya haraka kuhusu madai dhdi ya majaji 34 wanaoshukiwa na kashifa hiyo. Hii ni mara ya kwanza tangu taarifa ya kashifa hiyo kutokea hali iliyosababisha Jaji huyo mkuu kuzungumza hadharani ambapo amesema kuwa idara ya sheria inapitia katika kipindi kigumu kutokana na maadili ya kisheria yaliyowekwa na wakongwe wa sheria kutetereka. Jaji huyo mkuu amesema kuwa...

Like
179
0
Tuesday, 15 September 2015
ULAYA YATAKIWA KUANDAA VITUO VYA KUWAPOKEA WAHAMIAJI
Global News

UMOJA wa mataifa umeelezea masikitiko yake dhidi ya mataifa kadhaa ya bara la Ulaya, namna yanavyozingatia sheria mbalimbali zinazokinzana kuhusiana na mipaka yake. Shirika linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa hatua hii itawaacha maelfu ya wakimbizi katika hali ya kutatanika kisheria. Shirika hilo la UNHCR, limesema kwamba muungano wa bara la Ulaya, unatakiwa kuandaa vituo vya kuwapokea wahamiaji, kuwaandikisha na kuwapiga msasa wahamiaji na wale wanaotafuta makao huko hasa wanaowasili nchini Ugiriki, Italia, na...

Like
211
0
Monday, 14 September 2015