MAKAMANDA wa kijeshi kutoka pande mbili zinazopigana nchini Sudan Kusini wanakutana mjini Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili njia za kutekeleza makubaliano ya kusitisha vita. Mkutano huo utazungumzia masuala yakiwemo kuondolewa vikosi kutoka vitani, kubuni maeneo yasiyo chini ya ulinzi wa kijeshi na kuondolewa kwa wanajeshi wa kigeni kutoka nchini humo. Makubaliano ya amani yaliyotiwa sahihi mwezi uliopita yakiwa na lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe hayakutekelezwa huku pande zote zikilaumiwa kwa kukiuka makubaliano...
MAWAZIRI wa Mambo ya Ndani kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo mjini Brussels katika mkutano wa dharura kujadili hali ya wakimbizi. Watajadili mapendekezo ya kuwapa makazi wakimbizi 120,000 katika sehemu mbalimbali za umoja huo waliowasili nchini Ugiriki, Italia na Hungary. Mawaziri hao watajadili pia kuanzishwa kwa vituo maalumu kuwasaidia, kuwasajili na kuwachunguza wakimbizi wanaowasili katika mataifa hayo matatu ya eneo la...
MISRI imesema jeshi lake la ulinzi limeua raia 12 kwa bahati mbaya,wakiwemo watalii kutoka Mexico wakati wa operesheni ya kupambana na ugaidi. Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo imetuma kikosi kwa ajili ya kufanya uchunguzi kuhusu tukio hilo kwa upande wa Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amekemea tukio hilo na ameitaka serikali ya Misri kufanya uchunguzi wa...
UCHUNGUZI uliofanywa Nchini Ghana, na mwandishi habari za uchunguzi , Anas Aremeyaw Anas uliomchukua miaka miwili umegundua kuwa majaji pamoja na viongozi wa juu wa mahakama nchini humo wanakula rushwa . Anas tayari amekwisha waandikia waraka Rais wa nchi hiyo pamoja jaji mkuu ambao nao tayari wamekwisha andaa tume ya kuwahoji majaji wote wanaotuhumiwa. Anes, Mwandishi wa habari za uchunguzi, ambaye pia ni mwanasheshia aliwafuata majaji kuwapa hongo ili wawaachie huru watuhumiwa. Katika maeneo mengine alijifanya mwenye kushitaki ili atoe...
JESHI la anga la Ufaransa limeanza kurusha ndege za upelelezi katika anga ya Syria kukusanya data katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Dola la Kiislamu. Waziri wa mambo ya kigeni ya Ufaransa Laurent Fabius amesema kuwa ndege hizo zinaamua muda muafaka na hatua za kuchukuliwa dhidi ya wapiganaji wa IS. Australia leo imetangaza kujiunga na mashambulizi ya anga nchini Syria, na itawachukua wakimbizi elfu 12,000...
KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekosoa jinsi bara la Ulaya linavyoshughulikia mzozo wa sasa wa Wahamiaji. Amesema hali imefikia katika kile alichokiita , ishara ya aibu” kutokana na tofauti zilizopo kimataifa. Jana Jumanne, wahamiaji kadhaa, ikiwa ni pamoja na familia zilizo na watoto, wamelazimisha kupita vizuwizi vya polisi katika kambi ya kuandikishwa katika mpaka wa Hungary na ...
POLISI wamewakamata watu watatu waliongia na bomu katika sehemu mpya ya maduka mjini Nairobi. Watu waliondolewa kwenye sehemu hiyo ya Garden City,ili kuwawezesha polisi kulitegua bomu hilo. Mkuu wa polisi katika mji wa Nairobi alimewaambia waandishi wa habari kwamba bomu hilo la kutengenezwa liligunduliwa na walinzi kwenye kituo cha usalama cha sehemu hiyo ya maduka. Mkuu huyo amearifu kuwa watuhumiwa hao watatu wanachunguzwa ili kubaini , iwapo wana uhusiano na magaidi, na hasa kundi la al-Shabab la nchini...
MAELFU ya waandamanaji waliokuwa wakipeperusha bendera za Uturuki wamevamia makao makuu ya chama kikuu cha Kikurdi cha HDP. Jengo hilo lililoko katika mji mkuu wa Ankara baada ya kuvamiwa lilichomwa moto. Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu amelaani vikali mashambulizi na uvamizi huo katika ofisi za kisiasa na hata kwa nyumba za habari na ametoa wito wa kusitisha...
JESHI la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno, kama sehemu ya juhudi za vita dhidi ya Boko Haram. Imebainika kuwa Kundi hilo limekuwa likitumia farasi kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanavijiji huku jeshi la Nigeria likionekana kupata mafanikio katika vita vyake dhidi ya Boko Haram. Taarifa zinasema kuwa tayari kumepigwa marufuku kwa matumizi ya pikipiki ambazo zilikuwa zikitumiwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwasafirisha wapiganaji wake katika...
KIONGOZI wa kanisa katoliki Duniani Papa Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa hilo waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi katika kanisa hilo. Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama. Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na kuolewa upya hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kushiriki kwenye huduma zinazotolewa na...
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ameyakosoa vikali madai ya kumtaka Rais Bashar al-Assad ajiizulu akisema kuwa wanaoyatoa ndio wenye dhamana ya umwagikaji damu nchini Syria. Akizungumza mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Hispania aliye ziarani nchini Iran José Manuel Margallo, waziri Zarif amesema kuwa hakuna suluhisho la kijeshi kwa mzozo wa Syria na kwamba hakuna anayeweza kulazimisha matakwa yake kwa watu wa Syria. Ingawa Zarif hakuitaja nchi yoyote kwa jina, lakini uwezekano mkubwa...