Global News

Ubelgiji yalifungua tena ”Jumba la Makumbusho ya Afrika” lenye utata
Global News

Jumba la Makumbusho linalohifadhi sana iliyoporwa Afrika wakati wa ukoloni limefunguliwa tena karibu na Brussels baada ya kukarabatiwa. Maafisa wake wanasema jumba hilo sasa limejaribu kubadilisha mtazamo wa kikoloni. Jumba hilo la makumbusho lililo katika mji mdogo wa Tervuren karibu na Brussels, ambalo siku za nyuma lilikosolewa vikali kutukuza ukoloni wa Mbelgiji na unyama wake dhidi ya wenyeji wa nchi zilizotawaliwa na nchiyo, lilifungua tena milango yake Jumamosi (08.12.2018) baada ya miaka 5 ya kazi za kulikarabati. Kuanzishwa kwa...

Like
857
0
Monday, 10 December 2018
Wabunge wa Somalia waandaa hoja ya kutokuwa na imani na Rais
Global News

Wabunge nchini Somalia wamewasilisha hoja bungeni ya kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais Mohammed Abdullahi Farmajo. Mmoja wa wabunge ambaye amechochea hoja hiyo Abdifitah Ismail Dahir ameiambia BBC wanamtuhumu Rais kwa uhaini baada ya kusaini makubaliano ya kisiasa na kiuchumi na Ethiopia na Eritrea. Amesema Rais ameshindwa kuwashirikisha taarifa wenzie kuhusiana na makubaliano yanayohusisha bandari za Somalia. Wanamlaumu pia Rais kwa madai ya kuwarejesha wahalifu isivyo halali. Wabunge wapatao 92 wanapaswa kusaini hoja hiyo ya...

Like
701
0
Monday, 10 December 2018
‘Marekani ikitengeneza makombora sisi pia tutatengeneza’ aonya rais Putin
Global News

Urusi itaunda makombora yaliyopigwa marufuku chini ya mkataba wa vita baridi ikiwa Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo, ameonya rais Vladimir Putin. Tamko lake linakuja baada ya shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi Nato, kuilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa makubaliano kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa ya kadri (INF). Makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na USSR,yalipiga marufuku mataifa hayo yote mawili dhidi ya kuunda makombora ya masafa mafupi na yale kadri. Rais wa...

Like
705
0
Thursday, 06 December 2018
Wahouthi, serikali ya Yemen mazungumzoni Sweden
Global News

Wawakilishi wa serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia wameelekea Sweden, ambako tayari ujumbe wa waasi wa Kihouthi ulishawasili mazungumzo ya kusaka amani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Ujumbe wa serikali ya Yemen uliondoka mjinji Riyadh, Saudi Arabia, mapema leo Jumatano, huku chanzo kimoja ndani ya serikali hiyo kikiliambia shirika la habari la Ujerumani, dpa, kwamba wanatazamiwa kuwasili mjini Stockholm jioni. Tayari ujumbe wa Wahouthi ulishawasili nchini Sweden tangu jana Jumanne, wakisindikizwa na mjumbe maalum wa Umoja...

Like
547
0
Thursday, 06 December 2018
Marlboro mbioni kuhamia kwenye uzalishaji wa bangi
Global News

Kampuni ya Altria, ambayo ni wazalishaji wa chapa maarufu ya sigara za Marlboro wapo katika mazungumzo na kampuni moja ya kuzalisha bangi nchini Canada ili wawekeze mtaji wao. Kampuni ya Cronos imethibisha kuwa katika mazungumzo na Malboro ambayo inataka kuinunua ili kuingia rasmi kwenye biashara ya bangi. Canada iliruhusu kisheria uvutaji wa bangi kama starehe mwezi wa Oktoba mwaka huu, ni nchi ya pili kufanya hivyo baada ya Uruguay. “Tupo kwenye mazungumzo, kampuni ya Altria inataka kuwekeza kwenye kampuni yetu...

Like
1395
0
Thursday, 06 December 2018
Apandikizwa uso mpya baada ya kujaribu kujiua kwa kujipiga risasi
Global News

Cameron Underwood anasema hakumbani sana na watu wanaomkodolea macho wale kumuuliza maswali tangu amabandikiziwe uso. “Niko na pua na mdomo kwa hivyo ninaweza kutabasamu, kuongea na kula chakula kigumu tena,” anasema. Cameron alikuwa azingumza miaka miwili baada ya kujipiga risasi alipojaribu kujiua mwaka 2016. Alipoteza pua lake, sehemu kubwa ya chini ya mdomo na meno yake yote isipokuwa moja tu katika kisa hicho. “Ninashukuru sana kwa upasuaji huu wa kupandikizwa uso kwa sababu imenipa fursa ya pili ya maisha,”...

Like
594
0
Wednesday, 05 December 2018
Ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binaadamu
Global News

Umoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binadamu kuliko ilivyokua huko miaka ya nyuma. Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Poland, kiongozi wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa, amesema kuwa mwaka huu ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi duniani. Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajia kuleta mabadiliko kwa kuanza kufanyia kazi mkataba wa hali ya hewa wa ParisUmoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto...

Like
554
0
Monday, 03 December 2018
Viongozi wawasili Buenos Aires kwa mkutano wa G20
Global News

Viongozi wa nchi 20 zilizoendelea zaidi kiuchumi wataanza mkutano wa kilele leo mjini Buenos Aires, Argentina, ambao unatarajiwa kugubikwa na mivutano ya kibiashara, pamoja na mzozo mpya kati ya Urusi na Ukraine. Rais wa Marekani Donald Trump ni miongoni mwa viongozi ambao tayari wametua mjini Buenos Aires, baada ya kufuta mkutano wake na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kutokana mzozo mpya kati ya Urusi na Ukraine katika bahari ya Azov. Kuwepo kwa Trump katika mkutano huo kunapokelewa kwa maoni mchanganyiko,...

Like
616
0
Friday, 30 November 2018
Ukraine yawazuia wanaume wa Urusi kuingia nchini mwake
Global News

Maafisa wa Ukraine leo wamewazuia wanaume raia wa Urusi wa umri kati ya  miaka 16 na 60 kuingia nchini humo katika hatua ya karibuni ya kuongezeka kwa mvutano baina ya nchi hizo mbili jirani Mgogoro wa muda mrefu ambao uliibuka  tena Jumapili iliyopita wakari walinzi wa mpakani wa Urusi walipozigonga na kuanza kuzifyatulia risasi meli tatu za Ukraine karibu na Rasi ya Crimea, ambayo Urusi iliiinyakua mwaka wa 2014. Meli hizo zilikuwa zikijaribu kupita katika mlango wa Kerch kuelekea katika...

Like
612
0
Friday, 30 November 2018
Mamia watumia njia ya mkato katika mbio za Marathon, China
Global News

Wanariadha takriban 250 waliokuwa wanashiriki mbio za half marathon nchini China walinaswa na kamera za siri wakitumia njia ya mkato kumaliza mbio hizo. Wengi walipitia vichakani na wengine kwenye vichochoro. Waandalizi wa mbio hizo zilizofanyika Shenzhen, China, wanasema waligundua pia wakimbiaji 18 waliokuwa wamevalia vibango vya nambari za kuwatambua wanariadha vilivyokuwa bandia. Kulikuwa pia na wanariadha watatu ambao wameelezwa kuwa wanariadha walaghai waliokuwa wanajifanya kuwa watu tofauti. Wote waliopatikana wakifanya udanganyifu huo...

1
618
0
Friday, 30 November 2018
Ujerumani yaandaa mkutano kuhusu Uislamu
Global News

Mkutano kuhusu Uislamu nchini Ujerumani umefunguliwa leo mjini Berlin, huku wachambuzi wakitarajia mafanikio madogo. Waziri wa mambo ya ndani Horst Seehofer mwenye msimamo mkali dhidi ya Uislamu, ndiye mwenyekiti. Mhafidhina Horst seehofer, mwanasiasa mwenye msimamo mkali, alisababisha mvutano mwezi Machi alipomkosoa moja kwa moja Kansela Angela Merkel akiipinga kauli yake kwamba “Uislamu una nafasi  yake Ujerumani.” Waziri mkuu huyo wa zamani wa mkoa wa Bavaria alisema Waislamu wanaoishi hapa bila ya shaka ni sehemu ya...

1
602
0
Thursday, 29 November 2018