Mtikisiko na vishindo vya wana mazoezi wa 95.5 morogoro vyasikika mapema asubuhi ya leo MATUKIO KWA...
“Mchezo wa October 12 ni muhimu sana kabla ya October 16, 2018 kwa hiyo sasa hivi tuangalie wa October 12 kwa sababu inabidi tukacheze kule Cape Verde halafu October 16 tunamalizia hapa Wallace Karia, Rais TFF. Watanzania waiunge mkono Taifa Stars, Waziri Mwakyembe na serikali yetu kwa kuchangia lakini mchango huo ni nauli yao wenyewe ya kuwafikisha Cape Verde. Cape Verde tutakwenda kwa mambo mawili, tangu ndege yetu imenunuliwa mipango yake ilikuwa ni kuwa na safari za nje ya nchi....
Kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita alikimbizwa hospitalini baada ya kuondolewa uwanjani kwa machela alipoumia akicheza mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Napoli hatua ya makundi. Liverpool walilazwa 1-0 ugenini Italia. Keita, aliyejiunga na klabu hiyo kutoka RB Leipzig ya Ujerumani kwa £48m majira ya joto mwaka huu, aliondolewa uwanjani baada ya kucheza dakika 19 pekee. Aliumia...
Kelvin De Bruyne arejea mazoezini kuungana na Nyota wenzake wa Manchester City Kiungo huyo raia wa uberigiji alipata majeraha septemba 19 mwaka huu kwenye dhidi ya...
Licha ya Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama kutangaza kuwa Mwamuzi wa pambano la watani wa jadi atatangazwa Alhamis ya wiki hii, taarifa za ndani zinasema Jonesia Rukiyaa atachezesha pambano hilo. Imeelezwa kuwa Rukiyaa atashika filimbi katikati ya Uwanja huku akisaidiana na Ferdnand Chacha pamoja na Mohammed Mkono. Aidha, chanzo hicho kimesema Mwamuzi wa mezani atakuwa ni Elly Sasii. Jana ilielezwa pia kuwa Mwanamama Florentino Zabron kutoka Dodoma angechezesha mechi hiyo lakini kumefanyika mabadiliko tena mengine....
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa hana tatizo na kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba licha ya kumwambia mchezaji huyo kwamba hatowahi tena kuwa nahodha wa klabu hiyo. Mourinho alimwambia Pogba kwamba sio nahodha wa klabu hiyo kutokana na wasiwasi kuhusu tabia yake. ”Ukweli ni kwamba nimechukua uamuzi huo ili asiwe nahodha wa pili lakini hakuna tatizo lolote kati yetu”, alisema Mourinho. ”Mimi ndio meneja ninaweza kufanya maamuzi kama hayo”. Akizungumza na chombo cha habari cha...
Masoud Djuma Kocha Msaidizi wa Simba ataendelea kubaki Dar es Salaam, ikiwa timu inakwenda Mkoani Mwanza kwa ajili ya kucheza michezo miwili ya Ligi kuu ampapo tarehe 20, September Simba SC itacheza na Mbao Fc kwenye Uwanja wa CCM Kirumba na Mchezo mwingine ni ule dhidi ya Mwadui FC kwenye uwanja huo huo wa CCM Kirumba utakao pigwa tarehe 22, September. Hatua hiyo inakuja baada ya viongozi wa kumkabidhiwa majukumu mengine ya kuwanoa wachezaji waliobakia Dar wakiwemo Juuko Mushid na...
Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard anaweza kufunga mabao 40 msimu huu na kujishindia tuzo ya mfungaji mabao bora Ligi ya Premia, kwa mujibu wa meneja wa klabu hiyo Maurizio Sarri. Kwa mujibu wa BBC, Hazard alifunga mabao matatu dhidi ya Cardiff Jumamosi na kuwawezesha The Blues kupata ushindi wa 4-1. Kufikia sasa amefunga mabao matano katika mechi tano zilizochezwa, moja kushinda mchezaji anayemfuata. Baada ya mechi hiyo ya Jumamosi, Sarri alisema Mbelgiji huyo huenda akawa ndiye mchezaji bora zaidi Ulaya....
Michuano ya vijana walio chini ya miaka 17 inayoendelea kutimua vumbi jijini Dar es salaa kufuzu fainali za Afcon leo Tanzania (Serengeti Boys ) watakuwa dimbani dhidi ya Rwanda (Amavubi Junior )vijana wa Kagame katika mchezo ambao utatoa matokeo ya nani atakuwa kinara katika kundi A. Mpaka sasa Rwanda na Tanzania zimetinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ikiwa Tanzania ndio inaongoza kundi hilo kwa idadi ya magoli ya kufunga ,katika Kundi B Burundi na Sudani tayari zimeyaaga mashindano...
Shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya Nyota wanaoshindania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya UEFA kwa mwaka 2017/2018 ambao ni Cristiano Ronaldo wa Juventus, Luka Modric wa Real Madrid na Mohammed Salah wa Liverpool. Hii ni baada ya kufanya mchujo wa wachezaji 10 kati ya hao ni washindi wa Kombe la Dunia mwaka huu. Luka Modrić (Real Madrid na Croatia) Mshindi wa Kombe la Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) 2018, Mchezaji Bora wa Dunia (Kombe la Dunia ‘FIFA World Cup’...
Baada ya siku takribani tano kupita tangu kikosi cha Yanga kiweke kambi mjini Morogoro, imeelezwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ameomba mechi moja kukipima kikosi chake. Taarifa kutoka Morogoro zinasema Zahera ameomba apatiwe timu moja ambayo haishiriki Ligi Kuu Bara ili aweze kukipima vizuri kikosi chake kabla ya kufikia hatua ya kucheza na timu za daraja la juu. Taarifa zinaeleza Yanga wametuma maombi kwa timu zaidi ya moja mjini humo na ambayo itakubali watakipiga nayo leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi...