Sports

COENTRAO KUTUA MONACO KWA MKOPO
Slider

Real Madrid na Monaco zimekubaliana dili la beki wa kushoto wa Rea Madrid mreno  Fabio Coentrao kwenda kuitumikia Monaco kwenye Ligue 1 kwa mkopo katika msimu wa mwaka 2015-16. Klabu hizi mbili zilitangaza makubaliano hayo siku ya jumatano Coentrao, 27, alijiunga na Real Madrid akitokea Benfica mwaka 2011 kwa ada ya Euro milioni...

Like
240
0
Thursday, 27 August 2015
MAN U YAILAZA BRUGGE 4-0
Slider

Katika muendelezo wa mechi za mkondo wa pili kufuzu kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya, usiku wa kuamkia leo timu kadhaa zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi. Manchester Utd imefanikiwa kusonga mbele kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Club Brugge na kufanya matokeo kuwa 7-1, katika mikondo yote miwili. Katika mchezo huo nahodha Wayne Rooney alidhihirisha kuwa bado yupo vizuri katika kucheka na nyavu, baada kufunga mara tatu. Droo...

Like
209
0
Thursday, 27 August 2015
BEIJING: WANARIADHA 2 WA KENYA WAPEWA MARUFUKU YA MUDA
Slider

Wanariadha wawili wa Kenya wamebainika kwamba walitumia dawa za kusisimua misuli katika mashindano yanayoendelea ya IAAF mjini Beijing. Wawili hao Koki Manunga na Joyce Zakary wamepewa marufuku ya mda baada ya kutumia dawa hizo kulingana na IAAF. Wanariadha hao wa mita 400 walilengwa kabla ya kushiriki katika mbio hizo katika hoteli yao mnamo tarehe 20 na 21 Agosti kulingana na taarifa hiyo ya...

Like
221
0
Wednesday, 26 August 2015
CELTIC NA MONACO ZATOLEWA KLABU BINGWA ULAYA
Slider

Usiku wa kuamkia leo timu kadhaa za soka barani Ulaya zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kufuzu kuingia katika hatua ya makundi kwenye mashindano ya klabu bingwa barani humo. Monaco ya Ufaransa, walikuwa nyumbani kucheza dhidi ya Valencia. Hadi mwisho wa mchezo huo Monaco imeibuka kidedea kwa jumla ya bao 2-1. Hata hivyo Valencia imefuzu hatua ya makundi kwa jumla ya bao 4-3, baada kushinda bao 3-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza. Nayo Malmo FF ikaiadhibu Celtic kwa jumla ya...

Like
241
0
Wednesday, 26 August 2015
BALOTELI KUREJEA AC MILAN KWA MKOPO
Slider

Mchezaji mpotevu wa Liverpool Mario Balotelli atarejea AC Milan kwa mkopo wa msimu mmoja baada ya klabu hizo mbili kuafikiana kuhusu mkataba wa mkopo Jumatatu, ripoti Italia zilisema. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia ameshuka sana tangu ajiunge na klabu hiyo ya Ligi ya Premia baada ya Kombe la Dunia mwaka jana na hajachezea Italia tangu wakati huo. Lakini huku mechi za Ubingwa Ulaya zikitarajiwa kuanza Ufaransa majira yajayo ya joto, mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 25 anatarajiwa kurejea...

Like
212
0
Wednesday, 26 August 2015
ARSENAL, LIVERPOOL HAKUNA MBABE
Slider

Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech aliokoa mara mbili mipira ya hatari iliyokuwa ikielekea langoni mwake na kuisaidia timu yake kupata alama moja katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool. Katika mchezo huo mikwaju miwili ya Philippe Coutinho ililenga mwamba huku kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey akikataliwa goli alilofunga kipindi cha kwanza kutokana na kuwa katika mstari wa kuotea. Cech aliokoa kwa mara nyingine mkwaju wa karibu wa Christian Benteke na kuucheza tena kwa umahiri mpira uliopigwa...

Like
215
0
Tuesday, 25 August 2015
ROBERTO MARTINEZ KUONGEZA NGUVU EVERTON
Slider

Meneja wa klabu ya Everton, Roberto Martinez ameelezea mpango wake wa kufanya usajili mpya kwa wachezaji watatu kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili. Miongoni mwa wachezaji anaowatazama meneja huyo ni mlinzi wa klabu ya River Plate, Ramiro Funes Mori, 24 Lakini pia Everton wamekuwa na mazungumzo na klabu ya Dynamo Kiev juu ya kumchukua mshambuliaji Shakhtar Donetsk’s Bernard. Lakini pia Everton imeonyesha kuvutiwa na mshambuliaji wa Uruguay Leandro...

Like
239
0
Monday, 24 August 2015
MOURINHO: USHINDI WETU UTAWANYIMA RAHA WAPINZANI
Slider

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema matokeo ya timu yake dhidi ya West Brom yatawanyima raha wabaya wao. Ameyasema hayo baada ya kupata ushindi wa kwanza tokea msimu mpya wa ligi ya England ianze. Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita, Chelsea iliibuka kidedea kwa jumla ya bao 3-2 dhidi ya West Brom na kushuhudia nahodha wake John Terry akilimwa kadi nyekundu katika dakika ya 54 ya mchezo baada ya kumchezea vibaya mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon. Ushindi...

Like
218
0
Monday, 24 August 2015
MANCHESTER CITY YAITANDIKA EVERTON 2-0
Slider

Manchester City imefanikiwa kurejea kileleni kwenye Premier League kufuatia ushindi wao dhidi ya klabu ya Everton. Ushindi huo wa ugenini ulifanikishwa na Aleksandar Kolarov pamoja na Samir Nasri na kuufanya mchezo kumalizika kwa matokeo ya 2-0. City walikuwa awali wameshinda mechi moja pekee kati ya sita walizochezea Goodison Park – ushindi huo wa pekee ukiwa kwenye safari yao ya kushinda taji 2014. Kutwaa tena taji hilo ndilo lengo lao msimu huu baada yao kutumia pesa nyingi tena kujengwa upwa kikosi,...

Like
269
0
Monday, 24 August 2015
HAPPY BIRTHDAY E SPORTS
Slider

Leo kipindi pendwa cha michezo Tanzania cha E SPORTS kimefikisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake Katika kusherehekea siku hii muhimu kikosi cha watangazaji wa michezo ndani ya Efm waliungana na wadau wa Stars supporters kusherehekea siku muhimu katika historia ya mapinduzi ya michezo nchini Timu hii machachari kabisa inaundwa na Maulid Kitenge, Omary Katanga, Ibrahim Masoud, Sud Mkumba, Mussa Kawambwa, Oscar Oscar, Francis Mhando, Yusuph Mkule pamoja na Dokta...

Like
670
0
Friday, 21 August 2015
OTAMENDI NDANI YA MAN CITY
Slider

Beki wa timu ya taifa ya kandanda Argentina, Nicolas Otamendi, amesaini na miamba wa Uingereza, Machester City, timu hiyo imetangaza Alhamisi kufuatia makubaliano na Valencia wa Uhispania kukamilisha biashara hiyo. Otamendi, 27, amekubali kandarasi ya urefu wa miaka mitano ingawa dau husika halikutangazwa. City wameimairisha ngome yao na Otamendi ambaye ataungana tena na mwenzake wa zamani katika majitu wa Ureno, FC Porto, Eliaquim Mangala na ndugu yake kwenye kikosi cha Argentina, Martin Demichelis pamoja na nahodha Vincent Kompany wa...

Like
214
0
Friday, 21 August 2015