Bwana E Mr Jimmy Jiam wa EFM akipozi na mshindi wa EFM Muziki Mnene Bango eneo la Sinza, jijini Dar Es Salaam. Mshindi huyo alionekana akiwa anasikiliza 93.7 EFM na pia alikuwa ameweka stika ya EFM kwenye sehemu yake ya kazi. Mshindi mwingine wa EFM Muziki Mnene Bango akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa zawadi na bwana E wa EFM. Dada huyo alikuwa ameweka stika ya EFM kwenye sehemu yake ya biashara eneo la Magomeni, jijini Dar Es Salaam. Bwana...
WAKATI leo rais wa Sudan Salva Kiir akitarajia kusaini muafaka wa kugawana madaraka mjini Juba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza mbinyo kwa rais huyo, likionya kuwa liko tayari kuchukua hatua ya haraka ikiwa hatosaini muafaka wa kumaliza vita vilivyodumu miezi 20. Rais Kiir anatarajiwa kusaini muafaka wa kugawana madaraka mjini Juba , pamoja na viongozi wa Kenya, Uganda, Sudan na Ethiopia, lakini msemaji wake amesema bado hajaridhishwa. Kiongozi wa waasi Riek Machar alisaini makubaliano hayo wiki moja...
UMOJA wa Ulaya umesema uko tayari kuisaida Hungary kulishughulikia ongezeko la wahamiaji wanaovuka mipaka yake. Umoja huo umesema utaipa nchi hiyo kile kinachoitwa kuwa ni hadhi ya ‘eneo hatari la uhamiaji’, ikiwa na maana kuwa nchi hiyo ipewe raslimali za ziada kupambana na hali hiyo. Hayo yanajiri baada ya serikali ya Hungary kusema kuwa zaidi ya wakimbizi 2,000 waliingia nchini humo hapo jana wiki hii pekee nakuifanya nchi hiyo ikabiliwe na changamoto ya kuwasili nchini humo raia wa nchi jirani...
IMEELEZWA kuwa uvuvi haramu kwa njia ya sumu wilayani Ukerewe unahatarisha maisha ya watu kwa kuugua ugonjwa wa ini na figo huku wengine wakipoteza maisha kwa ugonjwa huo. Wakiongea na Efm baadhi ya wakazi wa ukerewe walioathirika na ulaji wa samaki waliovuliwa kwa sumu wamesema uvuvi haramu ndio chanzo cha wao kuugua ugonjwa wa ini na figo na kufanya familia zao kuishi kwa taabu. Kwa upande wake daktari kutoka katika hospitari ya rufaa Bugando jijini mwanza Mathayo James...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imevitaka vyama vya siasa kuzingatia ratiba ya kampeni ya uchaguzi wa rais kwa kufanya mikutano kwa tarehe, sehemu na mahala kwa mujibu wa ratiba. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na NEC, vyama vyote vya siasa vinatakiwa vizingatie ratiba ya kampeni ya uchaguzi wa rais na viache kufanya mikusanyiko ya aina yoyote ambayo haipo katika ratiba ya kampeni hizo. Chama kitakachokiuka maelekezo hayo kitakuwa kimekiuka kipengele cha maadili ambacho kinaelekeza kuwa ni wajibu wa vyama vya...
Usiku wa kuamkia leo timu kadhaa za soka barani Ulaya zilishuka dimbani kutafuta tiketi ya kufuzu kuingia katika hatua ya makundi kwenye mashindano ya klabu bingwa barani humo. Monaco ya Ufaransa, walikuwa nyumbani kucheza dhidi ya Valencia. Hadi mwisho wa mchezo huo Monaco imeibuka kidedea kwa jumla ya bao 2-1. Hata hivyo Valencia imefuzu hatua ya makundi kwa jumla ya bao 4-3, baada kushinda bao 3-1 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza. Nayo Malmo FF ikaiadhibu Celtic kwa jumla ya...
Mchezaji mpotevu wa Liverpool Mario Balotelli atarejea AC Milan kwa mkopo wa msimu mmoja baada ya klabu hizo mbili kuafikiana kuhusu mkataba wa mkopo Jumatatu, ripoti Italia zilisema. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia ameshuka sana tangu ajiunge na klabu hiyo ya Ligi ya Premia baada ya Kombe la Dunia mwaka jana na hajachezea Italia tangu wakati huo. Lakini huku mechi za Ubingwa Ulaya zikitarajiwa kuanza Ufaransa majira yajayo ya joto, mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 25 anatarajiwa kurejea...
IMEELEZWA kuwa Mlipuko mkubwa uliotokea nje ya kituo cha kusambazia gesi katika mji wa Herat nchini Afghanistan, umesababisha vifo vya watoto kumi na mtu na kumjeruhi mmoja. Msemaji wa hospitali mojawapo karibu na eneo hilo amesema kwamba watu wengine 18 wamejeruhiwa katika eneo palipotokea mlipuko ambalo hutumika kama kambi ya wakimbizi. Sanjari na hayo baadhi ya picha katika mitandao ya kijamii bado zinaonesha uwepo wa miale ya moto angani ingawa haijabainika iwapo mlipuko huo ulikuwa ajali au shambulizi....
SHUGHULI ya kuzika mabaki ya zaidi ya watu arobaini imefanyika katika eneo lililojitangazia uhuru la Somaliland ambapo Mabaki hayo yalipatikana katika kaburi moja. Taarifa zinasema kuwa Mifupa hiyo ya watu ilipatikana wakati mitaro ya mabomba ya maji ilipokuwa ikichimbwa katika mji mkuu Hargeisa. Hata hivyo bado inaaminika kwamba watu hao waliuawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea mwaka...
JESHI la polisi mkoa wa kipolisi Ilala limelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi wa vyama vinavyounda umoja wa Katiba ya wananchi-UKAWA– kutokana na mgombea wa nafasi ya Urais kupitia umoja huo Edward Lowasa kufika eneo la kariakoo kwa lengo la kutaka kuwaona wafanyabiashara wa soko hilo. Lowasa amefanya ziara leo ya kutembelea baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo Tandale, Tandika na Kariakoo ili kutathimini hali ya maisha ya wananchi. Kamanda wa polisi Ilala Lucas...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Mikoa na Serikali za Mitaa kusimamia changamoto na mapungufu katika usimamizi wa ujenzi wa barabara nchini ili kuleta manufaa kwa wananchi. Ameongeza kuwa ni wajibu wa ngazi hizo za uongozi kuhakikisha kuwa kazi za barabara hazifanyiki kwa viwango duni na kukomesha uwepo wa upendeleo katika uteuzi wa wakandarasi wa kazi za ujenzi wa barabara kinyume cha Sheria ya Manunuzi. Rais Kikwete ameyasema hayo wakati...