Kampuni ya mashindano ya bahati nasibu inayodhamini Ligi Kuu ya Kenya imetia saini mkataba wa kuwa mdhamini wa klabu ya Hull City ya Uingereza. Kampuni hiyo ya SportPesa, ambayo huandaa mashindano ya kubashiri matokeo ya mechi nchini Kenya, imetia saini mkataba wa kudhamini Hull City kwa misimu mitatu. Klabu ya Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye Ligi ya Premia msimu utakaoanza mwezi ujao. Hull City watafungua msimu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya mabingwa Leicester City. Kwa mujibu wa taarifa kutoka...
Mechi ya kirafiki kati ya miamba wa Uingereza, Manchester City na Manchester United, imefutiliwa mbali kutokana na mvua kubwa. Mechi hiyo ilikuwa imepangiwa kuchezewa uwanja waBirds Nest, Uchina na ingekuwa ya kwanza kwa mameneja wapya Pep Guardiola na Jose Mourinho. Jumapili, Mourinho alikuwa amedokeza kwamba hali katika uwanja huo ilikuwa mbaya. Hata kabla ya mechi kuahirishwa rasmi, Guardiola alikuwa amesema matumaini yake ni kwamba wachezaji wake wasiumie. City na United wamesema “waandalizi wa mchuano huu pamoja na klabu zote mbili”...
Wafanyakazi wengi kusini mwa India leo wamepewa likizo kwa sababu ya filamu ya mwigizaji filamu inayoanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema leo.Filamu hiyo ni ya mwigizaji nyota wa asili ya Tamil, Rajinikanth. Hatua hiyo imechukuliwa kuzuia watu kutumia visingizio kama vile kwamba wanaugua ili wasifike kazini. Inahofiwa wengine huenda hata wangezima simu zao au kutofika kazini bila kueleza sababu. Filamu hiyo kwa jina Kabali inaonyeshwa katika kumbi 12,000 za sinema leo. Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana...
Shirikisho la Soka barani Africa (CAF) limepata mdhamini mpya baada ya kumalizika kwa mkataba wake na kampuni ya mawasiliano ya Orange. Orange imekuwa mdhamini mkuu wa mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009. Kabla ya hapo, kampuni nyingine ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne. Sasa, mdhamini mpya atakuwa kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa. Kampuni hiyo itaanza kwa kudhamini michuano ya Kombe la Taifa Bingwa Afrika mwaka 2017 ambayo itaandaliwa nchini...
Katika tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa huwa ni fahari kubwa sana akiwa ni bikira. Mathalan ni dhihirisho la mwanamke kuwa amelelewa na kutunzwa vyema. Ni dhihirisho la usafi. Hata hivyo jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa watoto wao wa kike. Amini usiamini wazazi huwa wanamlipa ”Fisi” kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza. Wanaamini kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii! Malimwengu haya. Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini...
Mshambulizi wa Ufaransa na Juventus Paul Pogba ameomba kuihama klabu hiyo ya Italia.Magazeti ya michezo nchini Italia yamechapisha habari hiyo kama kichwa kuwa Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 23 ameomba aruhusiwe kuondoka kwani posho lake linavutia. La Gazzetta dello Sport liliongoza na kichwa ”Pogba ameamua kuondoka Juventus”Gazeti hilo linadai kuwa mfaransa huyo amekwisha kubaliana posho lake na Mashetani wekundu huku ikisisitiza kuwa sababu kuu iliyomfanya makamu wa mwenyekiti wa klabu hiyo bwana Ed Woodward asiandamane na...
Licha ya kuwapo kwa wabunifu kadhaa za ndege na magari, huku wananchi wakitaka Serikali iwaunge mkono kwa kuwawezesha, huenda wengi wao wasifikie ndoto zao. Tayari mkazi wa Tunduma mkoani Songwe, Adam Kimikile (34) aliyetengeneza helikopta ni kama amepigwa ‘stop’ na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kujihusisha na utengenezaji au ubunifu wa ndege bila kufuata taratibu. TCAA imesema anayetaka kutengeneza ndege ama vifaa vyake, azingatie kanuni za usafiri wa anga na kupata kibali cha mkurugenzi wake mkuu na hatua...
BAADA ya Serikali kufanya uchambuzi wa sifa za Wanafunzi wanaostahili kusoma program maalum ya Ualimu wa sekondari kwa masomo ya sayansi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),ni wanafunzi 382 ndio wamekidhi kusoma program hiyo kati ya wanafunzi 7,805 waliondolewa katika mgomo wa walimu wa chuo hicho. Akizungumza na waandishi habari Ofisini kwake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa wamefanya uchambuzi huo ili kutoa haki kwa watu wenye sifa ya kusoma program maalum kwa walimu wa...
Bodi ya utalii nchini inakanusha madai ya mwandishi Cara Anna kufuatia taarifa yake aliyoitoa kwenye chombo cha habari cha Miami Herald chenye makao yake nchini Marekani akiripoti kifo cha Gugu Zulu Raia wa Afrika kusini aliyefariki dunia wakati akijaribu kupanda mlima Kilimanjaro, hapa Tanzania. Kwenye ripoti ya mwandishi huyo amedai kuwa raia huyo wa afrika Kusini amepoteza maisha wakati akijaribu kupanda mlima Kilimanjaro nchini Kenya Zulu mwenye umri wa miaka 38 ni dereva wa mbio za magari alikuwa katika ziara...
Kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Mkenya Tom Alex Olaba aagana na uongozi wa klabu hiyo, akizungumza kupitia Sports headquarters Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwile amesema uongozi wa Ruvu Shooting umetoa pongezi zao pamoja shukrani kwa kocha huyo aliyeirudisha Ruvu Shooting kwenye ligi kuu aidha ameongeza kuwa kwa sasa klabu hiyo itaongozwa na kocha mzawa mwenye uzoefu na klabu...
Mtendaji mkuu wa Azam Fc, SADI KAWEMBA kupitia Sports Headquarters amekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kwamba mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ ametemwa kikosini na kocha Mkuu wa klabu hiyo Mhispania, Zeben...