Ni habari mbaya kwa wale wanaofurahia kile wanachofikiri ni kikombe kimoja cha divai kwa siku. Utafiti mpya wa kimataifa ulimwenguni uliochapishwa katika jarida la Lancet umethibitisha utafiti uliopita ambao umeonyesha kwamba hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe. Watafiti wanakubali kwamba unywaji wa kiwango cha kadri unaweza kukulinda dhidi ya ugonjwa ya moyo lakini waligundua kwamba hatari ya saratani na magonjwa huzidi faida yoyote ya pombe mwilini. Mwandishi wa utafiti alisema matokeo yake yalikuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya...
Wagombea wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamelalamikia dosari nyingi wanazosema zilitokea wakati wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili. Milolongo mirefu ya wapiga kura ilishuhudiwa katika vituo vingi na mitambo ikafeli kwenye baadhi ya vituo. Aidha, upigaji kura uliathiriwa katika baadhi ya maeneo baada ya mvua kubwa kunyesha, huku baadhi ya wapiga kura wakilalamikia majina yao kutokuwepo kwenye sajili katika baadhi ya vituo. Mmoja wa wagombea wa urais wanaotaka kumrithi Rais Joseph Kabila anayeondoka baada ya kuongoza...
Jeshi la Zimbabwe lilitumia “nguvu nyingi” dhidi ya waandamanaji wa upinzani baada ya uchaguzi wa kiti cha Urais. Hayo yamesemwa na tume maalum iliyoundwa kuchunguza kiini cha ghasia zilizotokea nchini humo. Watu 6 waliuwawa, baada ya vikosi vya jeshi kutumwa ili kukabiliana na waandamanaji hao waliozua ghasia katika maeneo kadhaa ya mji mkuu Harare mnamo Agosti 1. Tume huru ya uchunguzi huo, inasema jeshi lilitenda mabaya makubwa bila huruma, wakati ilipoamua kuwamiminia risasi waandamanaji waliokuwa wakitoroka. Lakini baadhi ya...
Jangili mmoja nchini Marekani ameamriwa kuangalia filamu ya wanyama ya Bambi kila mwezi baada ya kukutwa na hatia ya kuua “mamia” ya mbawala. Muwindaji huyo kutoka Missouri David Berry Jr anatakiwa kuangalia filamu hiyo walau mara moja kwa mwezi wakati akitumikia kifungo chake cha mwaka mmoja gerezani. Alitiwa nguvuni mwezi Agosti pamoja na ndugu zake wawili kwa kuwaua mbawala, kisha kuwachinja na kuondoka na vichwa huku akiacha miili ya wanyama hao ioze, waendesha mashtaka wamesema. Kesi hiyo ni moja ya...
Mama wa mtoto aliye raia wa Yemeni amezuiwa kumuona kijana wake aliye karibu kuaga dunia kutokana na sheria ya kuwazuia wageni kutoka nchini mwake, familia imeeleza. Mtoto Abdullah Hassan alizaliwa na maradhi ya ubongo ambapo madaktari walisema hataweza kuishi. Ndugu wanasema mama yake anataka kumuona kwa mara ya mwisho kabla ya kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua. Baba yake anasema mama wa Abdullah hawezi kwenda nchini Marekani kutokana na marufuku iliyowekwa na utawala wa Trump. Abdullah na Baba yake ni raia...
Mahakama Kuu nchini Afrika Kusini imeamuru Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma kulipia gharama zote za kesi zilizofunguliwa dhidi yake alipokuwa madarakani. Mahakama hiyo ya Kaskazini mwa Guateng imeeleza kuwa Zuma atapaswa kulipia gharama zote za uendeshaji kesi zake tangu mwaka 2005 bila kuihusisha Serikali. “Serikali haihusiki na gharama zozote za kesi dhidi ya Bw. Jacob Zuma, katika mashtaka ya jinai yaliyofunguliwa dhidi yake kwa namna yoyote,” imeeleza sehemu ya uamuzi wa Mahakama Kuu. “Mwendesha Mashtaka wa Serikali...
Umoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binadamu kuliko ilivyokua huko miaka ya nyuma. Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Poland, kiongozi wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa, amesema kuwa mwaka huu ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi duniani. Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajia kuleta mabadiliko kwa kuanza kufanyia kazi mkataba wa hali ya hewa wa ParisUmoja wa mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto...
Urusi imezishambulia na kuziteka meli tatu za kivita za Ukraine zilizokuwa baharini katika rasi ya Crimea katika kisa ambacho kimezidisha uhasama baina ya mataifa hayo mawili. Meli mbili ndogo za kivita, pamoja na meli moja ya kusindikiza meli ndizo zilizotekwa na wanajeshi wa Urusi. Wahudumu kadha wa meli za Ukraine wamejeruhiwa. Kila taifa linamlaumu mwenzake kwa kusababisha kisa hicho. Leo Jumatatu, wabunge wa Ukraine wanatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuanza kutekelezwa kwa sheria za kijeshi. Mzozo wa sasa ulianza pale Urusi...
China imethibitisha inamzuia mkuu wa Interpol aliyepotea Meng Hongwei. Beijing imesema alikuwa anachunguzwa na tume ya kupambana na rushwa nchini humo kwa ukiukaji wa sheria. Meng, ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China, aliarifiwa kupoeta baada ya kusafiri kutoka mji wa Lyon Ufaransa , kuliko na makao makuu ya Interpol kwenda China mnamo Septemba 25. Interpol imesema imepokea barua ya kujiuzulu kwake mara moja kutoka kwa ofisi ya rais. Familia yake Meng haijawasiliana naye tangu...
Beka Flavour akilishambulia jukwaa la muziki mnene kinyumbani nyumbani SNURA ANELETA MAJANGA KWENYE JUKWAA LA MUZIKI MNENE 2018...
Mtikisiko na vishindo vya wana mazoezi wa 95.5 morogoro vyasikika mapema asubuhi ya leo MATUKIO KWA...