CHANJO ya ugonjwa wa Ebola imeanza kufanyiwa majaribio nchini Liberia, ambapo wafanyakazi 600 wa kujitolea wanatarajiwa kushiriki katika awamu ya kwanza ya majaribio hayo. Chanjo hiyo inayolenga kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya Ebola, imeanza kutolewa jana kwenye mji mkuu wa Liberia, Monrovia. Ingawa Waliberia wengi wameonyesha wasiwasi, wataalamu wa afya wamesema chanjo hiyo tayari imeonyesha mafanikio na ni salama kwa matumizi ya binaadamu....
BAADA ya hivi karibuni kujitokeza kwa migogoro baina ya viongozi wa Chama cha Alliance for Change –ACT, Chama hicho kimeamua kufanya marekebisho ya katiba ya chama ili kukinusuru na migogoro ya namna hiyo. Akizungumza na EFM Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama SAMSONI MWIGAMBA amesema kuwa Marekebisho hayo yatasaidia kusuruhisha migogoro inayojitokeza kwa baadhi ya viongozi wanaotumiwa kukivuruga chama. Amebainisha kuwa katiba mpya imerekebisha mapungufu ya katiba ya awali ambayo ilikuwa haina kamati ya nidhamu na maadili...
RAIS wa Ujerumani JOACHIM GAUCK na msafara wake amewasili nchini . Mara baada ya kuwasili akiwa ameambatana na mkewe Bibi SCHADT amelakiwa na Makamu wa Rais Dokta MOHAMED GHARIB BILALI pamoja na burudani za ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali na wananchi waliojitokeza kumpokea. Rais huyo ambaye anaitembelea Tanzania kwa mara ya kwanza kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais JAKAYA KIKWETE leo amepokelewa katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo Rais huyo akiwa na mwenyeji wake, JAKAYA KIKWETE...
Everton imemsajili mshambuliaji wa Tottenham Aaron Lennon kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu kabla dirisha la usajili halijafungwa hapo jumatatu Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ameichezea klabu ya Spurs mara 267 mara baada ya kuwasili kwenye klabu hiyo mwaka 2005 na kufanikiwa kutwaa kombe la ligi Bosi wa Klabu ya Everton Roberto Martinez amezipiku klabu za Hull City na Stoke City katika kuupat wino wa mshambuliaji huyo na kuweka matumaini makubwa kutokana na uwezo pamoja uzoefu wake kwenye...
Suge Knight kushtakiwa kwa mauaji ya rafiki yake na chanzo cha habari kimeeleza kuwa mkanda wa video uliorekodiwa kwenye tukio hilo utatumika kama ushahidi kuendesha kesi hiyo. Maafisa wa polisi huko Loss Angels wamesema kuwa mashtaka hayo yanahusishwa na kifo cha Terry Carter aliuawa siku ya alhamis baada ya Suge kumgonga na gari huko Compton Kesi hiyo itahusisha mashtaka ya kugonga na kukimbia pia kujeruhi na kusababisha kifo Mamlaka za kusimamia sheria zimekataa kumpa dhamana Suge siku ya jumatatu kwa...
MAMLAKA ya mapato Tanzania –TRA, imewataka wananchi kujiepusha na biashara za magendo kwani adhabu zinazotolewa kwa wahusika wanaokamatwa na na biashara hizo ni kali na zinarudisha nyuma maendeleo yao Taifa. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu na Mawasiliano wa TRA Richard Kayombo na kuongeza kuwa ni wakati sasa wananchi wanapaswa kuinua uchumi wa nchi yao kwa kulipa kodi. Kayombo ameongeza kuwa TRA imejipanga kikamilifu kwani kipo kikosi kinachoitwa fast Team ambacho kipo mahususi kwa ajili...
KAMPUNI ya simu za Airtel, leo imezindua promosheni kabambe itakayogharimu shilingi milioni mia tisa ijulikanayo kama airtel yatosha zaidi ,itakayomuwezesha mteja wake kijishindia gari aina ya Toyota IST. Akiongea wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa masoko ya airtel, Levi Nyakundi amesema promosheni hiyo ni nafasi ya pekee kwa wateja wao wanaojiunga na vifurushi vya airtel yatosha zaidi vya siku,wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana na pesa wanazozitumia, lengo likiwa ni kuhakikisha wanatoa huduma na...
JESHI la Nigeria limesema kuwa limefaulu kusambaratisha shambulio la pili la Boko Haram, juma moja tu baada ya kusambaratisha jaribio jingine la mashambulizi katika eneo la kaskazini mashariki mwa Maiduguri. Msemaji wa jeshi hilo Meja Jenerali Chris Olukade, amesema kuwa waliwauwa waasi wengi wa Boko Haram katika shambulio hilo lililotokea mapema Alfajiri leo, huku wakipata bunduki, risasi na magari yaliyokuwa yakitumika na waasi hao wa Boko Haram. Lakini wapiganaji wa vijijini wameliambia Shirika la Utangazaji la BBC kuwa wanakanusha hilo...
HATIMAYE majaribio makubwa ya chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola, yamepangwa kuanza nchini Liberia. Matarajio ni kuwa zaidi ya watu elfu thelathini watajitokeza katika zoezi hilo kubwa la majaribio ya chanjo hiyo iliyotengezwa na kampuni mbili za GSK na Merck. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, zaidi ya watu elfu tisa wamefariki katika mlipuko huo mkubwa wa Ebola ambapo Mataifa yaliyoathirika zaidi magharibi mwa Afrika ni pamoja na Guinea, Sierra Leone na...
KAMATI ya Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum la Katiba imewataka Watanzania kutokubali kutafasiriwa katiba pendekezwa na Wanasiasa au kikundi chocchote na badala yake waisome na kuijua ikiwa ni pamoja na kufuatilia matangazo ambayo Serikali inayatangaza. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Kwanza AGUSTINO MATEFU amesema kuwa kuna baadhi ya kikundi cha watu wachache ambacho kimevaa uhusika kwa ajili ya kuwataka waislam wasipigie kura katiba pendekezwa kwa kuwa hakuna kipengele cha Mahakama...
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE amemtaka waziri wa maliasili na Utalii ambaye pia ni mbunge wa Singida mheshimiwa LAZARO NYALANDU kujiuzuru endapo atashindwa kutekeleza agizo la utoaji wa tangazo katika gazeti la serikali juu ya tozo na mapato yatokanayo na wageni wanaolala katika hoteli za kitalii zinazozunguka hifadhi za Taifa hadi ifikapo leo jioni. Mheshimiwa ZITTO ametoa kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia taarifa za utekelezaji wa mikakati mbalimbali zilizotolewa na kamati ya Ardhi, maliasili na...