Christian Atsu alifanikiwa kuziona nyavu mara mbili na kuifanya Ghana iicharange mabao 3-0 timu mwenyeji wa mashindano ya Afcon Guinea huko Malabo siku ya jumapili Atsu ameifanya timu yake hiyo ya Black Stars kupata njia nyeupe kwenye robo fainali alipofungua goli mnamo dakika ya nne kabla ya Kwesi Appiah hajaongeza goli linguine Atsu mshambuliaji anaechezea Everton kwa mkopo akitokea...
Klabu ya Crystal Palace imetangaza kwenye tovuti yao siku ya jumapili kwamba amemsajili msenegali Pape Souare akitokea Ufaransa Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alihitimu mafunzo ya soka kutoka kwenye kituo cha kukuza vipaji vya mpira wa miguu cha Lille’s youth academy na kuiwakilisha Senegal katika michuano ya AFCON huko Equatorial Guinea Souare amekuwa mchezaji wan ne kumwaga wino na kutua Crystal Palace katika dilisha la usajili kwenye kipindi hiki cha mwezi wa kwanza baada ya Jordon Mutch, aliekuwa...
Bondia wa mchezo wa Masumbwi nchini Francis Cheka ambae makazi yake yapo mjini morogoro amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kukutwa na hatia yakumpiga mtu aliekuwa akimdai, akizungumza na efm kupitia kipindi cha Sport Headquarter baba mzazi wa Francis Cheka amesema haikuwa sahihi kwa mwanae kupewa hukumu hiyo na badalayake wangekaa na kuzungumza ili kuyamaliza matatizo hayo. Mzee huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kuna watu wenye chuki na mwanae wameitumia kesi hiyo ya muda mrefu kutimiza...
SERIKALI ya Jordan imesema imedhamiria kutumia kila njia kuyaokoa maisha ya raia wao anaeshikiliwa na wafuasi wa itikadi kali wa dola ya kiislam IS. Habari hizo zimetangazwa na shirika la habari la Jordan-Petra. Hapo Jana wanamgambo hao wa IS walimuonyesha katika kanda ya video mwandishi wa habari wa Japan Kenji Goto waliyemkata kichwa Serikali ya Japan imesema kanda hiyo ni ya kweli. Hapo awali wafuasi hao wa itikadi kali walionya watawauwa mahabusi wote wawili wa Japan ikiwa serikali mjini Amman...
shambulio la wanamgambo wa itikadi kali wa Boko Haram katika mji wa kaskazini mashariki ya Nigeria-Maiduguri,limeangamiza maisha ya watu wasiopungua wanane. Mashahidi wanasema Boko Haram wamepambana na vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na raia katika mapigano ambayo yalianza saa tisa za alfajiri ya leo. Vikosi vya serikali vinasaidiwa na jeshi la nchi kavu, na lile la wanaanga. Katika siku za hivi karibuni Boko Haram wameeneza hujuma zao hadi katika nchi jirani ya Cameroon....
WAKAZI wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jerry Silaa wakati akiongea kwenye kilele cha sherehe za kutimiza miaka 38 ya chama hicho mkoani Lindi zilizofanyika katika tawi la Mnazi Mmoja lililopo kata ya Mingoyo wilaya ya Lindi mjini. Silaa mbaye pia ni Mstahiki...
SERIKALI imesema imedhamiria kuweka mikakati madhubuti itakayowezesha lugha ya Kiswahili kutumika katika ngazi zote nchini ikiwemo utoaji wa hukumu katika mahakama zote ili kuleta haki na usawa kwa wananchi kupitia lugha hiyo. Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria mheshimiwa UMMY MWALIMU C wakati akitoa ufafanuzi wa swali lililoulizwa na mbunge wa viti maalumu mheshimiwa SABRINA SUNGURA ambaye alitaka kujua mikakati ya serikali ya kuhakikisha lugha ya Kiswahili inatumika na kuleta manufaa kwa watu wote....
D’banj afanya bonge la sherehe huko Nigeria kwa kuwakutanisha mastar kadhaa kutoka nchini humo lakini pia mwanamuziki huyo alithibitisha nguvu yake duniani kwakumshusha Amber Rose akiwa kama mshereheshaji wa sherehe hizo za maadhimisho ya...
nyuma ya pazia uandaaji wa video ya Four Five Seconds ya Rihanna, Kanye West and Paul McCartney...
Leo ilikuwa ni siku ambayo baadhi ya wafanyakzi wa kituo hiki cha 93.7efm ambao wamezaliwa mwezi huu wa kwanza waliunganishwa kwa pamoja na kufanyiwa suprise na wafanyakzi wenzao wa kituo hiki picha ni baadhi ya wafanyakazi hao wapatao saba wakisherehekea...
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Kandanbda Africa CAF imetangaza kwamba Guinea ndio imeshinda katika bahati nasibu ya kusonga mbele dhidi ya Mali. Uwamuzi ulichukuliwa Alhamisi saa kumi saa za Africa Magharibi mjini Malabo, na hivyo sasa Guinea itapambana na Ghana na Algeria itapambana na Ivory Coast....