KAMATI Ndogo ya maadili ya Chama cha Mapinduzi – CCM, leo inakutana kwa lengo la kuanza kazi ya kuwachunguza makada wake wakiwemo wajumbe wa NEC na Kamati kuu. Hatua ya kuanza kuchunguza kwa makada wa chama hicho hususani waliotuhumiwa kwenye sakata la Tegeta Escrow, ni utekelezaji wa agizo la Kamati Kuu ya CCM, iliyokutana Visiwani Zanzibar kujadili masuala mbalimbali wiki iliyopita. Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, amesema vikao vya kamati hiyo vitaanza leo na kasha...
Mataifa yanayounda kundi B ambayo ni Drc, Tunisia, Cape verde na Zambia katika michuano ya kombe la mtaifa Afrika zimejikuta zikikosa mbabe baada timu zote kuibuka na sare ya kufungana 1-1 Mchezo wa kwanza wa kundi hilo ulipigwa kwakuikutanisha Zambia na Congo ambapo Zambia ilitangulia kuziona nyavu za Drc kupitia mnamo dakika ya pili bao lililofungwa na mchezaji wake Given Singuluma na kudumu hadi mapumziko Bao hilo lilisawazishwa na mchezaji wa Drc Yannick Bolasie kwenye dakika ya 66 hadi mwisho...
Katika harakati za maandalizi ya vikosi vya timu za mataifa 16 kutoka katika bara la afrika kuelekea kunako michuano mikubwa yakusaka taifa bingwa katika mchezo wa soka inayo taraji kuanza mnamo tarehe 17/01/2015. Leo hii macho na masikio ya mashabiki walio wengi yanataka kusikia ama kuona ni taifa gani litaibuka kidedea katika michuano hiyo? Tutazame ubora na mafanikio ya timu mojamoja ambapo kwa sasa machoyetu yanaitazama timu ya taifa ya CONGO DRC ikiwa katika kundi “B” likiongozwa na Zambia,Tunisia na...
Timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) inatarajiwa kuwasili katika jiji la Mwanza, Januari 21 mwaka huu kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Taifa Stars ambapo nyasi zitawaka moto kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura, Amavubi yenye msafara wa watu 26, wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itawasili kwa ndege ya RwandAir na siku hiyo hiyo jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM...
Kama uliwahi kufiria kupewa zawadi ya gari na mpenzi wako kikubwa kwa sasa ni kujiuliza mara mbili kwamba iwapo mkiachana hali itakuwaje?. Baada ya kuachana kwa njia salama na amani Jason Derulo na Jordin Sparks miezi kadhaa nyuma huku kila mmoja wao akiyazungumzia mahusiano yao kama ni mambo binafsi hivyo hawakuwa na sababu ya kuweka wazi. Sasa Jordin Sparks alipokuwa akihijiwa kwenye moja ya vipindi vya redio kuhusu mahusiano yao ndipo alipogusia gari aina ya BMW alilopewa na aliekuwa mpenzi...
MJUMBE maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na Elimu GORDON BROWN, ameutaka Ulimwengu kulaani kutumiwa kwa Wasichana wadogo na kundi la waasi wa Boko Haram nchini Nigeria, kama washambuliaji wa kujitoa mhanga kwa kujilipua. BROWN ambaye ni Waziri Mkuu wa Zamani wa Uingereza, amekiita kitendo hicho kuwa Unyama mpya, wa waasi hao. Matamshi yake yamekuja baada ya ripoti kwamba Boko Haram imewatumia wasichana watatu kufanya mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria mwishoni mwa Wiki...
WAZIRI wa Mambo ya Nchi za nje wa Marekani JOHN KERRY amefanya mazungumzo leo na Waziri mwenzake wa Ufaransa LAURENT FABIUS mjini Paris, kuelezea mshikamano wa nchi yake na watu wa Ufaransa, baada ya shambulio la kigaidi wiki iliopita. KERRY amemueleza FABIUS kwamba hakuweza kuhudhuria maandamano ya Mshikano Jumapili iliopita kwa sababu ya ziara iliyopangwa tangu awali nchini...
MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, Jaji FRANCIS MUTUNGI amevitaka vyama vyote vya siasa kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria , Katiba na Kanuni ili kuepusha migogoro. Aidha msajili huyo amevitaka vyama hivyo view mfano mzuri wa kwa jamii kwa kudumisha Amani na Utulivu ndani ya vyama vya siasa. Kauli hiyo ameitoa leo katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kufuatia kuwepo kwa wimbi la migogoro ndani ya vyama hivyo....
NAIBU WAZIRI wa Maliasili na Utalii mheshimiwa MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na Serikali. Akizungumza na EFM Mheshimiwa MGIMWA amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali. Mheshimiwa MGIMWA amewataka vijana wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya Kiuchumi na Sayansi na Teknolojia na ndio sababu...
leo macho na masikio yetu yapo katika taifa la Jamhuri ya Gabon, Gabon ni nchi ya Afrika magharibi ya kati. Ime pakana na Guinea ya Ikweta, Kamerun, Jamhuri ya Kongo na Guba ya Guinea. Taifa hilo limepata uhuru kutoka kwa Ufaransa mnamo 17 Agosti 1960 Jamhuri hii imeongozwa na Rais wa wili, toka ipate uhuru akiwa ni Autokrat; na rais Aliyeshikilia El Hadj Omar Bongo amekua katika uongozi toka mwaka 1967 hadi sasa (2006) yeye ndiye kiongozi Afrika aliyeshikilia uongozi kwa mda mrefu. Gabon ni nchi yenye neema sana kuliko nchi...
KIONGOZI wa kundi la wapiganaji wa Kilebanoni la Hezbollah amethibitisha taarifa zinazodai kuwepo mmoja wa viongozi wa juu ndani ya kundi hilo anatuhumiwa kutumwa na Israel kuwapepeleza. Shekh Sheikh Hassan Nasrallah amesema kiongozi huyo anayetuhumiwa tayari anashikiliwa na kundi hilo tangu abainike miezi mitano wakati akifanya kazi kwenye idara ya usalama ya kundi hilo la Hezbollah. Kauli ya Shekh Nasrallah imekuja siku chache baada ya kutolewa taarifa kupitia vyombo vya habari vya Lebanon zinazodai kuwepoa kwa ofisa wa ngazi za...