WANAWAKE nchini wametakiwa kuachana na matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango na badala yake watumie njia asilia ili kuepuka madhara yatokanayo na njia za kisasa. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la kutetea uhai Pro-life wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na masuala ya afya ya uzazi na uzazi salama kwa akina mama. Amesema kuwa shirika hilo limeweka mikakati ili...
BUNGE la Jamhuri ya muungano wa Tanzania leo linaanza mjadala kuhusu sakata la wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta –ESCROW- kutokana na zoezi la kugawa ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali-CAG- na ya Takukuru kwa wabunge wote kukamilika. Taarifa zinaeleza kuwa mjadala huo unaanza kwa wabunge mara baada ya kamati ya –PAC- ikiongozwa na mbunge wa kigoma kaskazini mheshimiwa ZITTO KABWE kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi bungeni. Mbali na hayo suala la muingiliano wa madaraka kati ya bunge na...
WATU KUMI wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuanguka mjini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza kuwa Watu saba wamejeruhiwa pia baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka usiku. Mkuu wa Idara ya dharula Jenerali Mamdouh Abdul Qader amesema vikosi vya uokoaji vinawasaka Watu 15 wanaokisiwa kunasa kwenye kifusi. Mara kadhaa majengo yameanguka nchini humo, sababu kubwa ikiwa ni ujenzi usiofuata kanuni na Sheria pia usimamizi mbovu wa taratibu za ujenzi. Wakazi wa majengo ya karibu na lilipoanguka jengo...
SERIKALI imeshauriwa kuangalia upya suala la marekebisho ya kodi katika baadhi ya vifungu vya sheria ikiwemo kupunguza kiwango cha –VAT– kutoka asilimia 18 hadi kufikia asilimia 16 hususani katika sekta ya utalii ili kuboresha uchumi wa nchi. Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya hesabu za bunge mheshimiwa ANDREW CHENGE wakati akitoa maoni ya kamati hiyo mara baada ya kusomwa kwa mara ya pili muswada waongezeko la thamani ya kodi nchini-VAT-la mwaka huu...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea salamu za pole kutoka kwa Rais wa Marekani Barak Obama. Katika salamu zake Rais Obama ameelezea kufurahishwa na taarifa kwamba Rais Kikwete anaendelea vyema kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji kwa mafanikio na kuondoa tatizo la tezi dume alilokuwa nalo. Katika salamu zake, Rais Obama amesema kuwa alipata heshima kufanya ziara rasmi nchini Tanzania mwaka 2013, na pia kumualika Rais Kikwete kwenye mkutano wa Marekani na viongozi wa Afrika...
Paul, Peter and Jude Okoye walimpoteza mama yao miaka miwili nyuma inasikitisha saana kusema kwamba jana pia wamempoteza baba yao mzazi Kwa mujibu wa chanzo cha habari kimedai kuwa Mr. Okoye hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa goti na kuwa salama kiafya lakini hapo jana alipata ajali ya ndani baada ya kuteleza na kichwa chake kugonga sakafu ya marumaru Ingawa hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Peter, Paul na Jude Okoye ila Lola Omotayo-Okoye kupitia akaunti yake ya Instagram ameshea ujumbe wa...
WAZIRI wa Fedha wa Urusi, ANTON SILUANOV, amesema Urusi imepoteza Dola Bilioni 40 kwa mwaka kutokana na vikwazo ilivyowekewa na nchi za Magharibi kwa madai ya kuhusika katika mzozo wa Ukraine. Hata hivyo, Rais VLADIMIR PUTIN amesema hasara hiyo sio madhara makubwa kwa Uchumi wa taifa lake. SILUANOV ambaye alikuwa akitoa hotuba katika Kongamano la Kiuchumi mjini Moscow amebainisha kuwa wamepata hasara ya Mabilioni ya fedha kutokana na vikwazo vinavyohusishwa na siasa za Urusi kuelekea eneo hilo na kuongeza kuwa...
GHASIA zimezuka nchini Marekani, baada ya Wanasheria kuamua kutomfungulia Mashtaka Polisi wa Kizungu aliyeua Kijana Mweusi. Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Vitu mbalimbali vimechomwa moto, baada ya jopo la Wanasheria nchini humo kuamua kutomfungulia Mashtaka polisi DAREN WILSON, ambaye amemuua kwa kumpiga risasi kijana Mweusi MICHAEL BROWN. Tukio hilo lilitokea katika mji wa Ferguson mwezi Agusti mwaka huu. Kwa upande wake Rais wa Marekani BARACK OBAMA ametaka kuwepo kwa amani, licha ya kueleweka kwamba baadhi ya raia wa nchi hiyo watakuwa...
ZAIDI ya Wanawake 100 wa Jamii ya Kimasai wameandamana na kwenda kulala msituni kwa muda wa siku mbili wakipinga kitendo cha Serikali kukata miti ya Asili katika kijiji cha Matebete ,Kata ya Itamboleo Wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya. Wanawake hao wamechukua uamuzi huo wakipinga hekta zaidi ya 30,000 za miti wanayoitegemea katika shughuli zao kukatwa bila wao kushirikishwa. Mmoja wa Wanawake hao aliefahamika kwa jina la SOFIA KALEI ameeleza kuwa hawako tayari kuona msitu huo ukiteketezwa kwa sababu umekuwa...
UANDIKISHAJI wa Wananchi katika daftari la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao umeshaanza umeonekana kudorora. Hayo yamebainika baada ya EFM kutembelea vituo mbalimbali vya kujiandikisha jijini Dar es salaam. Akizungumza na EFM Mmoja wa Mawakala wa Uandikishaji Mtaa wa Msolome Kinondoni B ABDAN SENGODA ameeleza kuwa mahudhurio ya Wananchi sio mazuri tangu zoezi hilo...
...