Msanii kutoka Tanzania Shaa kutoka aliyefanya Vizuri kwenye wimbo wa Sugua gaga wimbo uliomfanya afungue ukurasa mpya wa muziki wake kwakujizolea mashabiki zaidi kutoka uswahilini. Hivi karibuni msanii huyo amekuwa nchini Kenya kikazi ambapo pia amefanya kazi na msanii Red Sun kutoka Kenya na kushoot video ya wimbo ambao hadi sasa umeonyesha ramani nzuri kwake. Shaa ni miongoni mwa wasanii wachache watakaobahatika kushea jukwaa na msanii wa Kimataifa kutoka Marekani Wyclef Jean ambae mwishoni mwa wiki hii anatarajiwa kuwepo nchini...
POLISI nchini Israel wamepambana na vijana wa Kipalestina waliokuwa wakirusha mawe ndani ya uwanja wa msikiti wa Al-Aqsa leo baada ya makundi ya Wayahudi wenye msimamo mkali kutangaza mipango ya kuzuru eneo hilo licha ya wiki kadhaa za hali ya wasi wasi. Ziara hiyo iliyopangwa na kundi la Wayahudi ikiwa ni pamoja na wanasiasa wa siasa za kizalendo zaidi ilikuwa ifanyike wiki moja baada ya jaribio la mauaji dhidi ya mmoja kati ...
MATOKEO ya awali ya uchaguzi mdogo nchini Marekani yanaonesha kuwa chama cha Republican kimechukua udhibiti wa baraza la Seneti kwa kupata kiasi ya viti 51 katika baraza hilo lenye viti 100. Pia chama hicho kinaelekea kupata ushindi wa kishindo katika baraza la wawakilishi kwa miongo kadhaa. Warepublican wamefaidika na wimbi la kutoridhika kwa wapiga kura na kutoa pigo kwa rais Barack Obama ambalo litapunguza uwezo wake wa kupitisha ajenda ...
JESHI la Polisi kupitia kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es salaam leo limeanza rasmi zoezi la ukaguzi wa magari ikiwa ni pamoja na kufanya makabidhiano ya Stika kutoka kampuni ya Vodacom na Puma ili kupunguza ajali za barabarani. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani MOHAMED MPINGA amesema kuwa Stika hizo ambazo ni za magari makubwa, madogo na pikipiki zitasaidia kupunguza ajali baada ya vyombo hivyo kukaguliwa kabla ya kuingia...
BARAZA la Mitihani la Tanzania limeidhinisha kutoa matokeo ya mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi uliuofanyika September 10 hadi 11mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Katibu mtendaji wa Baraza la mitihani Dokta CHARLES MSONDE ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa 808,085 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 429,624 sawa na asilimia 53.17 na wavulana 378,461 sawa na asilimia 46.83. Dokta MSONGE amethibitisha kuwa jumla ya watahiniwa 451,392 kati ya watahiniwa 792,118...
Nicholas Aaron “Nick” Young Mcheza kikapu huko Marekani ambae amezaliwa june 1 mwaka 1985 kwa sasa mahusiano yake na rapa anaefanya vizuri duniani raia wa Austria Iggy Azalea yamepamaba moto. hivi karibuni wawili hao walitokea kwenye upiga picha katika maandalizi ya sherehe za kitaifa huko Marekani, kwa sasa wawlili hao wamenunua nyumba ya pamoja Kupitia interview aliyoifanya na DuJour Magazine . Nick alikiri ya kuwa hakuwa kuwa kwenye mahusiano ya furaha kama aliyokuwa nayo sasa na Iggy Azalea Nick aliongeza kwamba Iggy...
Aliyekuwa mpeke wa Wizzy Khalipha Amber rose maarufu kama muva ametupia picha kwenye ukurasa wake wa instagram akionekana ameshikilia pesa kama anapiga simu na kuandika kuwa “tallking to my boyfriend on the phone #through love #the single life #masterbating is way too much fun and no you can’t have none” Muva anahatari ya kuwa mpweke katika mud a mrefu wa maisha yake ...
KATIKA kuelekea kusherehekea siku ya Usafi wa Mazingira Duniani wakazi wa Manispaa ya Morogoro wametakiwa kujenga vyoo bora ili kujikinga na magonjwa mbalimbali yatokanayo na uchafu Hayo yamebainishwa na Afisa wa Manispaa ya Morogoro GABRIEL MALISA wakati akizungumza na Efm mjini Morogoro. MALISA amebainisha kuwa katika kuelekea kusherehekea siku ya Usafi wa Mazingira duniani ni wajibu wa kila mwanachama hususani mkazi wa Morogoro na vitongoji vyake kuhakikisha suala la usafi linakuwa ni endelevu sanjari na kuhakikisha kila mwananchi anajenga...
WAFUGAJI wa Jamii ya kimasai wametakiwa kufuata taratibu za kupata ardhi kihalali ,badala ya kuendelea kuvamia maeneo ya hifadhi yaliyopo kisheria. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu CHIKU GALAWA ambapo ameeleza uvamizi huo umekuwa kero pindi wanapotakiwa kuondoka kwenye maeneo hayo. Amebainisha kuwa kwa kufuata taratibu itasaidia kuepusha migogoro isiyokuwa na tija ambayo imekuwa ikirudisha nyuma...
AFISA wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mapambano dhidI ya maradhi ya Ebola, ameionya jumuiya ya kimataifa isilegeze kamba katika harakati za kuyatokomeza maradhi hayo hatari. Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf mjni Monrovia, afisa huyo Anthony Banburry amesema ingawa zipo dalili za kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo, kila mtu anapaswa kuendelea kuwa makini. Banburry amesema Umoja wa Mataifa umejenga vituo vya kupambana na Ebola, na inahitaji watu wa kujitolea kuviendesha vituo hivyo. Wakati...
MAREKANI imesema itapeleka rasimu ya maazimio ndani ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo dhidi ya Watu wanaozorotesha hali ya kisiasa nchini Sudani Kusini. Rais wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia amesema baadhi ya wanachama wa baraza hilo wanaunga mkono hatua ya kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara ya silaha. Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa. Lakini Mapigano yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za kimataifa kuhakikisha makubaliano ya...