WANASAYANSI nchini Brazil wamesema kuwa virusi vya ZIKA ambavyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wakiwa na vichwa vidogo huenda ni hatari zaidi kuliko ilivyofikiriwa awali. Madaktari bingwa wamesema kuwa virusi vya Zika vinaweza kuwa sababu ya kutokea kwa matatizo ya neva za fahamu kwa mwanamke mmoja mjamzito kati ya watano wanaoathiriwa na Virusi hivyo. Madaktari wengi na watafiti kwa sasa wanakubali kuwa kuna uhusiano kati ya mbu anayeeneza virusi na tatizo la watoto kuzaliwa na dosari kwenye...
MKURUGENZI wa CIA John Brennan amesema kwa miaka mitano iliyopita Marekani imeharibu kwa kiasi kikubwa kundi la Al Qaed baada ya kuuawa kwa kiongozi wake mkuu Osama bin Laden kutokana na uvamizi wa vikosi maalum nchini Pakistan. Brennan amesema kuwa Bin Laden alikuwa nembo na mwenye mikakati imara na muhimu na ilikuwa lazima kumuondoa mtu huyo ambaye amehusika katika mashambulizi ya kigaidi mjini Washington na New York Septemba 11. Mkuu huyo wa CIA ameongeza kuwa kumuondoa kiongozi wa IS Abu Bakr Al-Baghdadi...
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao. Waziri, Mwalimu ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka wizara hiyo Dkt Mohamed Mohamed alipomwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za...
TANZANIA leo inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza Mei tatu. Katika maadhimisho ya Mwaka huu kubwa linalohimizwa na wadau wa Habari nchini ni kuitaka Serikali kuharakisha kupitisha Sheria ya Vymbo vya Habari kwa kuzingatia maoni yanayotokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali. Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaenda sambamba na matukio muhimu matatu ya kihistoria ya kuadhimisha miaka 250 ya Sheria ya kwanza ya uhuru wa Habari...
Shabiki mmoja wa timu ya Leicester amesema kuwa ana uhakika klabu hiyo itashinda ubingwa wa ligi na kumfanya kupata zaidi ya pauni 20,000 ambayo ni sawa na milioni 64 za Tanzania. Leigh Herbert aliwekeza 5000 baada ya kupata vinywaji kadhaa wakati wa likizo huko Newquay ,Cornwall mwaka uliopita. Nina furaha tele kwa sababu nina uhakika wa asilimia 100 kwamba hilo litafanyika. Leigh aliweka fedha alicheza kamari hiyo kufuatia uteuzi wa mkufunzi Claudio Ranieri.Nilifikiria kwamba atailetea kilabu hiyo kitu maalum. Nilijua...
Beki wa Liverpool Mamadou Sakho amepewa marufuku ya siku 30 na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya kuanzisha harakati za kumuadhibu baada ya kuaptikana ametumia dawa za kusisimua misuli. Marufuku hiyo ni ya mda hadi pale uamuzi wa mwisho utakapoafikiwa na kitengo cha maadili cha shirikisho hilo. Sakho mwenye umri wa miaka 26 alipatikana ametumia dawa za kusisimua misuli kufuatia ushindi wa mechi ya taji la Europa dhidi ya Manchester United mnamo tarehe 27 mwezi Machi. Aliamua kutopinga...
RAIA wa Marekani amefungwa jela miaka 10 na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti. Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana. Kim alifikishwa kwa wanahabari mjini Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi...
GWIJI wa Soka la Kimataifa wa Liberia George Weah ametangaza rasmi kuwa atawania nafasi ya urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili. Weah, ambaye aliwahi kuchezea klabu za PSG, AC Milan, Chelsea, na Monaco amebainisha kwamba amekuwa na malengo ya kuliletea Taifa hilo mabadiliko, tangu alipoanza kujihusisha na masuala ya kisiasa mara tu baada ya kurejea Liberia mwaka 2003. Rais wa Sasa Johnson Sirleaf anamaliza awamu yake ya pili na ya mwisho katika utawala wake mwaka 2017 ambapo kwa mujibu...
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetakiwa kurekebisha mtaala wa kutoa mafunzo ya ukunga ili kuifanya taaluma hiyo iweze kuheshimika na kunusuru maisha ya watoto na akina mama wakati wa kujifungua. Wito huo umetolewa na Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA-Dokta. Sebalda Leshabari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Semina maalumu iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema Wizara hiyo inatakiwa kuangalia namana ya kurekebisha mitaala ya utoaji wa mafunzo ya ukunga...
MJUMBE wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Staffan de Mistura amezitaka Urusi na Marekani kuimarisha usitishaji tete wa mapigano nchini Syria kabla ya mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza miaka 5 ya mzozo nchini humo. Kauli hiyo ya de Mistura inakuja muda mfupi baada ya kulifahamisha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mazungumzo ya amani, ambayo amesema yamepiga hatua licha ya vikwazo vya hivi ...
MAMIA ya watu wamekusanyika nje ya uwanja wa ndege wa Kinshasa kuupokea mwili wa mwanamuziki Papa Wemba uliowasili nchini humo kutoka Abidjan. Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho. Maafisa wa serikali na wanadiplomasia watahudhuria ibada ya kumkumbuka mwanamuziki huyo katika uwanja wa ndege kabla ya mwili huo kupelekwa katika chumba cha...