Slider

SHULE YA SEKONDARI KIMANI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI SAFI NA SALAMA
Local News

SHULE ya sekondari Kimani iliyopo  kisarawe  mkoani Pwani inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa maji safi na salama  kutokana  na kuchangia kunywa maji  na wanyama  katika kisima kilichpo shuleni hapo. Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule  Nazarius Hongoa wakati alipokuwa akizungumza katika mahafali ya tatu  ya kidato cha nne  yaliyofanyika shuleni hapo ambapo amesema kuwa  wapo hatarini kukubwa na maradhi kutokana na maji kutokuwa...

Like
524
0
Monday, 30 November 2015
SHEIKH PONDA AACHIWA HURU
Local News

BAADA ya kukaa zaidi ya miaka miwili mahabusu hatimaye mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa morogoro leo imemwachia huru katibu wa taasisi na jumuiya za kiislamu Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda baada ya kuonekana hana hatia kwa makosa yaliyokuwa yakimkabili.   Hukumu hiyo imesomwa na hakimu wa mahakama hiyo bi Mary Moyo amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa pande zote mbili yaani upande wa mashitaka na upande wa mshitakiwa mahakama imemuona mtuhumiwa hana hatia na kumwachia huru kutokana na kifungu...

Like
209
0
Monday, 30 November 2015
ICC YAKUBALI OMBI LA KENYA
Global News

KAMATI maalum ya muungano wa nchi zilizotia saini mkataba wa Roma wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ya ICC, yenye wanachama 18 imelikubali ombi la Kenya la kukiondoa kifungu cha sheria ya 68 ya mahakama hiyo katika kesi inayomkabili Makamu wa rais wa nchi hiyo, William Ruto.   Hayo yamefikiwa baada ya hapo jana Kenya kusema iko tayari kujiondoa katika Mahakama ya ICC, iwapo haitapata hakikisho kuhusu namna kesi dhidi ya Ruto itakavyoendeshwa.  ...

Like
154
0
Friday, 27 November 2015
PAPA FRANCIS AZURU KITONGOJI CHA WATU MASIKINI KENYA
Global News

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Francis leo asubuhi amezuru katika maeneo wanakaoishi watu maskini katika kitongoji cha Kangemi, Nairobi, ambapo ametoa kauli kali dhidi ya matajiri wachache wanaowatenga maskini wenye shida.   Amewakosoa matajiri hao kwa kuhodhi mali ambazo zingewasaidia maskini.   Akizungumza katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi, Papa Francis amesema amezuru kwenye eneo linalokaliwa na watu wapatao 100,000, ili kuonyesha mshikamano kwao akiwataka wafahamu kwamba hayuko tofauti nao katika...

Like
247
0
Friday, 27 November 2015
MSD KUFUNGUA DUKA KUBWA LA KISASA MUHIMBILI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS
Local News

SIKU chache baada ya Rais Dokta John Magufuli kuiagiza bohari ya dawa nchini-Msd-kufungua maduka ya dawa kwenye Hospitali za kanda na Taifa,  tayari agizo hilo limeanza kufanyiwa kazi ambapo bohari hiyo wiki ijayo inatarajia kufungua duka kubwa la kisasa ndani ya hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu amesema tayari maandalizi ya kufungua duka hilo yamekamilika nalinatarajia kufunguliwa wiki ijayo huku akibainisha kuwa litatumia mfumo maalum wa kielektroniki ili kuhakikisha dhima ya kuwezesha upatikanaji wa dawa...

Like
289
0
Friday, 27 November 2015
WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARI YA DARESALAAM
Local News

WAZIRI MKUU mheshimiwa Majaliwa Kasim Majaliwa awasimamisha kazi kamishna wa kodi Tiagi Masamaki na Habibu Mpozya kitengo cha huduma kwa wateja kutokana ubadhilifu wa fedha kwa makontena zaidi ya 300 yaliyopotea. Waziri Mkuu pia  ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania –TRA,  na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushutukiza Bandarini hapo  leo. Maafisa hao wametakiwa pia kusalimisha pia hati zao za...

Like
1006
0
Friday, 27 November 2015
URUSI KUSHIRIKIANA KUPAMBANA NA IS
Global News

URUSI imesema iko tayari kushirikiana katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State.   Rais Vladmir Putin amemwambia mwezie wa Ufaransa Francois Hollande, kuwa shambulio dhidi ya ndege ya abiria ya Urusi na lile lililotokea mjini Paris, ambayo yote kundi la Islamic State limekiri kuhusika, kumefanya nchi hizo kuungana dhidi ya adui wao huyo.   Rais huyo wa Ufaransa yupo nchini Urusi kama sehemu ya kujaribu kutafuta muungano kuweza kuwadhibiti wapiganaji wa Islamic state nchini...

Like
180
0
Friday, 27 November 2015
HOFU YA UMMA JUU YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA YAPUNGUA
Global News

HOFU ya umma kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa imepungua katika kipindi cha miaka sita iliyopita. Kura ya maoni ya kimataifa inaonyesha kuwa hofu hiyo imepungua hasa katika nchi zilizostawi kiviwanda. Ni nchi nne pekee ambazo ni – Canada, Ufaransa , Uhispania na Uingereza ambazo kwa sasa raia wake wanaunga mkono serikali zao kuweka malengo katika mkutano wa dunia wa mazingira utakaofanyika wiki ijayo mjini Paris...

Like
180
0
Friday, 27 November 2015
VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KUWA NA MADAWATI YA HABARI ZA MAHAKAMA
Local News

VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuwa na madawati ya habari za Mahakamani, ili kuboresha uandishi wa habari hizo.   Hayo yamebainishwa na Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Shaaban Lila alipokuwa akizungumza na wanahabari wakati wa kufunga semina ya mafunzo ya uandishi wa habari za mahakamani ambapo amesema  pindi mtuhumiwa anapopandishwa  kizimbani  vifungu vya sheria ndivyo vinavyotumika kwa kuzingatia aina ya makosa ya mtuhumiwa.   Amewataka wanahabari kutoa taarifa kwa kuzingatia hukumu iliyotolewa badala ya wao kuhukumu...

Like
200
0
Friday, 27 November 2015
ASKOFU MKUU TABORA KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE ZIARA YA PAPA FRANCIS UGANDA
Local News

ASKOFU MKUU wa jimbo kuu la Tabora Mhashamu Paulo Ruzoka anaongoza ujumbe wa Tanzania kwenye ziara ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Francis nchini Uganda leo.   Papa Francis anatarajia kuwasili nchini Uganda leo kwa ziara ya siku mbili akitokea Kenya kabla ya kuelekea Afrika ya Kati.   Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania–TEC, Padre Raymond Saba amesema  Mabaraza ya Maaskofu ya Kenya na Uganda kwa pamoja yalitoa mwaliko kwa TEC kushiriki katika ziara ya Baba Mtakatifu...

Like
309
0
Friday, 27 November 2015
MASWALI NA MAJIBU YA MATONYA KWENYE KABALI
Entertanment

kuhusu kuandikiwa ngoma na Tunda Matonya:  Tunda ni mdogo wangu nimemfundisha muziki Kuhusu ulevi wa kupindukia Matonya: Mimi ni mlevi ila sio wa kutupwa na kwa sasa nimeacha baada ya kusemwa sana na mama yangu pamoja na watu wangu wa karibu. Kuhusu kufulia kimaisha Matonya: Mungu ni mwema Ghorofa moja gari tano maneno ya mtaani acha yapite Kuhusu kulelewa na Jimama: Matonya: anaenilea ni mama yangu mzazi hao wa mjini hawana nafasi kwangu Kuhusu kusafirisha unga nje Ndio sembe napeleka...

Like
330
0
Friday, 27 November 2015