TAASISI ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-MISA-kwa kushirikiana na Taasisi binafsi ya Friedrich Ebert Stiftung jana imezindua rasmi ripoti maalum ya kuangalia hali ya Vyombo vya habari ilivyo nchini kwa kuangazia masuala muhumu ya kiutafiti kwa nia ya kupima mwenendo na hali ya vyombo vya habari. Ripoti hiyo imelenga kutoa uchambuzi wa hali halisi ya namna Vyombo vya Habari nchini vinavyofanya kazi zake kwa uhuru na kwa kuzingatia sera, sheria na kanuni za uendeshaji wa vyombo hivyo. Akizungumzia...
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea jina la Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya Tano ambaye ni mheshimiwa KASSIM MAJALIWA Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi-CCM. Akitangaza jina hilo Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai amewaeleza wabunge kuwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais Mamlaka ya kuteua jina la Waziri Mkuu na kuliwasilisha bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa na wabunge. Kabla ya kutajwa kwa jina lake...
RAIS Barack Obama wa Marekani ameshambulia kile alichokieleza kuwa ni hofu ya kupita kiasi juu ya kitisho cha usalama kinachosababishwa na wakimbizi kutoka Syria. Katika hatua isiyokuwa ya kawaida Rais Obama amewashutumu wapinzani wake kisiasa, kwa kuwaweka wajane na yatima katika kundi la wahalifu. Hata hivyo Kupatikana kwa hati ya kusafiria ya Syria karibu na mwili wa mshambuliaji katika mashambulizi ya mjini Paris kumezusha hofu miongoni mwa wabunge wa Marekani na magavana kwamba ...
RAIS wa Nigeria Muhammadu Buhari ameagiza kukamatwa kwa Afisa mmoja mkuu serikalini kwa tuhuma za kuiba zaidi ya dola bilioni 2 zilizotengwa kwaajili ya vita dhidi ya kundi la Boko Haram. Kanali Sambo Dasuki ambaye alikuwa mshauri wa kitaifa kuhusu masuala ya usalama kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan, ameshtakiwa kwa kutoa kandarasi bandia za kununua helikopta 12, ndege 4 za kijeshi na silaha mbalimbali. Msemaji wa rais Buhari amesema kwamba ufisadi huo ulisababisha vifo vya maelfu ya...
KATIKA kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Afya kwa bei nafuu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii-PSPF-pamoja na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya-NHIF-wamesaini mkataba wa kutoa huduma hizo kwa wanachama waliojiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari wa PSP. Akizungumza na Wadau mbalimbali wa Afya Jijini Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando amesema kuwa wanachama hao watachangia kiasi cha shilingi Elfu 76 na 800 kwa mwaka ambapo wataweza kupata huduma bora za afya katika...
MABADILIKO ya Tabia Nchi, uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito mbalimbali na uchepushaji wa maji kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ni chanzo cha kukauka kwa mabwawa ya maji yanayotumika katika kuzalisha umeme. Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa wezi wa umeme nchini. Akizungumzia hali ya umeme nchini, Badra amesema kuwa kwa sasa hakuna mgawo...
SHIRIKA la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International, limesema uzio wa mipakani na udhibiti mwingine unaofanywa na mataifa ya Umoja wa Ulaya vinachochea ukiukwaji wa haki za binaadamu. Mkurugenzi wa shirika hilo barani Ulaya na Asia ya Kati John Dalhuisen, amesema kutanua uzio katika mipaka ya Ulaya kumechochea changamoto za kudhibiti wimbi la wakimbizi kwa njia za kistaarabu, na utaratibu mzuri. Ripoti hiyo imeangalia athari zinazosababishwa na uzio mpya, hasa katika mpaka wa Hungary na Serbia na wajibu...
LIMETOKEA tukio la ufyatulianaji mkali wa risasi kaskazini mwa Paris katika mtaa wa Saint Denis huku ripoti zikisema kuwa operesheni ya polisi kuhusiana na mashambulio ya Ijumaa inaendelea. Shirika la habari la AFP limeeleza kuwa Abaaoud Abdelhamid, anayedaiwa kupanga mashambulio hayo, ndiye aliyekuwa akisakwa kwenye operesheni hiyo mtaa wa Saint Denis. Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia tukio hilo wakisema kuwa milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri kwa saa za...
WANAWAKE wajawazito nchini wameshauriwa kufuata kanuni bora za Afya ikiwemo kuhudhuria Hospitalini mara kwa mara ili waweze kuepuka kujifungua watoto njiti. Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya watoto waliozaliwa kabla ya miezi 9, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick amesema kuwa endapo wanawake watatimiza lengo la kuhudhuria Hospitalini na kufuata ushauri wanaoupata kutoka kwa madaktari kuna uwekano wa tatizo hilo kupungua. Aidha, Sadick amewataka wanaume kutoa ushirikiano wa kutosha...
BUNGE la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeendelea leo kwa kikao cha pili kinachoenda sambamba na zoezi la Kiapo cha Uaminifu kwa wabunge wote. Hiyo imekuja baada ya jana Bunge hilo kufanikiwa kumpata Spika Mheshimiwa Jobu Ndugai atakayeliongoza kwa kipindi cha miaka mitano. Mheshimiwa Ndugai alishinda nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya Kura 254 kati ya 365 zilizopigwa na wabunge wote ambayo ni sawa na asilimia...
POLISI nchini Ufaransa wameendelea na msako dhidi ya kundi la wajihadi wanaoshukiwa kusababisha mauaji yaliyotokea mjini Paris Ijumaa ya wiki iliyopita. Tayari Polisi hao wameshavamia makao zaidi ya100 huku wakiwaweka washukiwa katika kifungo cha nyumbani wakiongozwa na mshukiwa mkuu Salah Abdeslam, mwenye umri wa miaka 26. Wakati hayo yakijiri, ndege za kivita za Ufaransa zimetekeleza mashambulio mapya na makali zaidi dhidi ya ngome ya Islamic State nchini...