Slider

MAREKANI YAIONDOLEA LIBERIA VIKWAZO VYA KIUCHUMI
Global News

MAREKANI imeiondolea Liberia vikwazo vya kiuchumi huku Rais Barack Obama akiipongeza nchi hiyo kwa kujitolea kufanikisha demokrasia tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2003. Vikwazo hivyo viliwekwa miaka 11 iliyopita dhidi ya kiongozi wa wakati huo Charles Talyor ambaye kwa sasa yupo gerezani kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, Rais Obama amesema kwa kuwa utawala wa Taylor ulimalizika na tayari kwa sasa yupo gerezani ina maana kwamba vikwazo hivyo havihitajiki...

Like
179
0
Friday, 13 November 2015
IDADI YA WAZAZI WANAOTUPA WATOTO YAPUNGUA
Local News

IMEELEZWA kuwa idadi ya wazazi ambao hutupa watoto wao imepungua kwa kasi tofauti na elimu ambayo hutolewa na serikali, jeshi la polisi pamoja na wadau mbalimbali wa haki za watoto juu ya kuwatunza watoto. Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa IRINGA–ACP- RAMADHAN MUNGI wakati akizungumza na wadau mbalimbali juu ya suala hilo na kuwaonya wazazi wenye tabia ya kutupa watoto mara baada ya kujigungua kuacha haraka kwani kufanya hivvo, ni kwenda kinyume na sheria za haki za binadamu....

Like
290
0
Friday, 13 November 2015
ANGLO GOLD ASHANTI YAJITOLEA KUWEZESHA MATIBABU YA UGONJWA WA MIDOMO SUNGURA KANDA YA ZIWA
Local News

KAMPUNI ya uchimbaji Madini ya Anglo Gold Ashanti imejitolea kuwezesha huduma za matibabu ya Ugonjwa wa Midomo sungura Katika kanda ya ziwa matibabu yanayotarajia kufanyika katika hospitali ya Rufaa ya Sokoe Toure jijini Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango huo Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo Tenga Tenga amesema miongoni mwa majukumu ya kampuni hiyo ni pamoja na kusaidia jamii kujikwamua na matatizo mbalimbali na kuwataka wananchi wanaosumbuliwa na ugonjwa huo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kupata...

Like
304
0
Friday, 13 November 2015
ZIMBABWE: MSHINDI WA MASHINDANO YA UBAYA KUKUTANA NA UPINZANI MKUBWA
Entertanment

Muandaaji wa mashindano ya Ubaya nchini Zimbabwe maarufu kama Mr Zimbawe bwana David Machowa amesema kwa mara ya kwanza mshindi wa muda wote wa mashindano hayo bwana William Masvinu anatarajiwa kukutana na upinzani mkali kufuatia kuongezeka kwa idadi ya washiriki. Tangu mwaka 2012 Masvinu amekuwa akitwaa taji hilo ambapo idadi ya washiriki walikuwa watano na alifanikiwa kubeba $100 na nafasi ya kulala katika moja ya hoteli za Harare akiwa amelipiwa kila kitu. Waandaji wa mashindano hayo wameongeza kitita cha fedha...

Like
657
0
Friday, 13 November 2015
AFRIKA NA ULAYA ZAKUBALIANA KUPUNGUZA IDADI YA WAHAMIAJI
Global News

VIONGOZI wa Muungano wa Ulaya na Afrika wametia saini makubaliano yanayotarajia kupunguza idadi ya wahamiaji wanaofunga safari hatari ya kutaka kufika Ulaya. Wakizungumza kwenye mkutano huo viongozi hao wameidhinisha kuundwa kwa hazina ya dola bilioni 1.9 bilioni za kusaidia mataifa ya Afrika katika suala la kukabiliana na wakimbizi. Miongoni mwa mataifa yatakayonufaika kutokana na hazina hiyo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Djibouti, Somalia, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia....

Like
291
0
Thursday, 12 November 2015
UN YATAFAKARI KUTUMA VIKOSI BURUNDI
Global News

UMOJA wa Mataifa unatafakari wazo la kutuma walinda Amani nchini Burundi iwapo machafuko nchini humo yatazidi kuendelea. Watu zaidi ya 200 tayari wameuawa huku maelfu ya wengine wakihama makazi yao tangu Aprili, mara baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu. Muungano wa Afrika tayari umekitaka kikosi cha polisi wa akiba cha kanda ya Afrika Mashariki kuwa tayari kutumwa Burundi iwapo hali ya Amani itakuwa mbaya...

Like
184
0
Thursday, 12 November 2015
WAFANYAKAZI URAFIKI WAGOMA KUSHINIKIZA NYONGEZA YA MISHAHARA
Local News

WAFANYA KAZI wa kiwanda cha nguo cha urafiki kilichopo mabibo Jijini Dar es salaam leo wamegoma kufanyakazi kwa kushinikiza uongozi wa kiwanda hicho kuwaongezea mishahara yao pamoja na kulipwa malimbikizo mengine wanayodai.   Wakizungumza na Efm wafanyakazi hao wamesema kuwa mishahara wanayo lipwa ni kidogo sanjari na makato mengine kwenye mishahara yao ikiwemo bima ya Afya ingawa Awali walishafungua kesi mahakama kuu ya rufaa ili waweze kulipwa madeni yao lakini bado hawajalipwa hadi sasa. Kwa upande wake Naibu meneja mkuu...

Like
334
0
Thursday, 12 November 2015
PROF. MSERU ATAMBULISHWA RASMI KUWA MKURUGENZI WA BODI YA HOSPITALI YA MUHIMBILI
Local News

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili leo imempokea na kumtambulisha rasmi mkurugenzi mpya wa bodi ya hospitali hiyo Profesa Lawrence Mseru kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli kuivunja bodi iliyokuwa ikiongozwa na mkurugenzi dokta Hussein Kidanto siku chache zilizopita.   Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Salam Afisa uhusino wa hospitali hiyo dokta Amnieli Eligisha amesema kuwa tayari mkurugenzi huyo ameanza kazi ya kuhakikisha ana boresha huduma ya matibabu ikiwemo kufanyia matengenezo mashine...

Like
686
0
Thursday, 12 November 2015
RIADHA: PUTIN AAGIZA MADAI YA DAWA YAFANYIWE UCHUNGUZI
Slider

RAIS wa Urusi Vladimir Putin ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusiana na madai kwamba wanariadha nchini humo wamekuwa wakitumia dawa za kusisimua misuli. Rais Putin ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa mara ya kwanza tangu tume huru ya shirika la kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli duniani (Wada) kutoa ripoti yake Jumatatu juu ya matumizi ya dawa hizo nchini Urusi. Kwa upande wake Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko amesema kuwa ingawa wao wanachangamoto ya kimfumo lakini mfumo wa kukabiliana...

Like
229
0
Thursday, 12 November 2015
JESHI LA KENYA LATUHUMIWA KUFANYA BIASHARA SOMALIA
Global News

JESHI la Kenya limetuhumiwa kujihusisha na shughuli mbalimbali kinyume na malengo ikiwemo kufanya biashara badala ya kufanya kazi zinazowahusu nchini Somalia. Taasisi ya Waandishi wa habari Wanaopigania haki imelituhumu Jeshi hilo kujiingiza katika masuala mbalimbali ya kibiashara yanayowaletea faida na kuacha kazi ya iliyowapeleka ya kulinda Amani. Hata hivyo Taasisi hiyo imewalaumu baadhi ya maofisa wa jeshi hilo kushirikiana katika biashara haramu na wapiganaji wa Al Shabaab jambo ambalo ni kinyume cha...

Like
285
0
Thursday, 12 November 2015
TARIME: WANANCHI WAMTAKA DIWANI KUTEKELEZA AHADI ZAKE
Local News

WANANCHI wa kata ya Turwa wilayani Tarime Mkoani Mara wamemtaka diwani wao kutekeleza ahadi alizo ahidi wakati wa kampeni zake  ikiwemo kutatua tatizo la ukosefu wa maji safi na salama. Wakizungumza na Efm wakazi hao wamemtaka kiongozi huyo atakapoanza kutekeleza majuku yake aanze na matatizo yaliyopo kwenye kata hiyo yanayowakabili kwa muda mrefu. Kwa upande wake kiongozi Mteule ambaye ni diwani wa kata hiyo Zakayo Wangwe amesema kuwa atahakikisha anawatumikia wananchi ipasavyo kwa lengo la kuleta maendeleo ya...

Like
323
0
Thursday, 12 November 2015