CHAMA cha kihafidhina nchini Poland cha sheria na haki PiS kimeshinda uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa jana jumatatu. Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi zinasema kuwa Chama cha PiS kilipata asilimia 37.6 ya kura, huku chama cha Civic Platform PO kimeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 24.1. Mgawanyiko rasmi wa viti bungeni ulikuwa bado haujapatikana, lakini wadadisi wanasema matokeo huenda yakatoa kwa ...
KUFUATIA uwepo wa mitazamo tofauti kwa tume ya Taifa ya uchaguzi kuhusu kupendelea upande mmoja wakati wa utangazaji wa matokeo, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema Tume inafanya kazi zake kwa mujibu wa utaratibu iliyojiwekea na sio kwa matakwa ya mtu binafsi. Aidha Jaji mstaafu Lubuva amesema kuwa matokeo ya ngazi ya urais kutoka majimbo ya uchaguzi kote nchni hutangazwa kwa wananchi kwa kadiri yanavyo pokelewa na sio vinginevyo. Hata hivyo amesema kuwa hali hiyo imesababishwa na ucheleweshwaji...
WAANGALIZI wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC leo wametoa ripoti ya awali kuhusu Zoezi la uchaguzi linavyoendelea tangu kuanza kwa zoezi hilo la uchaguzi na kusema kuwa zoezi hilo limemalizika vizuri katika maeneo mengi ya nchi. Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam Kiongozi wa Timu ya Waangalizi kutoka EAC Mheshimiwa Arthur Moody Awori amesema kuwa kwa mara ya kwanza uchaguzi wa mwaka huu umekuwa wa ushindani mkubwa uliobebwa na mabishano bila ya kuwepo na vurugu zozote. Aidha...
PAKUA MATOKE HAPA 1445940504-MATOKEO RASMI YA WAGOMBEA URAIS TANZANIA MAJIMBO...
Makundi ya uokoaji yanaendelea na juhudi za kuyafikia maeneo ya Kaskazini mwa Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan, ili kuwaokoa watu wanodhaniwa kuwa wameathirika na tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo hilo jana. Hadi sasa imeelezwa kuwa zaidi ya watu 260 wamefariki, kutokana na tetemeko hilo ambalo halijawahi kutokea tangu kipindi cha muongo mmoja uliopita. Hata hivyo baadhi ya maeneo yaliyoathirika zaidi nchini Afghanistan, yanadhibitiwa na wanamgambo wa Taliban, na kusababisha hali kuwa ngumu ya...
WAZIRI wa ulinzi wa Ujerumani Ursula von der Leyen anatarajiwa kukutana na waziri mwenzake wa Iraq kutafuta njia za kurekebisha hali inayosababisha watu kuikimbia nchi hiyo. Akiwa mjini Baghad waziri huyo anatarajiwa kukutana na Waziri Mkuu Haider al Abadi na waziri wa ulinzi Khaled al Obeidi kwaajili ya mazungumzo hayo. Akizungumza jana usiku kabla ya kuanza ziara yake hiyo von der Leyen amehimiza kuwepo kwa umoja ndani ya serikali ya Iraq na kuongeza kwamba maslahi ya Ujerumani katika eneo hilo...
ASASI isiyo ya kiserikali ya AGENDA imetoa wito kwa serikali na wadau wengine kuelimisha jamii juu ya madhara ya madini ya risasi na jinsi ya kuyaepuka kwani yanaathari kubwa kwa watoto na mama wajawazito. Akizungumza na waandfishi wa habari jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa Asasi hiyo Silvani Mng’anya amesema kuwa katika wiki ya kukuza uelewa kwa jamii kuhusu athari za madini ya risasi wananchi wanatakiwa kujua kuwa madini hayo yanaathiri mfumo wa mwili wa binadamu ikiwemo ubongo, moyo...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC-imeendelea kutoa matokeo kwa ngazi ya Urais kutoka majimbo mbalimbali yaliyokamilisha Zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa katika Uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka huu. Awali akizungumza kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amewataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani Tume imejipanga vyema kuhakikisha kila matokeo yanayopatikana inayatangaza. Leo ni siku ya pili tangu kukamilika kwa Zoezi la...
Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameshtakiwa na chama cha mpira wa miguu FA kwa utovu wa nidhamu. Mourinho ameshitakiwa na Chama hicho cha mpira kutokana na lugha pamoja na tabia kwa ujumla kwenye mchezo kati ya Chelsea na West Ham United ambapo upande wake ulipokea kichapo. Mourinho alisimamishwa baada ya kumfuata mwamuzi Jon Moss kwenye chumba chake wakati wa mapumziko siku jumamosi. Klabu zote mbili zimeshitakiwa kwa kushindwa kuwaongoza wachezaji wao na kutakiwa kutoa majibu ifikapo October 29...
katibu Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya Gianni Infantino ameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. Infantino alijumuika kwenye orodha ya wanaowania nafasi hiyo saa chache kabla ya siku ya mwisho ya kupokea maombi ambayo ni jumatatu Maamuzi haya ya Infantino kuungana Michel Platini kwenye maombi hayo ili kuweza kuchukua nafasi ya Sepp Blatter, 79. Kunazidi kuongeza kasi ya matarajio ya kuwa na mchuano mkali. Rais wa shirikisho la mpira...
WANAMGAMBO wanne wanaotuhumiwa kuwa wa kundi la Dola la Kiislamu wameuwawa leo pamoja na polisi wawili wa Uturuki katika mashambuliano ya risasi yaliyotokea katika mji wa Diyabakir kusini mashariki mwa Uturuki. Taarifa kutoka usalama zimesema kuwa polisi ilikuwa imefanya upekuzi kwenye nyumba kadhaa katika kitongoji cha mji huo ambapo inadhaniwa kwamba wapiganaji wa jihadi wamekuwa wakijificha na ndipo wanamgambo hao walipowafyatulia risasi polisi. Hata hivyo mapigano makali bado yalikuwa yakiendelea na kwamba polisi ina hofu kuwa wanamgambo...