KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ataliarifu baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo, kuhusu ziara yake ya Mashariki ya Kati, iliyolenga kutuliza ghasia zilizodumu kwa wiki kadhaa sasa. Ban Ki-Moon alitoa ombi la kuzungumza na baraza hilo haraka kupitia njia ya video, kutokea mji wa Ramallah, uliyoko katika Ukingo wa Magharibi wa Palestina. Katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alifanya ziara ya kustukiza katika eneo hilo jana, ili kutoa onyo kwa pande mbili...
MGOMBEA ubunge Jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi-CCM Fredrick Mwakalebela amesema endapo akipata ridhaa ya kuongoza Jimbo hilo atahakikisha anatenga ofisi maalamu kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya watu wenye ulemavu. Akizungumza katika kikao na chama cha walemavu mkoa wa Iringa Mwakalebela amesema kuwa atahakikisha kundi hilo maalumu linapewa kipaumbele katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya na...
CHUO cha elimu na mafunzo ya ufundi Stadi (VETA) kimekuwa miongoni mwa taasisi kumi bora za Afrika katika utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi. Afisa habari wa Chuo hicho, DORA TESHA amekiambia kituo hiki kuwa, tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na umoja wa Afrika (AU) kwashirikiana na mashirikia ya USAID na FHI 360 zilizoshirikisha taasisi zaidi ya arobaini kwa lengo la kutambua taasisi bora zinazotoa elimu ya mafunzo ya ufundi stadi katika Afrika. Amesema kuwa sababu ya kuanzishwa mchakato...
CHAMA cha upinzani nchini Canada cha Liberal kimeshinda uchaguzi mkuu na kufikisha kikomo uongozi wa karibu mwongo mmoja wa chama cha Conservative. Chama hicho kinachoegemea siasa za mrengo wa kati, chini ya uongozi wa Justin Trudeau, kilianza kampeni kikishikilia nafasi ya tatu kwa mujibu wa kura za maoni lakini sasa kimeongoza kwa kura. Trudeau, mwenye umri wa miaka 43, ambaye ni mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu Pierre Trudeau, amesema raia wa Canada walipigia kura mabadiliko halisi ambapo pia Waziri Mkuu...
Milipuko imesikika katika mji mkuu wa Congo, Brazzaville kufuatia maandamano makubwa yaliyoitishwa na vyama vya upinzani kupinga hatua ya rais aliyeko madarakani Denis Sassou Nguesso kutaka kubadilisha katiba ili kumruhusu kuwania muhula wa tatu. Vyama vya upinzani viliitisha maandamano hayo na inasemekana kuwa wanajaribu kuingia katikati mwa jiji hilo la Brazzaville. Serikali ilikuwa imepiga marufuku maandamano yoyote kabla ya kura ya maoni itakayoamua iwapo katiba ya taifa hilo itabadilishwa au...
KATIKA kuhakikisha jitihada za kuboresha Sekta ya elimu nchini zinaleta mafanikio, asasi ya utafiti ya -TWAWEZA-kupitia mradi wake wa uwezo imeendesha mafunzo ya siku mbili katika wilaya ya mwanga yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kufanya kazi za kujitolea vijana wapatao 60 ili waweze kufanya tathmini juu kwa watoto katika nyanja za kuhesabu pamoja na kusoma kiswahili na kingereza. Akizungumza na E-FM Mratibu wa Mradi huo George Madundo amesema mafunzo hayo yatachangia katika shughuli za ukusanyaji wa taarifa za kubaini...
JUMUIYA ya wanafunzi waliosoma shule ya sekondari ya Mtakatifu Joseph kwa wameungana na wanafunzi wa sasa wa shule hiyo kuichangia damu hospitali ya Taifa ya muhimbili ili kuwasaidia watanzania wenye mahitaji ya kuongezewa Damu. Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wanafunzi wa jumuiya hiyo Mariam Zialo ameeleza kuwa wamefanya zoezi hilo pamoja na wanafunzi wa sasa wa shule hiyo baada ya kuona uhitaji mkubwa wa damu uliokuwepo katika hospitali hiyo. Kwa upande mwingine mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka...
Mwanariadha mlemavu nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius ameruhusiwa kuondoka gerezani mwaka mmoja tu baada ya kufungwa jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp. Aliachiliwa huru Jumatatu usiku badala ya Jumanne kama wengi walivyotarajia. Baada ya kuachiliwa huru, alielekea kwa mjomba wake Arnold Pistorius. Pistorius ameruhusiwa kukamilisha kifungo chake cha miaka 5, akiwa nyumbani...
BUNGE la Libya linalotambulika na Jumuiya ya kimataifa limeyakataa mapendekezo ya Umoja wa Mataifa ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Mbali na hayo Baraza hilo la wawakilishi limesema kuwa litashiriki mazungumzo ya Amani ya Umoja wa Mataifa pamoja na mahasimu wao wanaoendesha serikali nyingine kutokea mji mkuu wa Tripoli. Hata hivyo Mataifa ya Magharibi yanazishinikiza pande mbili kuyaafiki makubaliano ya Umoja wa Mataifa, miaka minne tangu kuangushwa na kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa Taifa hilo Muammar Ghadhafi....
WATU wasiopungua Elfu 15 wameandamana katika mitaa ya mji wa Dresden jana jioni, kuadhimisha mwaka mmoja tangu yalipofanyika maandamano ya kwanza ya vuguvugu la PEGIDA. Kauli zilizokuwa zinatumiwa na miongoni mwa waandamanaji hao zilikuwa za hisia kali dhidi ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusiana na msimamo wake wa kuwaunga mkono wakimbizi. Polisi mjini Dresden imeripoti kuwa makabiliano kati ya waandamanaji wa PEGIDA ikimaanisha Wazalendo wa Ulaya dhidi ya Kusilimishwa kwa mataifa ya Magharibi,” walifanya maandamano yake ya...
WAFUGAJI nchini wanatarajia kuondokana na hasara ya vifo vya mifugo yao ikiwemo ng’ombe, baada ya kuzinduliwa dawa mpya ijulikanayo kwa jina la Vectoclor Plus, inayodhibiti magonjwa yanayoenezwa na Kupe. Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti wa wadudu na magonjwa yaenezayo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dokta Martin Ruheta, amesema uzinduzi huo umekuja wakati muafaka, kwani utapunguza vifo vya mifugo ambapo kila mwaka wanyama wanakufa kwa asilimia 70 kwa sababu ya magonjwa ya...