IGGY AZALEA NA BOYFRIEND WAKE NICK YOUNG KUTUMIKA KWENYE TANGAZO JIPYA
Entertanment

Mbali na drama za rapa huyu wa kike Iggy Azalea mwenye asili ya Australia bado ana kila sababu ya kutabasamu kufuatia headlines za mafanikio anazoziweka kwenye tasnia ya burudani. Hivi karibuni Iggy azale na mpenzi wake Nick Young wamepitishwa kutumika kwenye picha ya tangazo la kampeni ya Forever 21‘s holiday . Akiongea na watu mara baada ya kupiga picha hizo Nick Young ambae ni mchezaji wa mpira wa kikapu katika ligi ya Nba huko marekani ameelezea furaha yake kupiga picha hizo...

Like
240
0
Thursday, 23 October 2014
DIAMOND ASHIKILIWA NA POLISI!!!
Entertanment

Baada ya Meneja wa Diamond kushikiliwa na polisi kwa ajiri ya kufanyiwa mahojiano kuhusiana na swala la msanii huyo kutumia sare za jeshi kwenye tamsha wakati anafanya Show, Leo inasemekana pia Diamond anashikiliwa na polisi leo kwa mahojiano zaidi kufuatia tukio hilo katika kituo cha Oysterbay Bagdad amezungumza na msemaji wa jeshi ili kujua taratibu zitakazofuatwa kulingana na kosa husika, Hata hivyo msemaji huyo ameongeza ya kuwa sheria itachukua mkondo wake  ...

Like
492
0
Thursday, 23 October 2014
REAL MADRID YAICHAPA LIVERPOOL 3-0 HUKO ANFIELD
Slider

Katika ligi ya mabingwa barani Ulaya Liverpool imechabangwa nyumbani Anfield kwa mabao 3-0 kutoka kwa Real Madrid huku Mario Balotelli akiingia lawamani. Meneja wa mchezaji huyo mtukutu, Brendan Rodgers amemlaumu mshambuliaji huyo kwa kitendo chake cha kubadilishana Jezi na Pepe mara tu baada ya dakika 45 za kwanza. Baadhi ya mashabiki wa jijini Dar es Salaam,Tanzania wamemtupia lawama mchezaji huyo ambaye pamoja na kununuliwa kwa pauni milioni 16 ameifungia Liverpool goli moja tu msimu huu. Wakati huo huo Arsenal wamepata...

Like
814
0
Thursday, 23 October 2014
WATANZANIA WASHAURIWA KUTOTEGEMEA ZAIDI UGUNDUZI WA MAFUTA NA GESI
Local News

WATANZANIA wameshauriwa kutotegemea zaidi ugunduzi wa mafuta na gesi kuwa ndio njia pekee ya kutatua matatizo ya kiuchumi nchini. Akizungumza na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam kwenye kongamano la kufunga maonesho ya tatu ya mafuta na gesi asilia Naibu Waziri wa Nishati na Madini mheshimiwa STEVEN MASELE amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia fursa hiyo kama njia moja wapo ya kuinua vyanzo vingine vya uchumi  MASELE Aidha Mheshimiwa MASELE amebainisha kuwa Serikali imeandaa mkakati wa kufungua mfuko utakaotumika kuifadhi mapato...

Like
287
0
Thursday, 23 October 2014
KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MWANZA NA IRINGA
Local News

KAMATI ya Hesabu za Serikali za mitaa inatarajia kwenda kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kukagua mapato na matumizi katika Halmashauri za mikoa ya Mwanza na Iringa. Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo RAJAB MBARUK MOHAMED ambapo amesema Kamati itaondoka leo kwa kuwa ripoti ya CAG inaonyesha kuwa Mwanza ndiyo ilifanya vibaya zaidi kuliko zote…. Hata hivyo amesema, kuna fedha zaidi ya bilioni mia tatu zilizotolewa na wafadhiri kwa ajili ya Halmashauri hazikutumika. MOHAMED...

Like
282
0
Thursday, 23 October 2014
MAPENZI YA NICKI MINAJ NA SAFAREE SAMUELS YAVUNJIKA
Entertanment

Ikiwa ni siku kadhaa toka stori za Nicki Minaj na Safaree Samuels mahusiano yao kuyumba, hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kufuatia post zilizotumwa na wawili hao katika muda tofauti huku kila mmoja akiandika maneno yake   mahusiano ya wawili hawa yaliyodumu kwa miaka isyopungua kumi na nne (14) kwa sasa hayapo tena, na hii imekuja mara baada ya Safaree Samuels kuonekana amezificha tatoo za Nicki minaj kwenye mwili wake kwa kuchora tatoo nyinginge mpya kwa juu yake kama alivyowahi kufanya Nick...

Like
403
0
Wednesday, 22 October 2014
MCHEZAJI WA QPR ASEMA HANA UZANI MKUBWA
Slider

Mchezaji wa QPR Adel Taarabt amemjibu kocha wake Harry Redknapp aliyesema kuwa mchezaji huyo ana uzani mkubwa hivyobasi hafai kucheza. Redknapp alitoa madai hayo alipoulizwa ni kwa nini hakumjumuisha kiungo huyo wa kati katika kikosi kilichocheza mechi dhidi ya Liverpool waliposhindwa kwa mabao 3-2. Hata hivyo Taarabt alipokuwa akiongea na kituo cha habari cha Daily Mail alijitetea kwamba madai hayo si ya kweli. “Nilikuwa na tamaa kubwa ya kucheza kabla ya mechi kuanza. Nilikasirika sana niliponyimwa nafasi ya kucheza.”alisema...

Like
234
0
Wednesday, 22 October 2014
KUNA UWEZEKANO WA KURUDISHA CHENJI KWA MASHABIKI AFRIKA?
Slider

Wachezaji wa Sunderland wameamua kuwarudishia Mashabiki wao gharama walizotumia kuutizama mchezo ambao mwisho wa siku walipokea kichapo cha bao 8-0 kutoka kwa Southampton. Hicho kilikuwa kisago kikubwa kabisa kwa Sunderland katika miaka 32. Mashabiki wana nafasi ya kudai pesa yao mpaka kufikia tarehe 5 ya Novemba mwaka huu. Akizungumza kwa niaba ya wenzake, nahodha John O’Shea amesema, “Tunashinda na kushindwa kama timu, wachezaji, uongozi na mashabiki lakini tungependa kuwatambua na kuwashukuru mashabiki waliosafiri umbali mrefu kuja...

Like
296
0
Wednesday, 22 October 2014
WATANZANIA WAFUNGWA MIDOMO NA UMRI WA MISS TANZANIA
Entertanment

kufuatia tuhuma mbalimbali juu ya mshindi wa shindano la Miss Tanzania kwamba hakustahili kupata taji hilo na kuwepo kwa taarifa zenye kuchanganya kuhusu umri wa mlimbwende huyo Sitti Mtemvu, jana kamati ya Miss Tanzania ilifanya kikao ikiwa pamoja na kujadili na waandishi wa habari ili kuweka mambo sawa kwa kutoa vielelezo vyao. hata hivyo hali ya Sintofahamu bado imeendelea kuwepo kwenye baadhi ya vichwa vya watu kupitia mitandao ya kijamii na sehemu nyinginezo kufuatia baadhi ya majibu ya Mrembo huyo wakati akihojiwa...

Like
408
0
Wednesday, 22 October 2014
TANESCO PAMOJA NA REA WAPELEKA WATAALAMU WILAYA YA MKULANGA
Local News

SHIRIKA la umeme nchini Tanesco kwa kushirikiana na wakala wa umeme vijijini -REA- wamefanikiwa kupeleka wataalamu wakutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya umeme katika vijiji vyote vya wilaya ya mkuranga ikiwa ni utekelezaji wa ahadi waliyoitoa kupitia kwa naibu waziri wa fedha ADAMU MALIMA. Akizungumza na EFM Ofisini kwake jijini Dar es salaam meneja wa Tanesco kanda ya Pwani na Dar es salaam MAHENDE MUGAYA amesema kuwa wataalamu hao watatoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutumia...

Like
504
0
Wednesday, 22 October 2014
MCT YAZINDUA TUZO ZA UMAHIRI ZA UANDISHI WA HABARI
Global News

 BARAZA la habari nchini-MCT kwakushirikiana na Kamati ya maandalizi ya tuzo za Umahiri za uandishi wa habari Tanzania-EJAT, leo imezindua rasmi tuzo hizo ikiwa ni mara ya sita tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza na wandishi wa habari Jijini Dar es salaam, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya EJAT, Meneja udhibiti na viwango wa MCT, Pili Mtambalike amesema tuzo za mwaka huu zimeongezewa mambo mapya mawili nakufanya jumla ya makundi ya kushindaniwa kuwa 21 kutoka 19. PICHA NI BAADHI...

Like
438
0
Tuesday, 21 October 2014
« Previous PageNext Page »