VIKAO VYA KAMATI YA BUNGE VIMEENDELEA LEO JIJINI DAR
Local News

VIKAO vya kamati za Bunge vimeendelea leo jijini Dar es salaam ikiwa ni siku ya pili ambapo ripoti za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma zimewasilishwa zikifatiwa na taarifa ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2012-2013 Katika Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma-PAC. Akisoma Ripoti ya CAG, mbele ya mwenyekiti wa kamati hiyo Zitto Kabwe, Msaidizi Mkaguzi Mkuu Nestory Karia amesema ofisi yake imebaini mapungufu mengi ya fedha katika baadhi...

Like
378
0
Tuesday, 21 October 2014
KAULI YA UN KUHUSU MATUMIZI YA NGUVU KINGONO SUDANI KUSINI
Global News

UMOJA wa  Mataifa  umesema  ubakaji  na  njia  nyingine za matumizi  ya  nguvu yanafanywa  na  pande  zote katika  vita vya  wenyewe  kwa  wenyewe  nchini  Sudan  kusini. Mwakilishi maalumu  wa  Umoja  wa  Mataifa  kuhusu  matumizi  ya  nguvu kingono katika  mizozo  ya  kivita, Zainab Hawa  Bangura, amesema hali  hiyo  imesambaa  mno  ambapo  hadi  mtoto  wa  miaka  miwili alikuwa  miongoni  mwa  wahanga. Mapigano  yalizuka Desemba mwaka  jana  nchini  Sudan kusini baada  ya  miezi ya  hali  ya...

Like
297
0
Tuesday, 21 October 2014
OSCAR PISTORIUS AMEHUKUMIWA JELA MIAKA MITANO
Global News

MWANARIADHA wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia. Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo. Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka...

Like
326
0
Tuesday, 21 October 2014
MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA MAFUTA YA TOTAL YA UFARANSA AUAWA KWA AJALI YA NDEGE
Global News

KAMPUNI kubwa ya mafuta ya Ufaransa, Total imetangaza kwamba mkurugenzi wake mkuu, Christophe de Margerie ameuawa katika ajali ya ndege iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Moscow nchini Urusi. Taarifa zimeeleza kuwa ndege ya binafsi aliyokuwa akisafiria afisa huyo imeanguka kwenye uwanja wa nukovo ulio nje kidogo ya jiji la Moscow. Vyombo vya habari vya Urusi vimesema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria mmoja tu, pamoja na wahudumu watatu, wote wakiwa raia wa Ufaransa....

Like
393
0
Tuesday, 21 October 2014
RAIS WA NIGERIA AELEZEA MAFANIKIO NA NJIA WALIZOTUMIA KUONDOA EBOLA
Global News

RAIS wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema mafanikio ya nchi yake dhidi ya maradhi ya Ebola yametokana na imani ya wananchi wa kawaida kwa maagizo yaliyotolewa na serikali, kuwataka wabadili mienendo yao ya kila siku maishani kama vile kusalimiana kwa kupeana mikono, na utaratibu wa mazishi. Amesema serikali yake ilikuwa na wasiwasi kwamba makanisa yangekataa kuitikia wito huo katika suala la komunio ambapo watu wapatao 1,000 wanaweza kushiriki kikombe kimoja. Ameyasifu makanisa kwa kuusimamisha utaratibu huo, na hata ule wa kutakiana...

Like
254
0
Tuesday, 21 October 2014
JWTZ YATOA TAMKO KUHUSU VIKUNDI AMA MTU MMOJA MMOJA WANAOTUMIA SARE ZAO ISIKILIZE HAPA
Entertanment

baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond kufanya show akiwa na mavazi yanayosemekana kuwa ni sare ya Jeshi yeye na dancers wake, lakini pia kuonekana kwenye baadhi ya picha akiwa na mavazi hayo huku ameshika siraha na kuvuta sigara hii ndio kauli kutoka kwa msemaji wa jeshi akisema siruhusa kwa vikundi ama mtu mmoja mmoja kutumia sare hizo, pamoja na said Fella moja ya watu wanaomsimamia Diamond akieleza kuhusu mavazi hayo kupitia interview ya redio leo kwenye 411...

Like
1462
0
Tuesday, 21 October 2014
MSANII YP WA TMK WANAUME FAMILY HATUNAE TENA
Entertanment

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Yessaya Ambikile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo  Efm imezungumza na kaka wa marehemu na kuthibitisha hilo kwa kusema Yp alikuwa anasumbuliwa na kifua.. EFM inawapa pole wanafamilia na wapenzi wa msanii huyu alieitumikia sanaa ya muziki wa kizazi kipya, Bongo fleva katika kipindi cha uhai wake                                          ...

Like
1032
0
Tuesday, 21 October 2014
MCHEZAJI AFARIKI AKISHEREHEKEA BAO INDIA
Global News

Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake. Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC. Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki. Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo. Taarifa...

Like
276
0
Tuesday, 21 October 2014
IMANI POTOFU NI KIKWAZO KWENYE UTOAJI WA CHANJO
Local News

IMEELEZWA KUWA, Imani Potofu dhidi ya Chanjo za Surua na Rubella zinazoendelea kutolewa kote nchini, zimekuwa kikwazo katika kufanikisha kampeni hiyo yenye lengo la kupunguza ongezeko la magonjwa ya milipuko kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miaka 15. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Ilala RAYMOND MUSHI wakati wa uzinduzi wa chanjo ya Surua na Rubella… Naye Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, bwana REGINALD MENGI amesema hilo. Kwa upande wake mratibu wa chanjo mkoa wa Dar...

Like
383
0
Tuesday, 21 October 2014
SIMU ZA MIKONONI, VYOMBO VYA HABARI KUTUMIKA KUTOA TAARIFA ZA AFYA
Local News

CHAMA Cha Wataalam wa Habari za afya Afrika-AHILA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wameandaa mikakati ya kusambaza taarifa muhimu za afya kwa wananchi kwa kutumia mitandao ya habari ikiwemo simu za mikononi Akizungumza na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mkutano wa kumi na nne wa wataalam wa habari za afya Afrika, Makamu wa Rais Dokta AHMED BILALI amesema kuwa taarifa za afya kutoka kwa wataalam mbalimbali wa afya nchini zitawafikia wananchi...

Like
273
0
Tuesday, 21 October 2014
WHO: EBOLA YAANGAMIZWA NIGERIA
Global News

Shirika la afya duniani linatarajiwa kutangaza rasmi kuwa taifa la Nigeria halina ugonjwa wa bola baadae hii leo, wiki sita baada ya kutoripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo . Nchi giyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, alipokea sifa tele kwa hatua zake za haraka kukabiliana na Ebola baada ya mwanmadiplomasia Mliberia mwenye ugonjwa huo kwenda Nigeria mwezi Julai. Shirika la afya duniani lilitangaza Senegal kutokuwa tena na Ebola mnamo siku ya Ijumaa. Mlipuko unaoshuhudiwa wa Ebola, umewaua watu...

Like
265
0
Monday, 20 October 2014
« Previous PageNext Page »