WAZIRI wa Fedha Mheshimiwa SAADA MKUYA amewataka Watendaji wa Sekta ya Bima Nchini kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao kwa Wahanga wa ajali za Barabrani ambao wanazidi kuongezeka hivyo kuhitaji huduma ya haraka ya Kibima kutoka kwao. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mheshimiwa MKUYA amesema kumekuwa na ongezeko la ajali za barabarani ambazo zinazotokea kila sehemu jambo linalopelekea kupoteza Taifa la kesho ikiwa ni pamoja na watu kupata Ulemavu wa maisha kutokana na ajali hizo....
MAKAMU wa Rais Dokta MUHAMMED GHARIB BILALI amewataka Wataalamu wa Sheria katika taasisi ya mafunzo ya Sheria kwa vitendo nchini kusaidia kutoa huduma za msaada wa Kisheria kwa Watanzania wa hali ya chini wasioweza kumudu gharama za huduma hiyo ili kuongeza chachu ya haki kutendeka. Dokta BILAL ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa vitendo ambapo amewataka wahitimu wa taasisi hiyo kuutumia Weledi wao katika kusimamia haki nchini...
WAGOMBEA URAIS nchini Tunisia wamebishana juu ya matokeo ya uchaguzi wa Duru ya pili uliyofanyika hapo Desember 21 mwaka huu. Mwanasiasa wa muda mrefu BEJI CAID ESSEBSI amedai kushinda, lakini mpinzani wake, ambaye ni Rais wa sasa MONCEF MARZOUKI amekataa kukubali kushindwa. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa hii leo, huku Bwana ESSEBSI mwenye umri wa miaka 88 anaaminika kushinda asilimia 54 ya kura, akiwa mbele ya Bwana MARZOUKI kwa asilimia...
WATU WAWILI wamefariki dunia akiwemo raia wa Kenya SUZAN BHOKE baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani na mpenzi wake. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya LAZARO MAMBOSASA amesema SUZAN amefariki dunia baada ya kupigwa na kitu kizito na anayedaiwa kuwa mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la EDDY CLEMENT. Kamanda MAMBOSASA amebainisha chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi na kwamba CLEMENT anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji...
RAIS JAKAYA KIKWETE leo anazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo Hatma kuhusu Sakata la Akaunti ya Tegeta ESCROW inasuburiwa kwa hamu. Sakata hilo limezusha mshikemshike Bungeni ambapo tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji FREDRICK WEREMA amejiuzulu kutokana na kutajwa moja kwa moja. Mawaziri Profesa SOSPETER MUHONGO Nishati na Madini,Profesa ANNA TIBAIJUKA Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini ELIAKIMU MASWI pia wanatakiwa kujiuzulu au Mamlaka za uteuzi kuwaondoa. Awali ilidaiwa...
MWILI wa aliyekuwa mnenguaji wa bendi za Twanga Pepeta na Extra Bongo, Aisha Mohamed Mbegu maarufu Aisha Madinda unazikwa leo nyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es salaam. Mazishi hayo yalitarajiwa kufanyika jana, lakini yalilazimika kuahirishwa baada ya Jeshi la polisi kuzuia hadi hapo mwili wake utakapofanyiwa uchunguzi kutokana na utata wa kifo chake. Awali akizungumza na Efm, Mkurugenzi wa Asset, inayomiliki bendi ya Twanga pepeta, Asha Baraka amewataka watu wote kumwombea Marehemu Aisha ili mwenyezi mungu amlaze mahali pema...
WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amewataka wamiliki wote wa Viwanda nchini kutotupa ovyo taka zisizo tibiwa kwa dawa kwenye mito ya maji ili kupunguza athari zitokanazo na tatizo hilo kwa binadamu. Profesa Maghembe ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akizindua rasmi ripoti ya utendaji wa Mamlaka za maji za Mikoa na miradi ya maji ya Kitaifa ya mwaka 2013-2014, kwa lengo la kuboresha huduma za maji nchini. Katika uzinduzi huo pia amesema kuwa hali ya upatikanaji...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu, Desemba 22, mwaka huu. Wakati wa mazungumzo yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita. Awali kulikuwa na taarifa kuwa rais Kikwete angefanya mazungumzo hayo leo huku baadhi ya wadau na wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii...
MKUU wa Mkoa wa Lindi MWANTUMU MAHIZA amemshauri Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi Tanzania-TPSF Dokta REGINALD MENGI kuwaweka pamoja Wafanyabiashara katika sekta binafsi ili waweze kupata fursa zaidi za kibiashara nje ya nchi. MAHIZA ameeleza hayo wakati akipokea shukrani kutoka kwa Dokta MENGI kutokana na kuliwakilisha vema Taifa nchini China. Amebainisha kuwa alipokuwa China pamoja na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini pia amesaini mkataba kwa niaba ya Taasisi hiyo kwa lengo la kufanya biashara kati ya nchi hizo mbili....
RAIS JAKAYA KIKWETE leo anatarajiwa kuhutubia Taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam. Katika Mkutano wake huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine pia anatarajiwa kuzungumzia mwelekeo wa Taifa. Akizungumza na EFM Katibu wa Chama Cha Mapinduzi-CCM ABDALLAH MIHEWA amethibitisha kufanyika kwa mkutano huo....
WANAFUNZI 438,960 kati ya 451,392 waliofaulu katika mtihani wa darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 katika shule za sekondari za serikali Nchini. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa upande wa elimu KASSIM MAJALIWA alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.28 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.8 ikilinganishwa na mwaka jana ambao ilikuwa ni asilimia 96.3. Mheshimiwa MAJALIWA amesema...