UJENZI kwa ajili ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza unaendelea kwa kasi baada ya serikali kulipa kiasi cha fedha kwa mkandarasi. Imeelezwa kuwa Serikali imeshatoa Shilingi Bilioni Nne kwa Mkandarasi ambaye ni Kampuni ya BCEG ya China. Ukarabati unaofanywa ni upanuzi wa Uwanja wa kuongeza njia za kurukia ndege, jengo la kuongozea ndege na ghala la mizigo. Kiasi hicho cha fedha kinafanya fedha ambazo serikali imeshamilipa Mkandarasi kufikia Shilingi Bilioni 13. Meneja wa Uwanja huo ESTHER MADALE amesema...
MKUU WA MKOA wa Pwani Mwantumu Mahiza ametoa muda wa Wiki moja kwa watendaji wa Wizara ya Ardhi na Wizara ya Maliasili na Utalii kulipatia ufumbuzi suala la uvamizi wa Hifadhi ya Kazimzumbwi. MAHIZA ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kutembelea Hifadhi hiyo ambapo alifuatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo. Amebainisha kuwa hifadhi hiyo ipo hatarini kutoweka na kuvamiwa na watu walioweka makazi ya kudumu na kuendesha shughuli mbalimbali....
CHAMA cha Wananchi -CUF kimetishia kutofanyika kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa endapo Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa TAMISEMI haitabadilisha utaratibu waliouweka wa upigaji kura. Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu Bara Magdalena Sakaya amesema kuwa chama hicho hakitakubali kuona wagombea wao wanaenguliwa kulingana na mwongozo na kanuni za uchaguzi zilizopo ambazo tayari waliitaka TAMISEMI kuzirekebisha kwani zina mapungufu kwa wagombea na hata wapiga kura....
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imefanikiwa kujenga vyumba 17 vya maabara kwa shule zake sita za Sekondari kwa gharama ya shilingi 568.6 milioni. Hatua ya ujenzi wa maabara hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari nchini. Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa maabara kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima aliyekuwa Mwenyekiti wa Kikao...
JUMLA ya shilingi milioni tano zimetolewa na Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Abdul Azizi Mohamed Abood katika kikundi cha kuweka na kukopa cha Tutapambana Silk kilichopo Chamwino Mjini Morogoro kwa ajili ya kuendeleza kikundi hicho katika miradi mbalimbali ya maendeleo. Akipokea msaada huo Katibu wa kikundi hicho Omary Simbeye amesema kuwa fedha hizo zitawasaidia kuweza kuiendeleza miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kujenga ofisi na kukabiliana na changamoto mbalimbali za ukosefu wa ofisi katika kikundi hicho. Aidha amesema...
KITUO cha Kulea Wazee wasiojiweza cha Fungafunga kilichopo Manispaa ya Morogoro kinakabiliwa na tatizo la Umeme kwa takribani miezi miwili sasa na kuwafanya kuishi kwa shida bila kujua muafaka wao kutoka Serikalini. Akizungumza na EFM Mwenyekiti wa Wazee hao JOSEPH KANIKI ameeleza kuwa wamekuwa wakikatiwa Umeme mara kwa mara na Shirika la Umeme Tanzania –TANESCO kwa kutolipa bili kwa muda mrefu huku wakiamini Shirika hilo na Serikali wana mawasiliano mazuri. KANIKI amebainisha kuwa kukosekana kwa umeme kunawafanya kushindwa kujihudumia hasa...
MKURUGENZI wa Umoja wa Wakulima wa Chai Rungwe –RSTGA LEBI GABRIEL ameeleza kuwa Wakulima wa zao hilo wanatakiwa kutumia mbegu mpya zilizofanyiwa utafiti wa Kitaalamu ili waweze kupata mazao bora zaidi. GABRIEL ametoa kauli hiyo alipotembelea Shamba la Chai la Kimbila lililopandwa Mbegu mpya za Chai. Amebainisha kuwa Mbegu hizo mpya za kisasa zitamsaidia Mkulima kuondokana na umasikini pindi atakapoanza kilimo chenye tija kwa sababu zinazaa zaidi kuliko mbegu nyingine....
SHIRIKA la Posta TPC wamebadilishana makubaliano ya msingi waliyoyaingia na kampuni ya simu ya Zantel ya huduma mpya ya biashara iitwayo POSTGIRO leo jijini Dar es salaam. Huduma hiyo mpya ya kibiashara ya kukusanya na kulipa fedha kwa niaba ya kampuni, shirika, kiwanda au taasisi za serikali na binafsi itarahisisha ulipaji wa ada, amana, gawio, kodi, pensheni, michango na mishahara. Akizungumza na waandishi wa habari jiijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa TPC DEOS MNDEME amesema inaridhisha kutambua kuwa TPC...
Tanzania imekuwa kwa kiwango kikubwa katika usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za Mlonge hali iliyochangia soko la bidhaa hizo kuwa katika ushindani wa kibiashara. EILEEN KASUBI ni mkurugenzi wa kampuni ya MOKAI MORINGA MLONGE amesema bidhaa za mlonge zimekuwa zikiuzika zaidi katika masoko ya ndani na nje kutokana na kuwepo kwa wajasiriamali wengi wanaosindika mlonge ingawa watanzania wengi wahajapata elimu juu ya matumizi ya bidhaa hizo. Amesema wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za mlonge wanategemea zaidi masoko ya maduka makubwa na...
IMEELEZWA kuwa, ili kupunguza msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam Wizara ya Ujenzi imepanga kujenga Daraja la pili pembeni ya Daraja la Salenda litakalo gharimu zaidi ya fedha za kitanzania shilingi bilioni mia moja. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi Dokta JOHN MAGUFULI ameeleza kuwa Daraja hilo jipya litakuwa na uwezo wakupitisha magari zaidi ya elfu sitini kwa...
SERIKALI kupitia ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji imeshauriwa kuweka kipaumbele suala la uwekezaji katika sekta binafsi ili kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuwa sekta hiyo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika maendeleo ya Taifa. Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya uchumi ya bunge mheshimiwa LUHAGA MPINA wakati akichangia muswada wa marekebisho ya sheria baina ya sekta ya umma na sekta binafsi uliyosomwa kwa mara ya pili na Waziri wa nchi ofisi ya...